Friday, April 17, 2015

PICHA MBALIMBALI KATIKA HARAMBEE





Mmiliki wa Blog hii akizungumza na Meneja wa mgodi wa Dhahabu wa acacia wa Tarime, Mkoa wa Mara,Gary Chapman, kabla ya kufanyika kwa harambee ya uchangiaji wa maboresho ya hospitali ya Wilaya ya Tarime.

MGODI WA ACACIA WACHANGIA MILIONI 225



MENEJA wa mgodi wa Dhahabu wa Acacia GoldMine ya Tarime, Garry Chapman akitoa mchango wa Sh Milioni 225 katika harambee ya uchangiaji wa maboresho ya hospitali ya wilaya ya Tarime,iliyofanyika katika hotel ya CMG.

HARAMBEE TARIME MOTO


MKUU wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga akimtambulisha kwa wananchi, Mwenyekiti wa Kamati ya maboresho ya hospitali ya Wilaya ya Tarime, Peter Zakaria katika ukumbi wa CMG MOTEL, ambapo alichangia Sh Milioni 10, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya ya hospitali ya Wilaya hiyo, Daniel Komote,jumla ya Sh Milioni 281.4 zilichangwa.

MILIONI 229 ZAHITAJIKA UKARABATI HOSPITALI YA TARIME.

TARIME-MARA.

MKUU wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga amesema zaidi ya Sh. Milioni 229 zinahitaji kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Tarime ambayo inabiliwa na uchakavu wa miundo mbinu ya majengo pamoja na kuwa na uhaba wa madawa,mashuka na vyandaruaili kuondoa tatizo kubwa liliopo kwa sasa linalowakabili wananchi wa Wilaya hiyo na zingine pamoja na nchi jirani ya Kenya ambayo kwa kiwango kikubwa wanapata matibabu katika hospitali hiyo.

Kuhusu suala la madawa amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wa majengo atakikisha upatikanaji wa madawa unakuwa wa kuridisha kuliko ilivyo hivi sasa, hali ambayo imesababisha wananchi kutojiunga na mfuko wa CHF unaowataka kuchangia kiasi cha sh. 10,000 kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya maboresho Peter Zakaria ambaye alichangia Sh Milioni 10 alisema kuwa hatakubaliana na ujinga wowote kwa kwamba anaonea uchungu fedha za umma kuteketea bila kufanya kazi yoyote na kwamba atahakikisha anasimamia vyema ujenzi huo na kwa uadilifu mkubwa.

Katika harambee hiyo iliyoshirikisha watumishi wa Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, Mgodi wa Acacia wa North Mara na watu binafsi jumla ya Sh Milioni 281.4 zilichangwa kupitia Akaunti ya benki ya NMB uboreshaji wa hospitali ya Wilaya ya Tarime N0.30410011011 , mashuka 50, madawa na vyandarua.
Hospitali ya Wilaya ya Tarime ilianzishwa mwaka 1956 ikiwa n alengo la kuhudumia wilaya hiyo na viunga vyake ambapo ilitoa huduma kwa kiwango cha Zahanati lakini kwa sasa idadi ya watu imeongezeka na inahitaji watumishi wengi ili kuweza kuendesha huduma hiyo ipasavyo.





Monday, February 23, 2015

DC-TARIME akiwa na RSO



katikati ni afisa Usalama Mkoa wa Mara.

GLORIOUS LUOGA-DC TARIME


MKUU wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga akipokea vitendea kazi.



MKUU wa wilaya ya Tarime akisaini kiapo.

Akiwa na mkewe, Mrs Stella Nyandindi mara baada ya kuapa.

Wakuu wa Wilaya,katika Mkoa wa Mara, wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kuapa, hapa ni bustani ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

DC MPYA TARIME AKILA AKIPO CHA UTII


MKUU wa wilaya Mteule,Glorius Bernard Luoga akila kiapo cha utii,kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Aseri Msangi katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Wednesday, February 4, 2015

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, ZIARANI.



ISIBANIA.






Jengo lenye rangi ya ugoro ni la kenya.

WATANZANIA, wametakiwa kuchangamkia fursa za kufanya biashara nchi jirani ili kukuza kipato chao na si kukaa na kulalamika kama ilivyo sasa.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Amantius Msole alipokuwa akizungumza na wafanyabiahara wadogo wadogo katika mpaka wa Tanzania na Kenya (Sirari) Mkoa wa Mara.

Amesema watanzania wanapaswa kufahamu juu ya Umoja wa Afrika Mashariki na kujua sheria zake ili wapate fursa za kufanya biashara na kwamba wawe tayari kufanya ushindani wa biashara kabla ya nchi nyingine kuingia ndani na kufanya biashara ambazo wao wanaweza kufanya.


“Nashangaa kuona hata maji ya kunywa, tunakunywa kutoka nchi ya Kenya na Uganda na huku tuna viwanda vingi nchini kwetu vyenye ubora ule ule, kwa hilo tu unaweza kuona wafanyabiashara wenzetu wamechangamkia fursa hii, pia sisi watanzania tumekuwa na kasumba ya kutopenda bidhaa zinazotengenezwa nchini kwetu,tuweni wazalendo” Alisema Msole.

Amesema kuwa katika ziara yote ya kutembelea maeneo ya mipaka kote nchini amegundua kuwa watanzania wengi hawajapata elimu juu umoja wa Afrika Mashariki na fursa ambazo wanaweza kuzitumia ili waweze kufanya kazi kwa pamoja, hivyo ameagiza wadau wote wanaohusika kutoa elimu haraka iwekezanavyo ili waweze kunufaika na umoja huo.



Akizungumza na Naibu Katibu Mkuu, Ofisa wa Mapato wa Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA), Kingori Mwangi alimweleza kuwa kwa upande wa Kenya, jengo la Mamlaka yao limeishakamilika kwa kiasi kikubwa na kwamba lina eneo la wanyama kama Ng’ombe, Mbuzi Kondoo na ndege aina ya Kuku(Animal Holding), ambapo wafanyabiashara wa Tanzania wanapofika wataweka mifugo yao tayari kwa kukaguliwa na kusafirisha nchini Kenya kwa kuuza.

Amesema kuwa kwa upande wa vyumba mbalimbali vilivyokamilika amesema kuwa vyumba vingi muhimu vimekalimika vikiwemo vya kukagua bidhaa zinazofaa na zenye sumu (Poison and Health Room), X-ray Chumba cha kuteketeza madawa yasiyofaa yanaoingia mpakani mwa Tanzania na Kenya (Incinerator), chumba cha kuifadhia samaki,chumba cha mbwa wa upelelezi wenye uwezo wa kunusa wezi, sumu, madawa ya kulevya na kadhalika ambalo litakabidhiwa mwezi feburari mwaka huu, huku jengo la Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) bado halijakamilika.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na viongozi wake wote kutoka Wizarani walifanya ziara katika Mikoa iliyoko mipakani, Mtukula, Sirari, Kabanga, Namanga na Hororo kwa lengo la kujifunza na kuhamasisha wananchi kuchangamkia fursa za biashara.