Thursday, January 19, 2017

MKOA WA MARA UNA UPUNGUFU WA CHAKULA

MUSOMA-MARA.

SERIKALI Mkoani Mara inawadhibitishia wananchi kuwa hakuna tatizo la ukosefu wa chakula kutokana na akiba iliyopo ya tani 461,000 ya ziada ya chakula iliyovunwa kwa mvua za vuli za mwaka 2015 /2016 pamoja na hayo Mkoa wa Mara una jumla ya idadi ya watu Milioni 1,700,000 na ifikapo Disemba inakadiliwa kuwa na watu Milioni 2, ambapo Mkoa unajitosheleza kwa tani 544,525 kwa mwaka mzima hivyo Mkoa una upungufu wa jumla ya tani 83,525.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mkuu wa mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa amesema kuwa pamoja na hali ya mvua za vuli kutokuwa nzuri lakini jumla ya tani 953,000 zilivunwa baada ya kulima ekari asilimia 42.

Dk. Mlingwa amesema kuwa ziada ya chakula ya tani 461,000 zilizopo mkoani hapo zina uwezo wa kujilisha mwaka mzima kwa kufikia mwezi mei hadi Agosti mwaka huu maana hata mvua za masika za mwaka 2016 kwani katika wilaya za Tarime ,Rorya, Serengeti na Butiama ambapo jumla ya tani 953,000 zilivunwa.



Amesema kuwa kutokana na asili ya watu wa mkoa huo kutumia nafaka aina mahindi , Mhogo na Mtama wamekuwa na dhana kuwa kunapotokea upungufu wa nafaka hizo wanadai kuna njaa wakati wanao uwezo wa kutumia nafaka nyingine kama vile mchele kwa kusaga unga wake na kusonga ugali pamoja na vyakula vingine kama vile viazi mbatata ,ndizi na vinginevyo.

Aliongeza kuwa mkoa ulikuwa na lengo la kuzalisha tani milioni 1,864,900 lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa lengo hilo halikuweza kufikiwa ambapo ekari 280,000 zilitarajiwa kulimwa na kuzalisha mavuno ya tani 760,000 kama hali ingekuwa ya hewa ingekuwa nzuri.


Mpango kabambe wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji umeandaliwa, ambapo kila halmashauri zimetakiwa kuandaa bajeti ya mradi huo kwa mwaka 2016/2017.



Sunday, January 1, 2017

TATIZO LA UVAMIZI WA TEMBO KUTOWEKA


SERENGETI.


SERIKALI kupitia wizara mbalimbali itaangalia upya uwezekano wa kutatua matatizo ya uvamizi wa wanyama aina ya Tembo wanaoharibu mazao ya wananchi.

Naibu Waziri wa Mali asili na Utalii, Mhandisi, Ramo Makani aliyasema hayo katika uwanja wa ndege wa Ikorongo baada ya kumaliza ziara yake katika Wilaya ya Serengeti, kutokana na hali asili aliyoina serikali kupitia Wizara zote nne itaangalia uwezekano wa kuangalia na kupitia upya na kuweka mikakati ya kuzuia wanyama hao wasiharibu mazao ya wananchi.

''Tuna Wizara zinazohusika na masuala mbalimbali, ikiwemo,ya Ardhi, Mifugo, Maliasili, na nyingine tutakaa kwa pamoja kuangalia changamoto zilizopo,nimeona kuna watu wanaishi kihalali na ni vijiji vilivyopo kwa mujibu wa sheria vinapakana sana na mapori ya akiba ya Ikorongo na Grumeti ambavyo kwa sasa vimekuwa vimekuwa vikivamiwa mara kwa mara’’Alisema Makani.
Akiwa katika kijiji cha Makundusi Wilaya ya Serengeti kinachopakana na mapori ya akiba alishuhudia wanyama hao walivyobomoa nyumba katika tukio lilitokea oktoba mwaka jana na kusababisha madhara makubwa ya kuhama kwa familia mbili ikiwemo ya Malimi Nyamuhanga yenye jumla ya wakazi 10 na nyingine ambapo wanyama hao walikula chakula chote kilichokuwa ndani ya nyumba.

Alisema kutokana na wananchi kuishi katika njia za mapitio ya wanyama(shoroba) na mabadiliko ya wanyama kwa kuvamia majumba ya watu na kula chakula na kuvamia mashamba ni jambo jipya ambalo linatizamwa kwa upana wake.

Akizungumza katika majumuisho ya ziara hiyo katika ofisi za pori la akiba la Ikorongo,Afisa wanyamapori Wilaya ya Serengeti, John Meitamei (DGO) alisema kuna ongezeko kubwa la wanyamapori aina ya Tembo,na wao kuwa na tabia ya kukumbuka walikotokea, mabadiliko ya tabia nchi, kumesababisha waingie katika maeneo ya wakazi na kusababisha madhara, hivyo wanaiomba serikali kunusuru wananchi wasipate matatizo.

Alisema kuwa wameweka mikakati mbalimbali ya kunusuru ikiwemo ya ujenzi wa uzio wa umeme ili wanyama hao wasiingie kwenye makazi ya watu pia wameiomba Wizara kuongeza vitendea kazi yakiwemo magari ya kuweza kufanya doria ya mara kwa mara ili wananchi waweze kuvuna mazao yao na kuunda kikosi kazi cha ulinzi kitakachoshirikiana na wananchi.

Akiwa katika kijiji cha Mugeta Wilaya ya Bunda katika mkutano wa hadhara, wananchi hao walimwomba Naibu Waziri huyo kuwasaidia chakula cha njaa haraka, ili kuwanusu na njaa kwani kwa sasa debe moja la mahindi linauzwa Sh.21,000 na kwamba endapo Serikali hatachukua hatua za makusudi debe la mahindi wiki ijayo litafikia sh.40,000.

Aliagiza kikosi dhidi Ujangili (KDU) na magari yaliyokuwa yakilinda mwaka wa juzi yaanza doria na vikundi vya ulinzi vya vijana viundwe na vitambuliwe na Serikali ili viendelee kulinda katika kijiji cha Maliwanda Wilayani humo ambapo alitoa tochi zipatazo 200 kwa ajili ya kufukuzia wanyama hao.








LADY DJ DEE KUTUMBUIZA DREAM GARDEN-MUSOMA.



MWANAMUZIKI mahili kutoka Mkoa wa Mara, Lady Jay De usiku huu anatoa Burudani kabambe katika Resort ya Dream garden iliyopo katika Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara ambapo atawaburudisha wakazi wa Mkoa wa Mara.

Hapa niko na Mkurugenzi wa Resort hiyo Abbas Chamba ambaye amesema kuwa huduma kubwa itatolewa katika bar hiyo ambayo kwake ameitaja kuwa ni ya aina yake katika Mkoa na Manispaa na yenye sifa kwa kuwa iliweza kujumuisha wagenii wa kitaifa katika Mkutano mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ALAT mwaka ulioisha ambapo tuzo ya kimataifa ya Tanzania Mayors Award ilifanyika katika ukumbi huu.


Mwaka mpya huu utawafurahisha wakazi wa Mkoa wa Mara waishioo nje na ndani ya nchi kupata burudani ya kipekee kwa kuwa watajumuika na mwimbaji wa kitaifa na kimataifa wa nyimbo za Kiswahili ambaye pia Mkoa wa Mara ndio makazi yake rasmi kwa kuwa ni mzaliwa wa Mkoa huu.

Lady Jay Dee atatumbuiza nyimbo zote alizoziiimba mwaka wa jana ukiwemo 'Ndi, Ndi, Ndi, ulio na washabiki wengi ncbi na nyingine za zamani.

Nao washabiki wa muziki wake bila kutaja majina wamesema kuwa ni mwanamziki anayefaa, na kumtaka achukue wanaziki wengine wenye uwezo ambao wapo katika Mkoa huu, akisemo mwimbaji mwenye sauti mithili ya Kasuku, Abdalla Ukwaju anayeibia bendi ya Magereza ya Mkoa wa Mara.