MUSOMA-MARA.
SERIKALI Mkoani Mara inawadhibitishia wananchi kuwa hakuna tatizo la ukosefu wa chakula kutokana na akiba iliyopo ya tani 461,000 ya ziada ya chakula iliyovunwa kwa mvua za vuli za mwaka 2015 /2016 pamoja na hayo Mkoa wa Mara una jumla ya idadi ya watu Milioni 1,700,000 na ifikapo Disemba inakadiliwa kuwa na watu Milioni 2, ambapo Mkoa unajitosheleza kwa tani 544,525 kwa mwaka mzima hivyo Mkoa una upungufu wa jumla ya tani 83,525.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mkuu wa mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa amesema kuwa pamoja na hali ya mvua za vuli kutokuwa nzuri lakini jumla ya tani 953,000 zilivunwa baada ya kulima ekari asilimia 42.
Dk. Mlingwa amesema kuwa ziada ya chakula ya tani 461,000 zilizopo mkoani hapo zina uwezo wa kujilisha mwaka mzima kwa kufikia mwezi mei hadi Agosti mwaka huu maana hata mvua za masika za mwaka 2016 kwani katika wilaya za Tarime ,Rorya, Serengeti na Butiama ambapo jumla ya tani 953,000 zilivunwa.
Amesema kuwa kutokana na asili ya watu wa mkoa huo kutumia nafaka aina mahindi , Mhogo na Mtama wamekuwa na dhana kuwa kunapotokea upungufu wa nafaka hizo wanadai kuna njaa wakati wanao uwezo wa kutumia nafaka nyingine kama vile mchele kwa kusaga unga wake na kusonga ugali pamoja na vyakula vingine kama vile viazi mbatata ,ndizi na vinginevyo.
Aliongeza kuwa mkoa ulikuwa na lengo la kuzalisha tani milioni 1,864,900 lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa lengo hilo halikuweza kufikiwa ambapo ekari 280,000 zilitarajiwa kulimwa na kuzalisha mavuno ya tani 760,000 kama hali ingekuwa ya hewa ingekuwa nzuri.
Mpango kabambe wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji umeandaliwa, ambapo kila halmashauri zimetakiwa kuandaa bajeti ya mradi huo kwa mwaka 2016/2017.
No comments:
Post a Comment