Saturday, February 18, 2017
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AMEUFUNGA MGODI WA DHAHABU WA BUHEMBA.
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameufunga mgodi wa dhahabu wa Buhemba kutokana na kutokithi vigezo vya uchimbaji wa madini kutokana na maafa ambayo huwa yanatokea katika mgodi huo mpaka pale taratibu za kisheria zitakapokamilika.
Akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo wa madini katika eneo la Irasanilo kijiji cha Biatika kata ya Buhemba kitongoji cha Ikoma ‘B’ Wilaya Butiama Mkoani Mara alisema kuwa serikali inapata hasara kubwa katika kutoa misaada mbalimbali yanapotokea majanga.
Aidha ametoa agizo kwa Shirika la Madini Taifa (STAMICO) na Wizara ya Nishati na Madini kupima eneo ili kujua lina ukubwa kiasi gani sambamba na kuweka mipaka ya eneo hilo(Beacon) ili kuweza kuwakabidhi wachimbaji wadogo wadogo kuendesha kazi ya uchimbaji katika eneo hilo.
Kamishina wa madini, Lucas Mlekwa alisema kuwa STAMICO inafanya utaratibu wa kuwagawia eneo hilo wachimbaji hao na kwamba taratibu zinafuatwa ili kuwakabidhi eneo hilo na kuhakikisha wachimbaji wengine ambao hawana maeneo wanapata na sio kuwamilikisha wachimbaji wale wale.
Katika ajali ya iliyotokea februari 13 mwaka huu,Samrya Zablon ambaye ni mmilikiwa eneo hilo alimdhibitishia Waziri Muhongo kuwa jumla ya wachimbaji wapatao 18 walikuwemo katika shimo hilo na kati ya hao 17 walijorodhesha majina yao na mmoja hakujiorodhesha jina wakati anaingia, lakini alitambuliwa na kwamba watatu walipoteza maisha, akiwemo Joseph Salige,Babuu Okungu wa Wilaya ya Rorya ambao miili yao imepatikana na maziko yamefanyika na Peter James(31). ambaye amenaswa hajapatikana na jitihada za uokoaji zinaendelea.
Uokoaji katika mgodi huo unaendelea kufanyika kwa kushirikiana na mgodi wa North Mara ambao wameleta wataalamu na vifaa vya uokoaji, Jeshi za zimamoto, Msalaba mwekundu, Polisi, Mgambo na wachimbaji wa eneo hilo ambapo Baba mzazi wa marehemu huyo James Matiko alithibitisha kuwa mnamo februari 13 mwaka huu mwanae Peter James aliingia kwenye duara hilo lakini mpaka sasa hajaonekana ambapo aliiomba ushirikiano ili mwanae aweze kupatikana na taratibu za maziko zifanyike.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment