Sunday, February 19, 2017

ANNE MAKINDA ASEMA MFUKO WA NHIF UTOE HUDUMA BORA.



MWENYEKITI wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Mheshimiwa Anne Makinda amesema kuwa endapo mfuko wa bima ya afya utatoa huduma nzuri watanzania watakuwa na afya bora,hivyo ni vyema kujenga mfuko huo kwa kutoa huduma bora zinazowaridhisha wateja kwani ndio mkombozi kwa watanzania na kumekuwapo na tabia za baadhi ya wauguzi na madaktari kuwa kikwazo pindi wanapotakiwa kuhudumia wagonjwa wanaotibiwa kwa mfuko huo hali inayowalazimu wananchama kwenda kupata huduma ya matibabu katika maeneo mengine na kuwataka watanzania kubadilika.

Amewataka watoa huduma kuwa na moyo wa unyenyekevu wakati wanapohudumia wagonjwa na sio kuwatolea matusi na kejeli na endapo atabainika atachuliwa hatua za kinidhamu kwani wakifanya hivyo nikuchafua mfuko wa Bima.

Aidha uongozi wa bodi hiyo pia umeonesha kusikitishwa na tabia za baadhi ya wauguzi na madaktari wanaouhudimia wagonjwa katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za serikali kuwabagua, kuwanyanyasa na kuwajibu kwa lugha za matusi wagonjwa wanaopatiwa matibabu wanaofika kutibiwa kupitia mfumo wa kadi zinazotolewa na mfuko huo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk. Charles Mlingwa aliwakemea vikali madaktari wa zahanati, vituo vya afya na hospitali zote za serikali na kuwataka kuzingatia usawa na maadili pindi wawapo katika majukumu yao na yeyote atakayeenda kinyume hatua za kinidhamu zitachukiliwa dhidi yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa mfuko wa bima ya afya wakalalamika upungufu wa watumishi katika vituo vya serikali na kumwomba mwenyekiti huyo alete watumishi katika vituo hivyo ili wananchi waweze kunufaika na mfuko wao.

Mchungaji Musa Marwa ambaye ni mtoa huduma alisema kuwa kuna tatizo kubwa katika kutoa huduma kutoka serikalini na kwamba wamebaki kulalamika kila siku lakini utekelezaji wake umekuwa mgumu kuwarekebisha wahudumu wa afya kwa kuwa wana lugha chafu katika kuwahudumia wagonjwa.


Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Musoma vijijini, Frola Yongolo amesema endapo kuna uwezekano wa kutoa mikopo kutoka katika mfuko huo ni vyema apewe mkopo wa kufanya ukarabati wa majengo katika eneo lake vikiwemo vitendea kazi na samani.

Kaimu Mkurugenzi wa Bima ya Afya (NHIF),Bernard Konga Changamoto huduma zisizorithisha kutoka kwa wananchi, msongamano mkubwa wa wagonjwa,unyapaa kwa wanachama wa bima ya afya,vituo vyingi vya serikali vina upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma,madai kutoka kwa watoa huduma kuwa na utata ambao umekuwa na udanganyifu ambalo si jambo zuri kwa mstabali wa mfuko wa bima hivyo ni vyema serikali ikawa na chombo cha uthibiti wa madawa kama EWURA walivyo.

Akijibu hoja za watoa huduma kuhusiano na dawa ambazo zinazosema hazipo kwenye bima amesema kuwa wao wanatoa kufuatia mwongozo wa serikali na juu ya suala la kadi za wanachama zitakuwa zinapatikana kikanda ambapo kanda za Mwanza, Mbeya, Arusha na Dodoma zimeundwa na kuhusu ya madai ya malipo ya watoa huduma taratibu zifanywa ili waweze kulipwa.






No comments:

Post a Comment