Saturday, April 15, 2017
Profesa Muhongo awataka wananchi kuzingatia elimu
MUSOMA.
MBUNGE wa Jimbo la Musoma vijijii na Waziri wa Nishati na Madini Pro. Sospeter Muhongo amewaomba wananchi kuweka jitihada kubwa katika sekta ya elimu kwani ndio pekee itakayoleta manufaa katika kukuza uchumi wa familia na Taifa.
Ameyasema hayo jana katika kijiji cha Bugoji, Muhoji na Chumwi katika ziara yake ya kukgua ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuongea na wananchi katika mikutano ya hadhara ambayo ilifanyika katika shule za msingi za Kanderema .
Aidha amewataka wananchi kutobakia kulalamika badala yake waongeze bidii katika utendaji wa shughuli za maendeleo ikwemo kilimo ili kuweza kuondokana na matatizo mbalimbali ya maisha.
Licha ya hayo akizungumzia juu ya mradi wa maji , aliwaeleza wananchi kuwa katika miradi mingine kama vile maji inasimamiwa na halmashauri na kwamba serikali inafanya kazi kwa mpangilio hivyo madiwani ndio wanapaswa kusimamia suala la maji kwa kuweka katika vikao vyao ili atakaposhughulikia suala hilo iwe rahisi.
Akizungumzia suala upungufu wa chakula amesema ni aibu sana kusema kuwa mna njaa huku mnazungukwa na ziwa,sisi ndo tungekuwa watu wa kwanza kusambaza chakula katika mikoa mingine, lakini kwa sasa ni tofauti, tunaomba chakula kutoka mikoa ya Mbeya,tubadilike kutoka kilimo cha kutegemea mvua na sasa tulime kilimo cha umwagiliaji, kwani shamba kama la Bugwema lipo na halitumiki’’ Alisema Muhongo.
Naye katibu wa Mbunge wa jimbo hilo Ramadhan Juma alisema Pro. Muhongo amekwishaleta vifaa vya ujenzi ambapo jumla ya mifuko ya saruji ipatayo 1269 na mabati 5120 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa shule za msingi 111 na sekondari 20 ambapo mgawanyo wa saruji katika ukanda wa Bukwaya shule 13 kati shule 18 ,ukanda wa mugango 13 kati ya 24, ukanda majita 40 kati ya shule 69.shule 4,majita shule 2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment