Friday, April 28, 2017
WAZIRI LUKUVI AGAWA HATI MILIKI
SIMIYU
WAZIRI Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amewakabidhi wakazi wa mji mdogo wa Lamadi Wilaya Busega Mkoa wa
Simiyu hati miliki za viwanja na kuagiza kuvunjwa kwa nyumba
zitakazojengwa kiholela mara baada ya kukamilisha mpango kazi
kabambe(Master Plan) katika Wilaya hiyo.
Zoezi hilo lililofanyika katika viwanja vya mikutano vya stooni ,
Lamadi wilayani humo lililoshuhudiwa na wananchi, huku akitoa elimu
kwa wananchi walioonekana kuhamasika kuwa na makazi bora mara
watakapopata hati miliki ili waweze itakayowawezesha kukopa na
kufungua biashara zao na kuondokana na umasikini.
Alisema kuwa lengo la serikali la kufanya urasimishaji huo ni
kuwataka wananchi kuweza kupata hati zitakazowasaidia kukopesheka
kwenye mabenki ili kujikwamua kiuchumi .
‘’Rais ameniagiza kuja kurasimisha ili wananchi muweze kupata makazi
yaliyo bora na ili kuondokana na makazi holela na kupata hati miliki
za viwanja ili muweze kukopesheka,ukiwa na hati unakuwa umefunga ndoa
ya halali ambayo ni mkataba halali na serikali ambao utakuwa unalipia
kodi ya ardhi kila mwaka na bila kubugudhiwa na Mkuu wa Wilaya au
Mtendaji wa kata’’. Alisema Lukuvi.
Aidha amewataka wananchi kutumia fursa ya hofa ya punguzo ya kulipia
asilimia 2 iliyotolewa na Rais Dk. John Magufuli katika kufanya
urasimishaji wa mpango kazi kabambe(Master Plan ) ili kuendeleza mji
huo kuwa wa kibiashara ambayo kufikia Juni 30 mwaka huu ndio mwisho
na kuweza kupata hati miliki.
Aliongeza‘’Kuna nyumba nyingi ambazo zimejengwa kiholela lakini rais
ametoa hofa rasmi ambapo leo nimekuja kutoa hati 122 kwa atakae ipata
ndio dhamana itakayomwezesha aweze kukuza uchumi wake ambao ni mtaji
wa maendeleo na kuondokana na umaskini’’.
Akiongea kwa hisia kali alisisitiza‘’ Serikali haiwezi Kuja
kuhalalisha maovu tu kila siku na kurasimisha na kutoa hati kwa
makosa yanayofanyika hivyo tumieni hofa hiyo mliyopewa ili
kuhakikisha wananchi wote wa mji wa Lamadi mnafanya urasimishaji wa
kupata makazi yaliyo bora, ili mpima atakapokuja asilazimike kuvunja
nyumba ili uweze kujenga nyumba upya,lakini kwa hawa waliopata
hati,mpango kazi ukija na ikalazimika eneo lile aidha ni barabara
inapita,italazika alipwe,lakini kama hiyo nyumba utakuwa umejenga bila
kibali itavunjwa hata kama umejenga ghorofa.’’Alisisitiza Lukuvi.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Busega Anderson Mbiginya akisoma
taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo alisema katika kipindi cha
kuanzia oktoba 2016 hadi sasa halmashauri hiyo imefanya upimaji wa
awali wa miundombinu ikiwemo ya shule, zahanati, malambo, majosho na
mabanio ipatayo 102 kati 180 sawa na aslimia 56.67na kufanya
urasimishaji wa makazi yanayoendelezwa kiholela na kutambua miliki
imekamilika kwa kupata viwanja 5,223 na upimaji wa awali viwanja
4,950.
Alisema umilikishaji wa viwanja ulianza Aprili mwaka huu katika eneo
la Lamadi ambapo hadi sasa hati 138 zimeandaliwa na kati ya hizo 122
zimekamilika na zimekabidhiwa .
Alisema kuwa kupitia urasimishaji serikali imefanikiwa kuongeza
mapato yatokanayo na tuzo na huduma za ardhi kwani zaidi ya shilingi
milioni 22.3 zimekusanywa katika kipindi cha wiki mbili na inakadriwa
kuwa shilingi 315 .4 zitakusanywa ikiwa viwanjwa 1,934 vilivyokamilika
kupimwa vitamilikishwa.
Alisema kuwa licha kuwa na mafanikio hayo kuna changamoto
zinazowakabili ambazo ni umbali mrefu wa upatikanaji wa huduma ya
baraza la Ardhi wilaya ambapo kwa sasa wananchi wanapata huduma ya
baraza la ardhi wilaya ya Maswa ambako ni wastani wa km 150 na
darubini ya kupimia (Total Station).
Nao baadhi ya wakazi wa eneo hilo waliopata hati waliishukuru serikali
kwa kuwaletea huduma hiyo kikanda ambapo kwao ilikuwa ni ndoto.
Akizungumza na gazeti hili, Mkazi wa mji mdogo wa Lamadi, ambaye ni
mwanamke,Lyabubi Gatulwa Mkelebe ambaye alichukua hati 3 alisema hati
hizo atatumia kwa kuweza kukopa benki ili aweze kuongeza hekali 50 za
kulima mpunga kwa njia ya kisasa ambapo kwa sasa ana heka 13 za
mpunga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment