Friday, April 28, 2017

MUSOMA YAWA YA KWANZA KUKAMILISHA MASTER PLAN.

MUSOMA

WAZIRI Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amepiga marufuku ujenzi usio na utaratibu ulio nje ya mpango kazi
kabambe(Master Plan) wa 2015-2035 uliozinduliwa jana katika Manispaa
ya Musoma ambao utagharimu kiasi cha Sh. Bilioni 15 ikiwa na pamoja na
miundo mbinu.

Alisema pia kuwa ni marufuku wananchi kujenga bila kuwa na kibali cha
ujenzi kutoka katika halmashauri za miji, mji na Manispaa na kwamba
watavunjiwa nyumba zao bila kulipwa fidia yoyote.

Aidha aliagiza uongozi wa Manispaa, kitengo cha mipango miji
kuhakikisha inatumia mpango kazi huo na kutumia wataalamu wazalendo
kwa kuwapatia ushauri wa kitaalamu endapo kutakuwa na utata.

‘’Ni marufuku Wizara ya Ardhi kutumia wataalamu kutoka nje kutupangia
mji, zitumike kampuni za kizalendo,kwani tumetumia gharama kubwa
katika kupanga mji wa Mwanza na Arusha kwa kuweka kampuni za kizungu
kwa kiasi cha zaidi ya Bilioni 22, lakini katika kupanga Master Plan
ya halmashauri ya Manispaa ya Musoma kampuni ya kizalendo ya upimaji
CRM Land Consultant zimetumika Sh Milioni 288 na kazi ni nzuri na ni
kitaalamu.

Alisema kuwa serikali iko tayari kuwajengea uwezo kampuni za kizalendo
ili kuweza kupanua wigo wa wataalamu wa nchini ili kupunguza gharama
zisizo za lazima na kuongeza kazi ya urasimishaji ili mji ukae katika
Madhari nzuri.

Amewaagiza watendaji wa mitaa kusimamia kuendeleza miji kwani mji
umepangwa upya kwa kuweka masharti ya uendelezaji wa ujenzi na sio
kufanya kazi moja ya ukusanyaji wa mapato kwani rasilimali zilizopo
zikitumika zitasaidia kukuza uchumi na kutoa hati kwa wananchi ili
ziwasaidie kuchukua mikopo itakayowasaidia kufungua biashara kubwa
ambayoo itawaingizia halmashauri mapato.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manipaa hiyo Joseph Masero alisema kuwa
Manipaa ya Mji wa Musoma ilipata hadhi ya kuwa Manipsaa mwaka 2005 na
mchakato wa kupata mpango kazi kabambe ulianza mwaka 2013 ambapo
Manispaa ndiyo ya kwanza nchini Tanzania kuwa na mpango kazi kabambe
(Master Plan).

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Vicent Naano alisema kuwa mpango kazi huo
utasaidia kuondoa ujenzi holela ili Manispaa iweze kupata eneo la
ujenzi wa viwanda ili kutekeleza Ilani ya CCM na sera ya serikali ya
kuwa na kuwa na viwanda na kuondoa tatizo la ardhi.


Aidha Profesa John Lupala Mkurugenzi alisema kuwa mara baada ya
kurekebishwa kwa sheria mbalimbali za ardhi mipango ilianza kufanywa
kwa kuanza kuandaa mipango iliyoandaliwa ni 26 katika miji 18
lakini kati ya miji hiyo ni Manispaa ya Musoma pekee ndiyo
imekamilisha mpango kazi (Master Plan).

Mtaalamu Mshauri wa kampuni ya mpango kazi kabambe ya (CRM Land
Consultant),Clara Kweka Msale aliwapongeza wataalamu walioshirikiana
nae kuhakikisha wanapanga mji huo ambapo kazi hiyo ilishirikisha
wadau wote.

No comments:

Post a Comment