Friday, May 6, 2011

UJUE UPANUZI WA MIJI (MADA)

UPANUZI NA KUKUA KWA MIJI

By: MAJURA, MCW
AFISA MIPANGOMIJI MKUU
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI


MTILIRIKO WA MAWASILISHO
• .
TAFSIRI AU MAANA YA MIJI (MAKAZI - HUMAN SETTLEMENTS)
• 2. KILICHOMO AU KINACHOFANYA MIJI
• 3. HAJA YA UWEPO WA MIJI
• 4. NGAZI MBALIMBALI ZA MIJI KINADHARIA
• 5. HATUA MBALIMBALI ZA MAKUZI YA MIJI
• 6. SABABU ZINAZOLETELEZA MIJI KUKUA
• 7. FAIDA ZA MIJI KUKUA
• 8.SHERIA, SERA NA KANUNI ZINAZOSIMAMIA MAKUZI NA MAENDELEZI YA MIJI NCHINI
• 9. TARATIBU ZA KUFUATA KATIKA KUPANUA MIJI KWA MUJIBU WA SHERIA NA NJIA MBADALA ZINAZOWEZA KUTUMIKA KUIPANUA
• 10. HITIMISHO.

TAFSIRI YA MJI
• 1. Mji au makazi ya watu ni sehemu yenye mkusanyiko wa watu na shughuli zingine zinazoendana na uendeshaji ya mikusanyiko hiyo ili kuiwezesha kujiendesha bila kuathiri uwepo wake.
• 2. Dhana ya mji endelevu inayopigiwa chepeo siku hizi na wataalamu mbalimbali inatokana na kutambua kuwepo kwa shida zitokanazo na uharibifu wa mazingira ukisukumwa na ubinafsi uliokithiri wa wanadamu wa leo ambapo kila mmoja anataka kujinufaisha pekee yake kadri inavyowezekana.

NINI KILICHOMO MIJINI
Ili mji uweze kuonekana na kufanya kazi za kimji unatakiwa uwe na shughuli zifuatazo (au baadhi yake) aghalabu kwa uwiano fofauti tofauti kulingana na kusudi la kuanzisha mji husika:
1) ViwandaSehemu ya kuishi watu (makazi halisi)
2) Huduma za umma (maofisi mbalimbali)
3) Burudani (michezo, maeneo ya wazi, makaburi nk.
4) Biashara nk.

HAJA YA KUWEPO KWA MIJI
Ø Miji ni vitovu vya ustaarabu na kuchochea maendeleo (vyuo vya mafunzo na utafiti)
Ø Miji husaidia kuwahifadhi watu wengi kwa pamoja katika eneo moja kwa madhumuni maalumu kama kambi ya wafanyakazi katika viwanda, ofisi na kutoa huduma kulingana na shughuli kuu
Ø Miji pia imetumika kwa nyakati mbalimbali katika historia kama ngome ya kulinda watu dhidi ya maadui nk.

NGAZI ZA MIJI KINADHARIA (Hierarchy of Settlements):
Makazi au miji inagawanywa katika makundi mbalimbali kufuata vigezo tofauti tofauti
u Vitongoji (hamlets)
u Vijiji (villages)
u Miji Midogo (Trading Centres)
u Miji (Towns) Manispaa (Municipalities)
u Majiji (Cities)
u Metropolitans
u Mkusanyiko wa majiji chini ya uongozi mmoja (Mega Cities).



HATUA MBALIMBALI ZA MAKUZI YA MIJI
Miji yote, isipokuwa michache iliyoanzishwa kwa makusudi na kwa kutumia nguvu, raslimali maalumu na misukumo ya kisiasa, inapitia katika taratibu, mifumo na mielekeo inayofanana. Hapa inamaana kwamba karibu miji yote huanza kama vijiji, miji midogo na hatimaye kufikia hadhi kubwa za nyakati hizo

SABABU ZINAZOLETELEZA MIJI KUKUA
Kuna sababu nyingi zinazosukuma miji kukua:
Ongezeko la watu wanaokaa katika mji husika
Maamuzi ya kisiasa kuipanua au kuanzisha miji fulani kwa makusudi maalum
Kuongezeka kwa shughuli (biashara, viwanda au kupatikana kwa miundombinu madhubuti kama reli na barabara) nk.


FAIDA ZA MIJI KUKUA
Ongezeko la thamani ya ardhi (increase of land value)
Matumizi ya ardhi kwa manufaa zaidi ya wakazi wa miji husika (Optimum utilization of land resources)
Kuwezesha utoaji huduma za kijamii na kimaendeleo kwa gharama nafuu zaidi za kiuendeshaji (economies of scales)


SHERIA, SERA NA KANUNI MUAFAKA HAPA NCHINI
Sheria ya Mipango miji na Vijiji ya mwaka 1956 (Cap 378) iliyokuwa ikitumika baada ya uhuru na kuendelea
Sheria ya Mipango miji Na. 8 ya mwaka 2007 kimsingi inayotumika sasa kwa kiwango kikubwa
Sera ya Mipango miji ya mwaka 2000
Sheria ya Serikali za Mitaa Na. 4 ya 1999
Sheria ya Mazingira Na. 191 ya mwaka 2004
Sheria na Sera za Sekta mbalimbali zinazohusiana na maendelezi ya miji
Kanuni zilizotungwa kusimamia na kufafanua sheria mbalimbali husika katika utekelezaji wake.


NGAZI ZA MIJI ZINAZO TAMBULIKA KISHERIA NCHINI
Ngazi za miji zinazotambulika kisheria nchini ni:
v Vitongoji/Vijiji (Minor Settlements)
v Miji midogo (Townships)
v Miji (Towns)
v Manispaa (Municipalities)
v Majiji (Cities)
v Mkusanyiko wa Majiji (Meg cities).

TARATIBU ZA KUZINGATIA WAKATI WA UPANUZI WA MIPAKA YA MIJI:
Sheria Mipangomiji Na. 8 ya mwaka 2007
Ø Katika kifungu Na. 7(1) hubainisha kuwa kila mamlaka husika ni mamlaka ya upangaji katika eneo lake la utawala
Ø Katika kifungu Na. 7(2) hutamuka waziwazi kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa ndie mwenye mamlaka ya kuamua kupanua mipaka ya miji hapa nchini Katika kifungu Na. 7(3) hubainisha kwamba endapo kuna vijiji vitamezwa na mipaka mipya ya mamlaka yeyote basi vijiji hivyo vitatakiwa kufutwa katika daftari ya usajili wa vijiji kwanza
Ø Aidha, katika kifungu Na. 7(4) inamtaja Waziri mwenye dhamana na masuala ya Mipangomiji kuweza kutangaza katika gazeti la umma ingawa baada ya kushauriana na Waziri wa Serikali za Mitaa, chombo chochote kuwa mamlaka ya upangaji au shirika na kinginecho
Ø Vifungu mbalimbali vya Sheria hiyo pia hubainisha majukumu mbalimbali Mamlaka ya Upangaji inatakiwa kuyafanya
Ø Katika kifungu Na. 8(1) kinamtaja Waziri mwenye dhamana na Mipangomiji kuwa na mamlaka ya kutangaza katika Gazeti la umma eneo lolote la ardhi kuwa eneo la kupangwa (declaration of planning areas)


HITIMISHO
Utaona kuwa miji kama walivyo wanadamu hupitia hatua mbalimbali za kukua na kwamba tupende tusipende itaendelea kukua ingawa kwa uwezo tofauti tofauti kulingana na lishe ipatikanayo.
Hivyo mamlaka husika zina wajibu wa kuelewa hatua hizo na kuzisimamia kikamilifu na kwa wakati

1 comment:

  1. Eva & Majura, shukrani kwa muhtasari huu. Kazi njema.
    Wananchi wanapaswa kuendelea kuelimishwa juu ya mambo mbalimbali yanayowahusu.

    ReplyDelete