Thursday, September 30, 2010

SIKU YA MAZIWA SHULENI DUNIANI,MARA.

Mkuu wa Mkoa wa Mara,Col.Mstaafu Enos Mfuru,akigawa maziwa kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Elizabeth James wakati wa sherehe hizo kitaifa zilizofanyika Mkoa wa Mara,juzi katika viwanja vya mukendo.
Wadau wa maziwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi kwa makini.

Mwisenge shule ya Msingi aliposoma Baba wa Taifa,Hayati Mwl.Julius Nyerere walipamba sherehe hizo,shule hiyo ni maalumu kwa watoto wasiiona,wenye ulemavu wa ngozi,na viziwi na wengine ambao hawana ulemavu wowote.


Maandamano ya sherehe hizo mbele ya mgeni rasmi.



Saturday, September 25, 2010

KAMBI YA WAVUVI BUSEKELA MAJITA


Moja ya kambi yua wavuvi inayotumika kwa wavuvvi makazi yao,katika kijiji cha Busekela,Kata ya Bukumi,Jimbo la Musoma Vijijini (MAJITA).ambapo kwa mara ya akwanza yangu nchi hii kupata uhuru hawjawahi kutembeleawa na Rais yoyote nchini.

RAIS WA KWANZA KUFIKA BUSEKELA BUKUMI MUSOMA VIJIJINI.

Baadhi ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kusikiliza sera za Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete katika uwanja wa Mukendo Mjini Musoma,Jimbo la Musoma Mjini.
Mgombea Ubunge pekee aliyepita bila kupingwa Nimrod Mkono, akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM,ana kuomba kura kwa chama cha CCM,nyuma yake ni Mlima Mtilo.


,Rais kikwete akitomba ridhaa kuwa Rais kwa mara nyingine tena,ni Rais wa kwanza kufika katika kijiji ch Busekela kata ya Bukumi Wilaya ya Musoma Vijijini.

Monday, September 13, 2010

Sunday, September 12, 2010

LELEMAMA NA SALMA KIKWETE

Kikundi cha lelemama kikitumbuiza mara baada aya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kuwasili Mjini Musoma.

UWT NA MAMA SALMA KIKWETE MUSOMA.



MAMA SALMA NDANI YA MJI WA MUSOMA

Akisalimiana na madiwani wateule wa Viti Maalum,Wilaya ya Musoma Mjini.
Akisalimia na viongozi wa Serikali.
Akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM,Wilya ya Musoma Mjini,Joseph Obetto.

Thursday, September 9, 2010

PICHA YA JK NA WAGOMBEA WAKE ZACHANWA MARA

Picha za wagombea wa Urais,Ubunge na Udiwani kata ya Mkendo ikiwa imebadikwa kwenye ukuta,kuashiria kuanza kwa kampeni Septemba 12 mwezi huu uwanja wa mkendo Mjini Musoma.
Kuchanwa huku kwa picha ni kuzipenda sana ama kutopenda wagombea waliokaa pamoja na mgombea Urais kwa tiketi ya CCM? TAFAKARI!!!

Wednesday, September 8, 2010

MABANGO YA JK NDANI YA MUSOMA.

Bango la CCM,likiwa kwenye viwanja vya Mkendo Mjini Musoma ambapo wiki hii kampeni rasmi mjini hapa zinaanza.JK akiwa na Mjane wa Baba wa Taifa.
Bango la CCM,likiwa katika barabara ya Nyerere,Mtaa wa Lucas Musiba,Nyasho,Mjini Musoma,Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete,akimjuli hali Mkuu wa Majeshi mstaafu,Jenerali Ernest kiaro,aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Rufani Bugando Jijini Mwanza.Juni 5,2010

MOSHI MWEUPE MUSOMA KUWAKA WIKI HII.

UZINDUZI wa Kampeni za CCM Mkoa wa Mara, unatarajiwa kufanyika Septemba 12 katika kiwanja cha Mkendo, Musoma Mjini huku mapambo mbalimbali ya kuwanadi viongozi yakisheheni shamra shamra hizo kwenye magari,mabango na nyumba.

Blog hii imeshuhudia mabango mbalimballi yakiwemo ya picha ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Mkuu wa Majeshi mstaafu,jenerali Ernest Kiaro,akiwa katika Hospitali ya Rufani ya Bugando Jijini Mwanza.

Bango jingine ni lile la Mjane wa Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Nyerere,Mama Maria Nyerere likiwa kati ya shule za Iringo na Mkendo(viwanja vya Mkendo) ambavyo ni maarufu kwa mikutano mbalimbali mjini Musoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya kitaifa,Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete atazindua rasmi Septemba 22,ambapo pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete atakuwa Mjini hapa Septemba 13 akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mara (UWT).

Chama cha Mapinduzi (CCM) kina sifa zinazostahili kuongoza nchi na kuwaletea watu maendeleo,huku ukimya ukitawala kwa vyama vingine vya siasa.