Wednesday, September 8, 2010

MOSHI MWEUPE MUSOMA KUWAKA WIKI HII.

UZINDUZI wa Kampeni za CCM Mkoa wa Mara, unatarajiwa kufanyika Septemba 12 katika kiwanja cha Mkendo, Musoma Mjini huku mapambo mbalimbali ya kuwanadi viongozi yakisheheni shamra shamra hizo kwenye magari,mabango na nyumba.

Blog hii imeshuhudia mabango mbalimballi yakiwemo ya picha ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Mkuu wa Majeshi mstaafu,jenerali Ernest Kiaro,akiwa katika Hospitali ya Rufani ya Bugando Jijini Mwanza.

Bango jingine ni lile la Mjane wa Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Nyerere,Mama Maria Nyerere likiwa kati ya shule za Iringo na Mkendo(viwanja vya Mkendo) ambavyo ni maarufu kwa mikutano mbalimbali mjini Musoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya kitaifa,Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Rais Jakaya Kikwete atazindua rasmi Septemba 22,ambapo pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete atakuwa Mjini hapa Septemba 13 akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mara (UWT).

Chama cha Mapinduzi (CCM) kina sifa zinazostahili kuongoza nchi na kuwaletea watu maendeleo,huku ukimya ukitawala kwa vyama vingine vya siasa.

No comments:

Post a Comment