MUSOMA.
JUMLA ya Wakufunzi wapatao 136 kutoka katika Wilaya za Mkoa wa Mara, wamepata mafunzo ya
Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2012
Akifungua mafunzo hayo ya siku 12, yaliyoanza Julai 16 katika Ukumbi wa
CCM Mkoa wa Mara, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa alisema zoezi la Sensa
halitakwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwani makarani wapo kwa ajili ya
kufanya kazi hiyo.
Alisisitiza kwa wananchi kwamba kuwa suala la Msingi ni
kwamba kila mtu atakayelala nchini Agosti 25 kuamkia Agosti 26 ni lazima
ahesabiwe mara moja tu.
“Ninawaomba wananchi wote mtoe ushirikiano wa kutosha kwa
makarani wa Sensa ili kupata taarifa muhimu na sahihi kwa ajili ya mipango
endelevu ya maendeleo ya nchi yetu”Alisema Tuppa.Na kuongeza “ kuweni marafiki
kwa makarani hapo ili wafurahie kazi yao na matokeo yake yawe mazuri.
Aidha amevitaka vyombo vya dola, kamati za ulinzi na usalama
za kila ngazi, Mgambo pamoja na vikundi vya ulinzi wa jadi chini ya dhana ya
ulinzi shirikishi vichukue nafasi zao ili kuhakikisha zoezi la sensa
linafanyika kwa usalama toka mwanzo hadi mwisho,sanjali na ulinzi wa vifaa vya sensa.
Aliwataka kufuatilia mafunzo hayo kwa makini na usikivu wa
hali ya juu ili hapo baadae wawe walimu wazuri watakaoendesha shughuli zote kwa
usahihi na kwamba yapo maboresho makubwa yaliyofanywa katika madodoso na mfumo
mzima wa utunzaji wa kumbukumbu kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia kwa
kutumia teknojia ya Scanning ijuliknayo kama Optical Mark Reader(OMR)ambayo
iliyotumika mwaka 2002.
Teknojia hiyo iliipa heshima kubwa nchi yetu katika Nyanja za
kimataifa na kupelekea baadhi ya nchi za kiafrika kujifunza na kuchaguliwa kuwa
mjumbe wa kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.
Alitoa pongezi kwa Wilaya ya Tarime ambayo ilitoa
ushirikiano wa kutosha katika jaribio la sense iliyofanyika katika kata za
Matongo, Nyangoto A na B mwaka 2011, viongozi wa madhehebu ya dini, Vyama vya
siasa, Mashirika yasiyo ya kiserikali, Taasisi mbalimbali za Umma na binafsi,
vyama vya walemavu,Wazee, vyombo vya habari,Wabunge, Madiwani.
Aliwashukuru pia Wazee wa mila na Koo, viongozi wa serikali
za Mitaa, viongozi n awatendaji ngazi ya Tarafa, Kata, vijiji hadi vitongoji na
mitaa katika kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi wa Mkoa wa Mara ili washiriki
katika zoezi la Sensa.
Awali akisoma hotuba yake Mratibu wa Sensa Mkoa wa Mara,
Ramadhan Mbega alisema kuwa mafunzo hayo yanashirikisha wakufunza wapatao 136
toka ngazi ya Mkoa na Halmashauri zote n akwamba uchaguzi wa wakufunzi hao
ulifanywa kwa umakini wa hali ya juu na hivyo wana imani nao na kwamba
wanatarajia kupata matokea chanya mwisho wa mafunzo hayo.
Alisema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwatayarisha
watendaji wote watakaohusika katika zoezi la kukusanya taarifa kwa kufuata
maelekezo kikamilifu kwa uelewa wa pamoja na kutoa ufahamu kwa wakufunzi jinsi
ya kufundisha, kutafsiri na kutumia melekezo kwa makrani na wasimamizi, pamoj
ana vifaa mbalimbali vya sensa.
Kufuatia sense zilizotangulia Mkoa wa Mara ulikuwa na watu
723,327 mwaka 1978,wanaume 118,476 wanawake 134,534 Mwaka 1988 wakikuwa watu
946,418 kati ya hao wanaume walikuwa 444,446 na wanawake 501,972, ambapo sensa
ya mwaka 2002 walikuwa watu 1,362,397 wanawake wakiwa 713,690 na wanaume
649,707
No comments:
Post a Comment