MUSOMA.
WATU wanne wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti
likiwemo la kujinyonga na ajali ya gari.
Akizungumza na blog hii, ofisini kwake Kamanda
wa Polisi,Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Absalom Mwakyoma alisema tukio
la ajali lilitokea majira ya saa 9:40
Alasiri ,Julai 14 ambapo watembea
kwa miguu watatu walifariki dunia katika barabara iendayo Saragana- Kusenyi
Suguti.
Alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Jpsum yenye namba za usajili T
752 BQR likiendeshwa na Antony Kusaga(45) mwenye mali hiyo ambaye aliwagonga
waenda kwa miguu, Asha Mwero(16) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza
katika Shule ya Sekondari ya Suguti Wilaya ya Musoma Vijijini ambaye alifariki
dunia siku hiyio hiyo akipata matibabu katika hospitali ya Mkoa Musoma.
Aliwataja wengine wawili waliofia hapo hapo kuwa ni Nyakwesi
Mwero ( 15) na Rebina Mwero (4) wote wakazi wa kijiji cha Suguti katika Wilaya
ya Musoma Vijijini.
Alikitaja chanzo cha ajali kuwa inasadikiwa kuwa ni mwendo
kasi aliokuwa nao dreva na kwamba dreva huyo alijisalimisha mwenyewe katika
kituo cha polisi na kwamba tayari amefikishwa mahakamani.
Katika tukio jingine lilitokea Julai 17,asubuhi katika
maeneo ya Mahakama kwenye nyumba ya Marehemu Dokta Emmanuel Magoti, mtu mmoja ambaye bado hajajulikana jina lake mwenye
jinsia ya kiume amekutwa akiwa amefariki baada ya kujinyonga ambapo mwili wake
umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospital ya Mkoa Musoma.
Amewataka wakazi wa Mji huo kwenda katika Chumba hicho
kutambua mwili wa marehemu ili mwili wake ukazikwe vinginevyo utazikwa na serikali
No comments:
Post a Comment