MUSOMA.
Na: Ghati Msamba.
MKUU wa Mkoa wa Mara,
John Tuppa amewataka viongozi n awadau mbalimbali kuhakikisha kunajengwa Mnara
wa kumbukumbu ya Mashujaa bila kupuuuza alama mbalimbali za mashujaa zilizopo
ikiwemo ya mnara mdogo uliopo sasa.
Aliyasema hayo katika
maaddimisho ya siku ya mashujaa iliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya kanisa
la Roman Cathoric (RC) Rwamlimi nje kidogo ya Manispaa ya Mji wa Musoma.
Alisema kuwa zoezi la ujenzi wa mnara mpya likisimamiwa na
kuratibiwa ipasavyo mwakani, maadhimisho hayo yanaweza kufanyika katika Mnara
mpya kuliko kwenda eneo jingine.
Aliongeza kuwa nia na madhumuni ya kuchagua Mnara mdogo kwa
kuwa ina kumbukumbu ya kuanguka kwa ndege tatu za kivita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
zilizoanguka mwaka 1979.
“Hapa pana nasaba
kubwa na maadhimisho hayo kuliko kufanyia kwenye viwanja vya wazi, na
kilichotoleta si dhehebu la dini bali ni alama ya Mnara yenye uhusiano na
maadhimisho haya”
“Hatuna malipo yanayolingana na ushujaa waliouonyesha
mashujaa wetu, hatuna.Tuendee kuwakumbuka na kuwaombea Amen”Alisema Tuppa.
Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mara kuendelea kufuata nyayo
za mashujaa wetu, kulinda hazina za ujasiri, uzalendo, umoja na amshikamano
walizotuachia na kutocheza amani iliyopo kwani haikujegwa siku moja na kwamba
endapo tutadhubutu kuiachia itaondoka mara moja lakini itagharimu muda
mwingi na jasho jingi kuirudisha.
Aidha maadhimisho hayo yanayanyika Julai 25, badala ya
Septemba 1, 1964 ya kila mwaka kwani julai
25,1979 ndiyo siku ambayo Taifa la Tanzania liliwapokea mashujaa rasmi
waliokuwa wanarudi nchini wakitokea Uganda baada ya kumaliza kazi kubwa ya
kishujaa ya kumng’oa nduli Idd Amin Dada, kwa mapokezi yaliyafanyika
Nyakanazi Mkoani Kagera na Septemba 1
ndiyo jeshi jipya la Wananchi wa Tanzania lilipoundwa baada ya jeshi la Zamani
lililoridhiwa kutoka kwa wakoloni lilipovujwa.
Mkuu wa Mkoa huyo ameipongeza Parokia ya Ramwilimi na Kanisa
Katoliki kwa kuutunza na kuulea Mnara huo na ushirikiano waliotoa kwa Serikali
kila ilipohitajika kufanya shughuli zake
katika eneo hilo snajala na madhehebu mengine yalishiriki katika maadhimisho
hayo bila kujali mahali maadhimisho hayo
yamefanyika.
Aidha ametaka wananchi kushiriki katika zoezi la sense ya
watu na makazi la litakalofanyika Agosti 26 2012 na kuhudhuria kwa wingi ili
kutoa maoni ya katiba Mpya pale itakapopita kupokea maoni juu ya katiba hiyo.
Kufanyika kwa Maadhimisho hayo kunatokana na agizo la Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, Dk. Jakaya Kikwete kutoa maelekezo siku hii isiadhimishwe Mkoa wa Dar
es Salaam pekee badala yake iadhimishwe kila Mkoa.
No comments:
Post a Comment