TARIME.
VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) Wilayani Tarime wameshindwa kuafikiana katika kikao cha kamati tendaji kilichofanyika juzi kupata mwafaka uliosababisha kufugwa kwa ofisi. Wanamtaka Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe kuwashuruhisha.
Mjumbe mmoja alisema kuwa kwa sasa kunampasuko mkubwa ndani ya chama
cha Chadema ambapo tayari kuna makundi mawili yanayodaiwa kuwa kundi moja ni la Mwenyekiti wa Vijana Taifa John Heche na kundi la George Waitara ambao wanadaiwa kuwa wapo mbioni na kwamba wanajipanga kugombea 2015
Katibu Mwenezi wa Chama cha Chadema Wilaya Marwa Maruri alikiri kwa
baadhi ya viongozi kuondoka wakati kikao kinaendelea. Baadhi ya wanachama Mjini Tarime walisema kuwa sababu ya kufungwa kwa ofisi kwa muda wa siku 3 imekuja baada ya Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Lucas Ngoto kusimamishwa uongozi na kamati Tendaji jambo ambalo alikuafikiwa na baadhi ya wananchama na kuibua mgogoro mkubwa ambao umewafanya baadhi yao kugawanyika makundi. |
Saturday, February 23, 2013
MPASUKO CHADEMA TARIME.
Wednesday, February 13, 2013
MBWAMWITU HAWATATOWEKA TENA-SERENGETI
SERENGETI
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI)
Dk.Simon Mduma amesema kuwa tishio la kutoweka Mbwa Mwitu katika hifadhi ya Serengeti
kutokana na magonjwa mbalimbali ya mbwa litatoweka kwani tayari wamepata chanjo
ili kuweza kumaliza magonjwa yanayosababisha kutoweka kwa Mbwa Mwitu.
Mbwa hao
waliochukuliwa eneo la Loliondo wamefugwa katika Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa
miezi mitatu hili likiwa ni kundi la pili lenye mbwamwitu 15 ambapo kundi la
kwanza lilitolewa Agosti 30 mwaka huu likiwa na mbwamwitu 11 waliachiwa ndani
ya hifadhi hiyo mwaka 1980 na kulikuwepo Mbwa
Mwitu wapatao 500.
Aidha Mbwamwitu
wapatao 15 ambao walikuwa wamefugwa katika eneo la Nyamuma ndani ya hifadhi
hiyo kwa ajili ya juhudi za kuwarudisha wanyama hao ambao walitopotea miaka ya
1990 wanaendelea vizuri.
Kukosekana
kwa wanyama hao ndani ya hifadhi hiyo kumesababisha kukosekana kwa kivutio
kingine muhimu ambapo watalii wanahitaji kuwaona.
Alitoa pongezi
kwa mashirika mbalimbal ikiwemo ofisi ya
Rais,ambayo ilichangia Sh. M.30 kwa ajili ya mradi wa mbwa mwitu kwani imesaidia kuongeza kivutio muhimu.
Alisema kuwa
kuna changamoto ambazo wanakabiliana nazo ikiwa ni pamoja mashirika mengi
kutofadhili mradi huo ambapo kwa sasa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom
ndio pekee iliyotoa ufadhili wa zaidi ya milioni 450.
Kutokana na
kuruhusiwa kwa mbwamwitu hao sasa imeongezeka na kufanya idadi ya wanyama hao
kufikia 26 ndani ya TANAPA ambapo Agosti 30 mwaka huu waliachiwa 11.
Hivi karibuni
Rais Jakaya Kikwete aliagiza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
kuhakikisha Mbwamwitu waliofunguliwa katika mbuga ya Serengeti wanakuwa salama muda
wote ili wasitoweke tena.
Sunday, February 3, 2013
CCM MWANZA WAHADHIMISHA KWA MICHEZO
MWANZA
CHAMA
cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza kimefanya maadhimisho ya
kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya michezo mbalimbali ikiwemo
ya mbio za baiskeli yaliyosisimua wakazi
wa Jiji la Mwanza.
Mbio
hizo zilizoanzia katika ofisi za CCM Makao Makuu kuelekea Barabara ya
kenyata-Usagara zilianza majira ya mbili asuhuhi na kuleta hamasha kubwa kwa
wakazi wa Wilaya ya Nyamagana ambao kwa pamoja walikuwa wakiwashingilia huku
wakisidikizwa na gari la Katibu wa CCM Wilaya hiyo likiwa na bendera kubwa ya
Chama.
Mshindi
wa kwanza katika mbio hizo alikuwa Gegedi Maduhu (25) mwenye namba 850, Mfanyabiashara ya
bodaboda ya baiskeli na Mzaliwa wa kijiji cha Mwamoto-Ngokolo Mkoa wa Shinyanga
aliyemaliza mbio hiyo na kuwaacha wenzake kwa takribani dakika 10 na kumaliza
mbio hiyo 10:40 katika Uwanja wa Kumbukumbu wa
Nyamagana.
Mshindi
wa Pili alikuwa Paulo Mathias ( 19)
mwenye namba 831 Mkazi wa
Shamaliwa kata ya Igoma Mwanza ambaye ni Mkulima wa mpunga aliyemaliza mbio
hiyo 10:44 na Mshindi wa tatu alikuwa Kulwa Kalamo (20) mwenye namba 834
aliyemaliza kwa muda wa 10:46 na alipewa kombe na fedha taslimu Sh.300,000.
Aidha
akizungumza na Uhuru, mara baada ya
kukamilika kwa mbio hizo, Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Nyamagana,Raphael
Shillatu alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kuhamasisha wananchi.
“Mchezo
huu ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia michezo
ili kuleta hamasha kwa vijana kwani
michezo ni ajira, pia huleta Mshikamano, Umoja, Upendo, Utulivu na Amani
na kukiwezesha chama kuwa na timu itakayofanya kazi pamoja na kuhakikisha
ushindi kuanzia chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2015”Alisema
Shillatu.
Aliongeza
kuwa mkakati huo ni ahadi yake wakati akiwa
anagombea Kiti hicho kuwa atahakikisha anaimarisha michezo yote ifikapo
maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama ikiwa ni pamoja na riadha ya Baiskeli, mpura
wa Miguu kwa wanaume ,bao,na baadae kuanzisha michezo mbalimbali kwa wanawake
ambao nduyo wenye hamasha kubwa hadi
ukomo wa Uongozi wake ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani kwa vitendo.
Aidha
washindi hao walipewa vitita vya fedha zilizokuwa zimefugwa kwenye bahasha
ambapo hata hivyo hazikutangazwa kwa
ajili ya usalama wao na kupewa bendera za CCM na mlingoti wake kupeperusha
bendera hizo maeneo ya makazi yao.
BODI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MUSOMA
BODI ya Hospital ya Rufaa ya Musoma ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uteuzi, wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara,John Tuppa,kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Baba Askofu Amos Muhagachi ambaye baada ya kuteuliwa alimtoa Katibu wa Hospital,Faustin Bigambo kwa utendaji mbovu katika Hospitali hiyo ili apangiwe kazi nyingine.
Saturday, February 2, 2013
UWT MUSOMA MJINI WAADHIMISHA KUZALIWA CCM
Wilaya ya Musoma Mjini imefanya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutembelea wagonjwa katika wodi mbalimbali katika Hospital ya Rufaa ya Musoma sanjari na kufanya usafi wa Mazingira,kutoa sabuni pamoja na Juice kwa watoto wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Musoma Mjini ,Amina Masisa,amesema kuwa katika kuadhimisha kuzaliwa kwa CCM,shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira
kata za Kamunyonge,Kitaji, Iringo,Nyasho,Mwisenge,Bweri,Makoko,Kigera, Mwisenge zimeungana na wajumbe kufanya usafi katika kata hizo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Stend Kuu ya mabasi(Bweri),Soko kuu Mjini,mwalo wa Mwigobero na kwenye Zahanati.
Amesema,Chama cha Mapinduzi kina mvuto wa peke yake na kwamba wamekuwa wakipokea wanachama wapya hasa kwa jumuiya hiyo na kwamba wamejizatiti kikamilifu katika kuhakikisha Chama kinaendelea kushika dola kuanzia mwakani kwa upande wa chaguzi za Serikali za Mitaa na 2015.
Uchaguzi Mkuu.
Kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi kitaifa kitafanyika katika Mkoa wa Kigoma ambapo,Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi.
Subscribe to:
Posts (Atom)