Saturday, February 2, 2013

UWT MUSOMA MJINI WAADHIMISHA KUZALIWA CCM



Wilaya ya Musoma Mjini imefanya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutembelea wagonjwa katika wodi mbalimbali katika Hospital ya Rufaa ya Musoma sanjari na kufanya usafi wa Mazingira,kutoa sabuni pamoja na Juice kwa watoto wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Musoma Mjini ,Amina Masisa,amesema kuwa katika kuadhimisha kuzaliwa kwa CCM,shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira
kata za Kamunyonge,Kitaji, Iringo,Nyasho,Mwisenge,Bweri,Makoko,Kigera, Mwisenge zimeungana na wajumbe kufanya usafi katika kata hizo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Stend Kuu ya mabasi(Bweri),Soko kuu Mjini,mwalo wa Mwigobero na kwenye Zahanati.

Amesema,Chama cha Mapinduzi kina mvuto wa peke yake na  kwamba wamekuwa wakipokea wanachama wapya hasa kwa jumuiya hiyo na kwamba wamejizatiti kikamilifu katika kuhakikisha Chama kinaendelea kushika dola kuanzia mwakani kwa upande wa chaguzi za Serikali za Mitaa na 2015.
Uchaguzi Mkuu.

Kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi kitaifa kitafanyika katika Mkoa wa Kigoma ambapo,Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment