Tuesday, January 29, 2013

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NA OPERESHEN


MUSOMA

JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara limefanikiwa kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga ya moto  katika Manispaa ya Musoma licha za zoezi hilo kuingiwa na dosari kwa baadhi ya wamiiliki wa maduka kukataa kukaguliwa na kulipia ada ya Ukaguzi.

 Akizungumza na Uhuru  ofisini kwake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara Don Mhally  alisema kuwa kwa upande wa Wilaya zingine zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini kwa Manispaa ya Musoma baadhi ya wamiliki walikataa kwa kile kinachodaiwa kuwa  utoaji wa fedha bila kupatiwa kifaa cha kuzimia moto.

Alisema kuwa  baadhi ya wamiliki wa maduka waliokaa kukaguliwa wameachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na kufikisha Mahakamani kwa kosa la kukiuka Sheria ya ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Na.14 ya mwaka 2007 pamoja na kanuni zake za mwaka 2008(Fire Safety Inspection and Certificate) na marekebisho yake ya mwaka 2012.


Jumla ya maduka ya kawaida zaidi ya 74 yamekaguliwa na kulipia gharama ya ukaguzi na cheti na makusanyo ilikuwa ni sh. 54,590,000,ambapo kutoka Julai-Novemba 2012 jumla ya maeneo 431 yamekaguliwa na zoezi hili ni la mwaka mzima wa fedha hadi Juni 30.

Aidha wametakiwa kuwa na kifaa cha kuzimia moto ambavyo vinapatikana kwa mawakala walioteuliwa, aliwataja kuwa ni Sodobhi Investment,Dawill Trading Agency(ZK) na Musoma Equipment Agency za Mjini hapa.
 

No comments:

Post a Comment