Thursday, January 10, 2013
DIWANI CCM AHUSISHWA NA MAUAJI YA KUKATWA VICHWA
BUTIAMA
Diwani wa CCM,kata ya Mugango,Wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara,Wandwi Maguru (34), amekamatwa na anahojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya kutisha ya kukata shingo la Tabu Makanya (68) katika tukio lilitokea Desemba 21 mwaka jana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwaykoma amethibitisha kukamatwa kwa diwani huo jana na kwamba mauji hayao ni ya imani za kishirikina ambayo pia yalihusu tukio la kwanza la Desemba 2 ambapo Blandina Peru(28) Mkazi wa Mahare alichinjwa na kukingwa damu ambvapo Desemba 3 majira ya saa tano asubuhi Sabina Maki (46) na kutoweka na kichwa chake.
Desemba 21,katika kijiji cha Kwikuba,kata ya Mugango, Wilaya Butiama,
Tabu Makanya(68), aliuawa na watu wanne wanaojulikana wakiwa nyumbani
kwake walimshambulia kwa fimbo na bapa za panga sehemu mbalimbali ili
kumlegeza mwili wake na baadaye kumchinja na kuchuka kichwa chake
ambacho walikiweka kwenye mfuko wa salphet na kutoweka nacho.
Mara baada ya kuondoka wauaji hao nyumbani kwa marehemu,ndipo yowe
ilipigwa na vijana waliokuwa kwenye nyumba hiyo ya uwani na majirani
walianza kuwafukuza wauaji hao ambao baada ya kuzidiwa walikitupa
kichwa hicho na kutoweka gizani kwenye kichaka.
Kuhusu tuko la mauaji ya Blandina Peru(28) ambaye alichinjwa na
kuchukuliwa damu lilitokea katika kijiji cha Mahare,Kata ya Etaro
Desemba 2 watu watatu walikamatwa na kufikishwa mahakamani Desemba 21.
Waliokamatwa ni Sura Siriro,Jani Magesa Shusha na Mgasa Nyarukama
Maumau na kuhusu tukio la mauaji ya Sabina Mkireri ambaye pia
alichinjwa na kuchukuliwa kichwa lililotokea Desemba 3 katika kijiji
cha Kabegi Kata ya Nyatende, Wilaya ya Butiama, watu sita wamekamatwa
na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Aidha Mwalimu Christina Manoni aliyepotea na baadae mwili wake kuonekana Desemba 4ukiwa unabishaniwa huku wengine wakidai ndiye wengine siye DNA itatatua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment