Thursday, January 3, 2013

MAUAJI YA KUKATWA VICHWA 6 WAHOJIWA 3 MAHAKAMANI.

MUSOMA,MARA. WAKAZI wa Mkoa wa Mara waomba iundwe tume kuchunguza mauaji yaliyojitokeza mwaka jana na ambayo anaendelea katika Mkoa huu, huku wakiomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema kufanya hivyo haraka kama alivyofanya kwa mmoja wa kiongozi wa juu ambaye aliuawa Mkoani Mwanza na wauaji kukamatwa haraka. Wakizungumza kwa nyakati tofauti , baadhi ya wakazi wa Mji huu, ambao hawakutaka kutaja majina yao kwa kuhofia usalama wao walisema kuwa wanamwomba,Mkuu wa Jeshi la Polisi,Said Mwema kutuma kikosi cha upepelezi kutoka makao Makuu kuchunguza tukio hili hatarishi kwa Mkoa huu. “Naona Kamanda huyu mpya kaanza vibaya, na kama ameshindwa bora ateuliwe mwingine,pia tunamwomba Mkuu wa jeshi la polisi atume vikosi vyake kufanya uchunguzi,kama alivyofanya kwa kiongozi mmoja aliyeuwa huko Mwanza na watu kupatikana”kilisema chanzo hicho cha habari. Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi,katika kijiji cha Kwikerege kata ya Etaro Wilaya ya Butiama,Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Etaro na Mkazi wa Kwikerege Wilaya ya Butiama,Kiba Hamisi (20) aliuawa kwa kushambuliwa na fimbo,mawe na kukatwakatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma kuwa anajihusisha na vitendo vya mauaji yaliyotokea maeneo ya jirani. Inadaiwa kuwa Marehemu alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti Nyakongo Nyangata(13) Mwanafunziwa Shule ya Msingi Etaro ambapo marehemu alikutwa chini ya uvungu wa kitanda katika chumba cha binti huyo na babu wa binti huyo,Butiti Makuna(84) mkazi wa Kukona Etaro, baada ya kumwona alipiga yowe, marehemu alitoka ndani ya nyumba huku akikimbia na wanachi waliokuwa wanatoka katika mkutano wa kutoa maoni ya katiba walijichukulia sheria mkononi bila kuuliza nini chanzo chake,wakati huo binti alikuwa anaoga,tukio hilo lilitokea Disemba 5 2012. Desemba 12 mwaka jana eneo la alikamatwa James phinias (21) Mkazi wa Kamunyonge, Manispaa ya Musoma alikamatwa akiwa na noti bandia tisa za sh.5,000 zenye namba zinazofanana alipokuwa ananunua bidhaa kwa mfanyabiashara Mwikwabe Ginga. Aidha katika tukio jingine mwendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda ,Thomas Majengo(20) Mkazi wa Kigera Kyara mjini hapa,alikutwa akiwa ameuawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwa kukatwa panga/sime sehemu za shingoni upande wa nyuyma chini ya kisogo na jeraha kwenye mguu wa kulia. Katika eneo la Nyakato Mshikamano kwa saanane,Desemba 22,mtu aliyejulikana kwa jina moja la gogogo mwenye umri kati ya miaka 40-45 mwenyeji wa Wilaya ya Bunda ambaye alikuwa amepanga huko aliuawa na wananchi ambao walikuwa wakimtuhumu kuvunja nyumba na kuiba pamoja na kukata watu mapanga kabla ya hajauawa aliwarushia wananchi mishale ili kukwepa asikamatwe. Marehemu kabla ya kupatwa na mauti alikuwa na pikipiki aina ya Toyo yenye Namba za Usajiri T.528 BYF ambayo watu hao waliondoka nayo na mmiliki wa pikipiki hiyo hajafahamika na tukio hilo lilitokea Desemba 20. Desemba 21,katika kijiji cha Kwikuba,kata ya Mugango, Wilaya Butiama, Tabu Makanya(68), aliuawa na watu wanne wanaojulikana wakiwa nyumbani kwake walimshambulia kwa fimbo na bapa za panga sehemu mbalimbali ili kumlegeza mwili wake na baadaye kumchinja na kuchuka kichwa chake ambacho walikiweka kwenye mfuko wa salphet na kutoweka nacho. Mara baada ya kuondoka wauaji hao nyumbani kwa marehemu,ndipo yowe ilipigwa na vijana waliokuwa kwenye nyumba hiyo ya uwani na majirani walianza kuwafukuza wauaji hao ambao baada ya kuzidiwa walikitupa kichwa hicho na kutoweka gizani kwenye kichaka. Kuhusu tuko la mauaji ya Blandina Peru ambaye aklichinjwa na kuchukiliwa damu lilitokea katika kijiji cha Mhare,Kata ya Etaro Desemba 2 watu watatu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani Desemba 21. Waliokamatwa ni Sura Siriro,Jani Magesa Shusha na Mgasa Nyarukama Maumau na kuhusu tukio la mauaji ya Sabina Mkireri ambaye pia alichinjwa na kuchukuliwa kichwa lililotokea Desemba 3 katika kijiji cha Kabegi Kata ya Nyatende, Wilaya ya Butiama watu sita wamekamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo. Aidha katika eneo la Nyasho Mjini hapa, Desemba 23 Veronika Yohana(7) aliuawa na baba yake mzazi Yohana Msafiri(38) kwa kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili kosa la ugomvi wa kifamilia. Katika tukio jingine kwa kushirikina na wananchi wa kijiji cha Balili Bunda, Kitongoji cha Rubana, zilipatikana bunduki mbili aina ya Shortgun Greener yenye namba 71154 na gobore moja na risasi 22 za Shortgun,zikiwa zimekatwa vitako na kuchimbiwa ardhini. Silaha hizo zilitumika katika tukio la Desemba 1na kuuawa mfanyakazi wa kampuni ya kutengeneza barabara ya Jijini Mwanza Nyanza Road Works,Silaha nyingine ilipatikana katika Kijiji cha Bunchugu,kata ya Sedeco,Tarafa ya Rogoro Wilaya ya Serengeti aina ya gobore iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na risasi moja. Katika Kijiji cha Kyankoma, Kitongoji cha Mamititu, Kata ya Nyamimange, Wilaya ya Butiama watu wawili waliuawa kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na wanachi waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma ya wizi wa Ng’ombe,Waliouwa ni Waitara Wambura(36), Mkazi wa kijiji cha Kyankoma na Masoya Wambura (32),Mkulima na mkazi wa kijiji cha Kitaramanka. Kuhusu taarifa ya jeshi la polisi kituo kidogo cha polisi cha Tegeruka,kufyatua risasi katika Kijiji cha Wanyere kwa ajili ya kuwanusuru watu wawili ambao walitaka kuuawa na wanachi kwa tuhuma kuwa ndio wanaosadikiwa kuwa wanakata watu vichwa,wakiwa na bunduki walifyatua risasi zipatazo 19 hewani kwa lengo la kuwatawanya. Waliokuwa wanataka kuuawa ni Nyamimori Manumbu (21) Mkulima na MKazi wa Nyamatoke Wilaya ay Bunda na Felix Mafuru (45),Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Wanyere,mtu mmoja aitwaye Simon Chiganga Dotto (37) Mkazi wa wanyere ambaywe alikuwa mstari wa mbele kwa kuwashambulia kwa mawe askari hao,alicharazwa na risasi kwenye shingo upande wa kushoto. Katika tukio hilo wanachi hao walimjeruhi Afisa Mtendaji wa Kijiji,Charles Ndagire (50) Mkazi wa Wanyere kwa kmakta panga kisogoni kwa madai kuwa yeyey ndiye aliyewaita polisi ambao waliwazuia wasiwauwe wahalifu hao,pia wananchi hao waliharibu pikipiki aina ya Toyo yenye namba za Uasjili T.309 BNE mali ya askari waliokwenda kuwachukuwa watuhumiwa waliokamtwa na wananchi hao ambayo ilikuwa imehifadhiwa katika ofisi ya Kijiji. Jeshi la Polisi Mkoani hapa,limetoa wito kwa wananchi kutojichulia sheria mkononi kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria,pia inapoteza ushahidi na kutojua mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment