Thursday, January 10, 2013
MWANZA COACH YAUA MCHUNGA N'GOMBE NA N'GOMBE
MUSOMA.
Basi la Kampuni ya Mwanza Coach limepata ajali leo asubuhi majira ya Saa 1 na kuuawa mchungaji wa Ngo’mbe na Ng’ombe wanne eneo la Lamadi Mkoa wa Simiu.
Basi hilo lenye namba za usajili T5500 ASA lililokuwa likiendeshwa na Dereva aliyejulikana kwa jina la Hashimu J na anashiliwa na Jeshi la polisi katika kituo kidogo cha Polisi Lamadi pamoja na Basi hilo,ambapo abiria wapatao 30 walihamishiwa katika basi jingine la Kampuni hiyo hiyo.
Pia Kampuni la Bunda Bus linalofanya safari zake kutoka Bunda kuelekea Dodoma,pia lilipata ajali ambapo lilipinduka na kuuawa watu wawili.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imezuia mifugo kutochungiwa barabarani kwani inahatarisha usalama wa wanyama, mchungaji pia uharibifu wa barabara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment