Monday, January 21, 2013

TRA MUSOMA WAKOSA MAPATO-BUSEKELA


MUSOMA VIJIJINI


Mamlaka ya Mapato( TRA) Mkoa wa Mara hukosa mapato kutokana na makusanyo ya samaki aina zote ambapo samaki ya aina dagaa wanasafirishwa kwenda nchi  jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa kongo,kenya, Uganda,Zaire,Msumbiji na uarabuni.  



Zaidi ya tani 10,000 za samaki aina ya dagaa usafirishwa kila siku wakati wa msimu wa dagaa ukifika,kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya uarabuni ambapo amekuwa akiwatumia wakazi wa hapo kuwasafisha na kutumia chanja maalumu ya kuanika na kupakia samaki hao kwenye malori tayari kwa kusafirishwa.
 
Diwani wa kata ya Bukumi,Chomya Ndege pamoja na wananchi wa kijiji cha Busekela walishindwa kusema juu ya tatizo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa alipofanya ziara yake ya kikazi na kufanya Mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Msingi Busekela huku Diwani huyo akilalamikia mambo mengine yakiwemo ya ukahaba uliopo katika kisiwa hicho,ujambazi na uvuvi haramu.

No comments:

Post a Comment