Thursday, January 10, 2013

ASKARI POLISI WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO.


ASKARI Polisi toka Mkoa wa Kagera E.9172 D/CPL David wa kituo cha polisi Mkoa wa Kagera na F. 5553 Detective Constable Gerald wa upelelezi Wilaya ya Bukoba wamekamatwa na meno ya Tembo wapatao watatu walioangamizwa.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,Absalom Mwakyoma alisema kuwa Jan.6 katika kijiji cha Rwamchanga, Tarafa ya Rogoro, Wilaya ya Serengeti maafisa wa polisi na Tanapa, wakiwa katika mwendelezo wa misako mbalimbali wanayoendelea nayo walimkamata Boniface Kurwa (31) mkazi wa Geita akiwa na pikipiki T.784 CCC akiwa na mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Nyarata Mkazi wa Mugumu akiwa anaendesha pikipiki T.884 BPH ambaye alikimbia na kuacha pikipiki, zilikamatwa zikiwa zimepakia mifuko yenye meno ya Tembo.



Alisema kuwa meno hayo yalikuwa vipande 17,vikiunganishwa jumla ni meno sita makubwa sawa na Tembo watatu walioangamizwa ambapo katika kumhoji akatoa ushirikaino wa kuelekeza kwamba walikuwa wameletwa na watu wawili ambao wamefikia Hotel ya Galaxy ambapo aliwaongoza hadi hapo na kubini kuwa maaskari hao ndio wahusika.



Aidha Maaskari hao pia walidai kuwa wamefika kwa maelekezo ya Bonniface Emmanuel (mnyarwanda),ambapo askari hao walifika na gari Namba T.403 BPK Carina-Metalic Silver inayodaiwa kuwa ni mali ya Koplo David.



No comments:

Post a Comment