ZIARA
ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mara,Askofu wa Kanisa la
Menonite kanda ya kati Amos Muhagachi imeibua mambo mengi yakiwemo wizi wa
kupindukia wa fedha za kuchangia huduma ya afya, fedha za manunuzi ya
vifaa vya hospitali upande wa Ugavi (Procurement).
Mara baada ya kuteuliwa, Mwenyekiti huyo akiwa na wajumbe walipata fursa ya kutembelea wodi na sehemu ya kuhifadhia miili ya Marehemu (Mochwari) na maabara na kubaini kasoro nyingi zikiwemo pia za uchakavu wa mabomba ya kupitisha maji taka ambayo yamezagaa ovyo na kuhatarisha maisha ya wagonjwa katika wodi namba 7.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wodi mbalimbali walilalamika uongozi uliopo kwa kutokuwa makini na kuzingatia usafi,ambapo katika wodi namba tatu na saba wagonjwa hujisaidia haja kubwa kwenye ndoo zao na kumwaga nje asububi hali ambayo imekuwa ikiibua milipuko ya wagonjwa mengine.
Aidha watumishi wa hospitali hiyo pia walipata fursa ya kutoa dukuduku zao ambapo wameiomba bodi hiyo kumfukuza Katibu wa Hospital hiyo,Faustin Bigambo,Mhasibu na Afisa Ugavi kwa kuwa wazembe na kuvuja fedha za Serikali huku wakiwa hawawajali wauguzi.
Akilalamikia fedha za kipindupindu ambazo zililetwa na Wizara ya Afya na kuliwa,Afisa Muuguzi,Musa Jackson alisema kuwa Jumla ya Sh. Milioni 78 hazijulikani zilipo tangu mwaka 2008 kwa ajili ya watumishi kuhudumia wagonjwa wa kipindupindu na kwamba mpaka sasa hawajalipwa fedha hizo.
Aidha Wizara ya Afya utoa kila mwezi jumla ya Sh. Milioni 26 kwa ajili ya uendeshaji(0c).

Naye Muuguzi Hawa Albert alitoa ombi kwa Mwenyekiti huyo kuwanusuru wafanyakazi hao kwa kuwa wamechoka kulalamika na kwani kuna malimbikizo mengi ya fedha zao zikwemo posho za wenye zamu za usiku,motisha na mashono ya nguo za wafanyakazi na makato kutoka PSPF.
Bodi hiyo ni jumla ya wajumbe 15 ambao waneteuliwa kutoka sekta mbalimbali zikiwemo,viongozi wa madhehebu ya dini,(Maaskofu na Mashehe), madaktari, wanasheria, wafanyabiashara, wanasiasa na wenye taaluma ya afya,elimu na Madaktari kati ya hao wanawake ni watatu.
No comments:
Post a Comment