Tuesday, January 29, 2013

AMBULANCE ZA PIKIPIKI ZAOTA BUIBUI





BUTIAMA.

 WAKATI Serikali inajitahidi kutoa huduma ya afya ya Mama Mjamzito na Mtoto kutotembea mwendo mrefu kutafuta huduma ya afya,pikipiki za kusaidia huduma hiyo(Ambulance)  zilizoletwa katika Wilaya ya Butiama kuhudumia wananchi zimeshindwa kusambazwa.


Pikipiki hizo mpya zipatazo nne zimehifadhiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma,na zimeota Buibui na uwezi kuzitambua kuwa ni pikipiki zilizoletwa kwa ajili ya kusaidia huduma ya haraka kwa wagonjwa wenye hali mbaya kutoka kijiji fulani kwenda sehemu huska ambapo kikao cha  Bodi ya hospitali tayari kilishapitisha pikipiki hizo zinatakiwa kufanya huduma katika vjiji vya Balaga, Nyegina na Masinono.


Mganga Mkuu wa Musoma,Dk.Genchwele Makenge amesema kuwa Pikipiki hizo zimeshindwa kufanya kazi kutokana na kutosajiliwa kazi ambayo ni ya Wizara ya Ujenzi pia ukaguzi kutoka kwa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoani hapa.



Aidha kwa sasa gari la wagonjwa katika kituo cha afya cha Murangi limeharibika ambapo kwa sasa Wilaya ina Magari mawili ambayo hayatoshelezi kufanya huduma ya haraka kwa wagonjwa ambao hali zao zinakuwa mbaya.Wilaya ya Butiama ina vijiji 120,kata 34,Tarafa 3 na  Zahanati 59,ambapo pia alitoa wito kwa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ambapo watalipa Sh.10,000 kwa mwaka itakayowawezesha kutoa huduma bora ambayo itasaidia kupunguza gharama kwa mgonjwa.

Akizungumzia juu ya ukaguzi wa pikipiki za wagonjwa(Ambulance) kutokaguliwa na kusababisha wagonjwa kukosa huduma hiyo,Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Reuben Mataso alisema kuwa ameshindwa kufanya hivyo kutokana na pikipiki hizo kutokuwa na usajili.


No comments:

Post a Comment