Friday, January 4, 2013

MAITI YAOKOTWA IKIWA HAINA BAADHI YA VIUNGO


MUSOMA.



MAITI ya mwanamke asiyejulikana imeokotwa katika kitongoji cha Nyamiongo,Mtaa wa Nyarigamba ukiwa hauna baadhi ya viungo vya mwili.



Diwani wa Kata ya Makoko,Aloyce Lenatus, ambaye aliambatana na jeshi la polisi katika eneo la tukio alisema kuwa mwili huo ulikuwa wa mwanamke na ulikuwa umekatwa matiti,miguu na masikio.


Alisema kuwa kulikuwa na taarifa ya kupotea kwa mwanamke Disemba 18 mwaka jana,ambaye alimtaja kwa jina la Christina Manono ambaye alikuwa mwalimu mstaafu,akifundisha shule John Bosco iliyoko Mtaa wa Mukendo.


Aliongeza kuwa jeshi la polisi Mkoani hapa lina changamoto kubwa na linapaswa kuwa makini katika matukio hayo ili Wilaya na Mkoa kwa ujumla iendelee kuwa na utulivu na wananchi wakae kwa amani bila hofu yoyote.



“Tumezungumza na Mganga kuwa maiti huyo afanyiwe uchunguzi kabla ya kuzikwa mwili huo,na baadhi ya ndugu zake wametambua nguo za marehemu kuwa ambazo aliondoka akiwa amevaa kikiwa ni kikoi na sketi,lakini baada ya kuona maiti hiyo aliikataa kuwa si ndugu yao.




Alidai kuwa inawezekana wauaji hao wako na Mwalimu ambaye yawezekana wamechukua nguo zake na kwenda kutupa kwa maiti iliyookotwa ili kupoteza lengo kwani maiti huyo alikuwa ameharibika sana kiasi kwamba nywele ziko kisogoni tu na kichwa kimekuwa fuvu,hivyo inaonekana maiti hiyo ni ya muda mrefu kama miezi miwili ama mitatu kulingana na muda uliptolewa taarifa ya kupotea kwa Mwalimu huyo.


Taarifa kutoka jeshi la Polisi inasema kuwa Januari 3 majira ya 10:30 za jioni, Mtaa wa Nyarigamba, Kata ya Makoko Manispaa ya Musoma,Maiti ya mtu mmoja ambaye hajatambuliwa kw ajina iligundulika ikiwa imefukiwa pembeni ya mwamba kwa kutumia mawe na udongo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara,Absalom Mwakyoma katika taaarifa yake kwa waandishi wa habari alisema kuwa kulitokea uvumi uliohusisha mwili wa marehemu na mwanamke mmoja ambaye amepotea na haujulikani alipo tangu Desemba 14 anayaeishi mtaa wa Makoko Ziwani


Mganga wa zamu,Joseph Nyamagwira alipopigiwa simu alisema kuwa hawawezi kufanya uchunguzi bila ya kupewa taarifa na jeshi la polisi, huku jeshi hilo likidai kuwa mwili wa marehemu tayari umefanya uchunguzi katika hospital ya Mkoa na imebaini kuwa mwili huo umefukiwa haujulikani ni wa nani.



Akizungumzia unyanyasaji wa akina mama,Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere,Kata ya Mukendo, Debora Sadhu ametoa wito kwa mashirika ya kutetea haki za akina mama, na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kufanya ziara ya kuelimisha umma na kupinga kwa nguvu unyanyasaji huu, ambao umekithiri hasa kwa akina mama pekee.







No comments:

Post a Comment