Sunday, February 3, 2013

CCM MWANZA WAHADHIMISHA KWA MICHEZO



MWANZA

CHAMA cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza kimefanya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya michezo mbalimbali ikiwemo ya mbio  za baiskeli yaliyosisimua wakazi wa Jiji la Mwanza.

Mbio hizo zilizoanzia katika ofisi za CCM Makao Makuu kuelekea Barabara ya kenyata-Usagara zilianza majira ya mbili asuhuhi na kuleta hamasha kubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Nyamagana ambao kwa pamoja walikuwa wakiwashingilia huku wakisidikizwa na gari la Katibu wa CCM Wilaya hiyo likiwa na bendera kubwa ya Chama.

Mshindi wa kwanza katika mbio hizo alikuwa Gegedi Maduhu  (25) mwenye namba 850, Mfanyabiashara ya bodaboda ya baiskeli na Mzaliwa wa kijiji cha Mwamoto-Ngokolo Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza mbio hiyo na kuwaacha wenzake kwa takribani dakika 10 na kumaliza mbio hiyo 10:40 katika Uwanja wa Kumbukumbu wa  Nyamagana.

Mshindi wa Pili alikuwa Paulo Mathias ( 19)  mwenye namba  831 Mkazi wa Shamaliwa kata ya Igoma Mwanza ambaye ni Mkulima wa mpunga aliyemaliza mbio hiyo 10:44 na Mshindi wa tatu alikuwa Kulwa Kalamo (20) mwenye namba 834 aliyemaliza kwa muda wa 10:46 na alipewa kombe na fedha taslimu Sh.300,000.

 Aidha akizungumza na  Uhuru, mara baada ya kukamilika kwa mbio hizo, Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Nyamagana,Raphael Shillatu alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kuhamasisha wananchi.


 “Mchezo huu ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia michezo ili kuleta hamasha kwa vijana kwani  michezo ni ajira, pia huleta Mshikamano, Umoja, Upendo, Utulivu na Amani na kukiwezesha chama kuwa na timu itakayofanya kazi pamoja na kuhakikisha ushindi kuanzia chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2015”Alisema Shillatu.

Aliongeza kuwa mkakati huo ni ahadi yake wakati akiwa  anagombea Kiti hicho kuwa atahakikisha anaimarisha michezo yote ifikapo maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama ikiwa ni pamoja na riadha ya Baiskeli, mpura wa Miguu kwa wanaume ,bao,na baadae kuanzisha michezo mbalimbali kwa wanawake ambao nduyo wenye hamasha kubwa  hadi ukomo wa Uongozi wake ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani kwa vitendo.

Aidha washindi hao walipewa vitita vya fedha zilizokuwa zimefugwa kwenye bahasha ambapo hata hivyo hazikutangazwa  kwa ajili ya usalama wao na kupewa bendera za CCM na mlingoti wake kupeperusha bendera hizo maeneo ya makazi yao.

No comments:

Post a Comment