Wednesday, February 13, 2013

MBWAMWITU HAWATATOWEKA TENA-SERENGETI




SERENGETI

Mkurugenzi  wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI) Dk.Simon Mduma amesema kuwa tishio la kutoweka Mbwa Mwitu katika hifadhi ya Serengeti kutokana na magonjwa mbalimbali ya mbwa litatoweka kwani tayari wamepata chanjo ili kuweza kumaliza magonjwa yanayosababisha kutoweka kwa Mbwa Mwitu.


Mbwa hao waliochukuliwa eneo la Loliondo wamefugwa katika Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa miezi mitatu hili likiwa ni kundi la pili lenye mbwamwitu 15 ambapo kundi la kwanza lilitolewa Agosti 30 mwaka huu likiwa na mbwamwitu 11 waliachiwa ndani ya hifadhi hiyo mwaka 1980 na kulikuwepo   Mbwa Mwitu wapatao 500.

Aidha Mbwamwitu wapatao 15 ambao walikuwa wamefugwa katika eneo la Nyamuma ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya juhudi za kuwarudisha wanyama hao ambao walitopotea miaka ya 1990 wanaendelea vizuri.


 Kukosekana kwa wanyama hao ndani ya hifadhi hiyo kumesababisha kukosekana kwa kivutio kingine muhimu ambapo watalii wanahitaji kuwaona.

Alitoa pongezi kwa  mashirika mbalimbal ikiwemo ofisi ya Rais,ambayo ilichangia Sh. M.30 kwa ajili ya mradi  wa mbwa mwitu kwani  imesaidia kuongeza kivutio muhimu.



Alisema kuwa kuna changamoto ambazo wanakabiliana nazo ikiwa ni pamoja mashirika mengi kutofadhili mradi huo ambapo kwa sasa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom ndio pekee iliyotoa ufadhili wa zaidi ya milioni 450.

Kutokana na kuruhusiwa kwa mbwamwitu hao sasa imeongezeka na kufanya idadi ya wanyama hao kufikia 26 ndani ya TANAPA ambapo Agosti 30 mwaka huu waliachiwa 11.


Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete aliagiza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kuhakikisha Mbwamwitu waliofunguliwa  katika mbuga ya Serengeti wanakuwa salama muda wote ili wasitoweke tena.


No comments:

Post a Comment