Sunday, March 7, 2010

(WASANII )PIA HABARI YA RAIS JK. TABORA.

Msanii wa The Comedy Orginal, Masanga Mkandamizaji,Emmanuel Mgaya akiteta jambo na wanafunzi wenzake katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Dar Es Salaam (DSJ).Masanja alipata Astashada( Cheti cha Utangazaji katika Chuo hicho Mwaka 2009, kufanya sherehe Disemba 12 mwaka huo huo katika,Uwanja wa Msimbazi Center.



Msanii wa Luninga,Simon Simalenga akituma Ujumbe, Pembezoni kwake ni mwanafunzi mwenzake,CR wa Darasa la Diploma IIA,Pendo Malogoi akisikilza kwa makini hoja zinazotolewa na wanafunzi wenzake hawapi pichani,nyuma yao ni Wanaofurahia jambo ni Mary na Eva-Sweet Israel Musiba(Picha na Codula Hechei).
HOJA:
Mwalimu wa Nidhamu akitoa Nasaha,Edwin Mpokasye ni Mwalimu wa Masomo
Radio na Research na Film.
SHUKRANI:

Naibu Mkuu wa Nidhamu,Madam Yusto Santipa akitoa shukrani kwa wanafunzi wanaohitimu Stashadada na Astashada katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Dar es Salaam (DSJ).Pia kwa Uongozi wa Chuo kwa kumteua kuwa Mwalimu Mkuu Msaidizi na Msimamizi wa Taaluma ya Habari( Coordinator of Studies) Novemba 2009.

SURA TOFAUTI ZA MKUU WA CHUO,REV.WILSON CHIDUO, ALIYEMALIZA MUDA WAKE.
AKISITIZA JAMBO.


HABARI KUTOKA TABORA ZIARA YA KIHISTORIA YA RAIS JK.
Na El - hadji Yuusuf
Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Halfani Mrisho Kikwete, kesho anatarajia kuvunja historia nchini kwa kufanya ziara katika kata ya kitunda wilayani Sikonge Mkoani Tabora, kwa kuwa Rais wa Kwanza kuitembelea kata hiyo toka Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, ameyasaema hayo alipokuwa akizungumza ba waandishi wa habari, kuwa Rais atafanya ziara hiyo mara tu baada ya kumaliza kulihutubia taifa kwenye kilele cha siku ya wanawake duniani.

Alisema kwa mujibu wa kumbu kumbu, kata ya Kitunda haijawahi kutembelewa na kiongozi wa ngazi za juu nchini kuanzia Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais tangu Tanzania ilipopata uhuru Disemba 9 mwaka 1961.

Alisema awali Rais kikwete, alipanga kuitembelea kata hiyo lakini alishindwa kufika katika kata hiyo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuharibu miundo mbinu ya barabara, lakini aliahidi kurejea na kufanya ziara nyingine katika kata hiyo.

Alisema akiwa kitunda Rais Kikwete ataweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Kitunda, ambacho pia kitakuwa na chumba cha Upasuaji kisha atafanya mkutano wa hadhara ambao utakuwa mkutano wa Kwanza kufanywa na Rais katika kata hiyo.

Machi 10 Rais kikwete, atakitembelea kijiji cha Milenia cha Mbola katika Tarafa ya Ilolanguru, wilayani Uyui Mkoani Tabora, ambapo atatembelea shamba la mkulima bora wa kijiji hicho na kisha kusalimiana na wananchi.

Rais kikwete anatarajia kurejea jijini Dar, mara baada ya kukamilisha ziara hiyo ya siku mbili mkoani Tabora.

Wakati huo huo Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kesho anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kitaifa yanaadhimishwa Mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya wanawake na watoto Magreth Sitta, Rais Kikwete atapokea maandamano ya wananchi saa 4 asubuhi katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini hapa na kisha kulihutubia Taifa kabla ya kuendelea na ratiba nyingine.

Waziri Sitta, alisema kuwa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yamebesha ujumbe Usemao " Baada ya miaka 15 ya Beijing wanawake wanaweza wapewe nafasi" huku serikali ikieleza imetekeleza mambo yapi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wanawake nchini.

HABARI KUTOKA ARUSHA.

NA SHAABAN MDOE,ARUMERU.

CHAMA cha kuweka na kukopa cha umoja wa vijana wa ccm kata ya Nkoharanga (UVCCM SACCOS) wilayani Arumeru kimepatiwa vitendea kazi ikiwemo komputa na printa venye thamani ya shilingi milioni 1,370,000 ili kusaidia chama hicho kufanya kazi zake kiufasaa.

Vifaa hivyo vimetolewa jana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Wililam Sarakikya baada ya kupokea maombi kutoka kwa wanachama wa saccos hiyo.

Sarakikya alisema ametoa vifaa hivyo baada ya kugushwa na juhudi za vijana wa chama cha mapinduzi baada ya kuamua kuanzisha saccos hili kujikwamua kimaisha.

Alisema vijana wameonyesha mwamko kuwa awatakiwi kuwa tegemezi kwani chama kinahitaji vijana wenye moyo wa kujituma na ubunifu kitu ambacho vijana hao wameonyesha kuwa nacho na kukifanyia kazi.

Alisema ilani ya chama cha mapinduzi haiwezi kutekelezwa kwa maneno bali kwa vitendo vijana wameonyesha kutekeleza hilo hivyo viongozi wao hawana budi kuwa unga mkono kwa kuwapa vitendea kazi ili waweze kutimiza hazma yao

"Vijana wakionesha kujikwamua viongozi inatubidi kuwa saidia mimi niliguzwa na changamoto walizonazo kwenye saccos yao hivyo sinabudi kuwasaidia na naahidi kuwa saidia zaidi hadi waweze kufikia malengo waliyojipangia"alisema Sarakikya.

Kwa upande wao vijana hao kwenye risara yao iliyosomwa na katibu wa UVCCM kata ya Nkoaranga Christopher Parangyo iliwataka viongozi wengine kuwa na moyo kama huo kwani vijana hao bado wanahitaji vitendea kazi vingine kama mashine ya kudurufu karatasi.

Naye mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Arumeru Gabriel Nnko aliwataka vijana wa maeneo mengine kuiga ubunifu wa vijana wa kata hiyo ili kujikwamua na maisha na kuwataka wasiwe tegemezi kwa umri wa ujana ndiyo umri pekee kwa kujipanga kimaisha.

Saturday, March 6, 2010

DSJ PICTURES

Msajili wa wanafunzi,Victor Sinka akisitiza wanafunzi kulipa ada.
Mkuu wa Nidhamu,Brother Edwin Mpokasye (Mwl wa Radio Broadcating,Film na Research alisitiza jambo.













MKUU WA CHUO MSAAFU AKITOA NASAHA.











Bi, Eva-Sweet Israel Musiba akiwa amejumuika na wenzake siku ya Baraza lake la Mwisho Chuoni hapo.Eva-Sweet ni Mwandishi wa habari wa kampuni ya Uhuru Publication limited.Amehitimu Stashahada ya Uandishi wa Habari Chuoni hapo. Pia aliwahi kugombea nafasi ya Urais akashindwa kwa kura mbili(2) tu! ameweka historia kubwa ya Chuo kwa chaguzi zilizowahi kufanyika hapo,kwa takribani miaka 10 ya Chuo. Na kuwa Mwanamke wa Kwanza kushinda kwa kishindo pia kwa wanaume pia haijawahi kutokea ushindani kama huo.
Hivi sasa ana nia kugombea Ubunge kupitia Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) Mkoa wa Mara.









PICHA ZA BARAZA LA WANAFUNZI (DSJ)




Mkuu wa Chuo Mstaafu Rev.wilson Chiduo akisikiliza maoni ya wanafunzi.






Viongozi wa serikali wa wanafunzi ya sasa. Isack Mpayo(RAIS) na Malika (Makamu wa Rais) aliyevaa miwani na ushungi mwekundu kichwani.

BARAZA LA WANAFUNZI (DSJ)

Mkuu Mpya wa Chuo cha uandishi wa habari cha DSJ,Joachim Rupepo aliyeweka mkono kinywani na Msajili wa wanafunzi, Victor Sinka na Mwalimu wa Somo la Photojournalism, wakifuatilia kwa karibu maoni mbalimbali ya wanafunzi katika mkutano wa wanafunzi(School Baraza) uliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana Chuoni hapo. Walimu wa Nidhamu,Madam Yusto Santipa(Cooridator of Studies) na Edwin Mpokasyewakisikiliza maoni ya wanafunzi wao siku ya Baraza la wanafunzi.
Siku hii ilikuwa ni baraza langu la mwisho kuhudhuria ambapo nilihitimu katika Chuo hicho na mahafali kufanyika Dec.12 mwaka 2009 katika Ukumbi wa Msimbazi Center.








Viongozi wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO),Saimon Simalenga Rais aliyeshinda kwa kura mbili tu! dhidi ya Mpinzani wake Eva-Sweet I. Musiba aliyeweka historia ya Chuo kwa kuongoza kwa kura nyingi zaidi kuliko inavyotajiwa kila Uchaguzi wa Chuoni hapo,John Magali(Makamu wa Rais) na Sada Nassor ambaye alikuwa mgombea katika nafasi ya Makamu wa Rais lakini wanawake walishindwa kumchagua kutokana na wanawake wenyewe kutoaminiana kuwa wanaweza kuongoza.Sada Nassoro alijiuzulu baadae katika nyanja ya siasa kwa madai kuwa alishinikizwa kugombea.





Tuesday, February 23, 2010

PICHA MBALIMBALI ZA WAKUBWA.

Aliyekuwa Waziri wa fedha,Mh.Bazil Pesambili Mramba akigonganisha glass na Mwandishi wa habari Bi.Eva-Sweet Musiba kama ishara ya kutakiana kheli katika uzinduzi wa bia aina ya Ndovu,iliyofanyika katika ufukwe wa ziwa victoria Yughlong,Jijini Mwanza.





Miss Tanzania akikabidhiwa bendera ya Tanzania na Mkurugenzi wa TIC kabla ya kwenda kwenye mashindano ya Urembo wa Dunia mwaka 2009,

Kajege baada ya kjushinda kesi atinga Bungeni rasmi,kajege anayeonyesha mikono alikata rufaa na kushindwa dhidi ya Mtamwega Muganywa wa Chama cha TLP.