NA SHAABAN MDOE,ARUMERU.
CHAMA cha kuweka na kukopa cha umoja wa vijana wa ccm kata ya Nkoharanga (UVCCM SACCOS) wilayani Arumeru kimepatiwa vitendea kazi ikiwemo komputa na printa venye thamani ya shilingi milioni 1,370,000 ili kusaidia chama hicho kufanya kazi zake kiufasaa.
Vifaa hivyo vimetolewa jana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Wililam Sarakikya baada ya kupokea maombi kutoka kwa wanachama wa saccos hiyo.
Sarakikya alisema ametoa vifaa hivyo baada ya kugushwa na juhudi za vijana wa chama cha mapinduzi baada ya kuamua kuanzisha saccos hili kujikwamua kimaisha.
Alisema vijana wameonyesha mwamko kuwa awatakiwi kuwa tegemezi kwani chama kinahitaji vijana wenye moyo wa kujituma na ubunifu kitu ambacho vijana hao wameonyesha kuwa nacho na kukifanyia kazi.
Alisema ilani ya chama cha mapinduzi haiwezi kutekelezwa kwa maneno bali kwa vitendo vijana wameonyesha kutekeleza hilo hivyo viongozi wao hawana budi kuwa unga mkono kwa kuwapa vitendea kazi ili waweze kutimiza hazma yao
"Vijana wakionesha kujikwamua viongozi inatubidi kuwa saidia mimi niliguzwa na changamoto walizonazo kwenye saccos yao hivyo sinabudi kuwasaidia na naahidi kuwa saidia zaidi hadi waweze kufikia malengo waliyojipangia"alisema Sarakikya.
Kwa upande wao vijana hao kwenye risara yao iliyosomwa na katibu wa UVCCM kata ya Nkoaranga Christopher Parangyo iliwataka viongozi wengine kuwa na moyo kama huo kwani vijana hao bado wanahitaji vitendea kazi vingine kama mashine ya kudurufu karatasi.
Naye mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Arumeru Gabriel Nnko aliwataka vijana wa maeneo mengine kuiga ubunifu wa vijana wa kata hiyo ili kujikwamua na maisha na kuwataka wasiwe tegemezi kwa umri wa ujana ndiyo umri pekee kwa kujipanga kimaisha.
No comments:
Post a Comment