Saturday, March 6, 2010

BARAZA LA WANAFUNZI (DSJ)

Mkuu Mpya wa Chuo cha uandishi wa habari cha DSJ,Joachim Rupepo aliyeweka mkono kinywani na Msajili wa wanafunzi, Victor Sinka na Mwalimu wa Somo la Photojournalism, wakifuatilia kwa karibu maoni mbalimbali ya wanafunzi katika mkutano wa wanafunzi(School Baraza) uliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana Chuoni hapo. Walimu wa Nidhamu,Madam Yusto Santipa(Cooridator of Studies) na Edwin Mpokasyewakisikiliza maoni ya wanafunzi wao siku ya Baraza la wanafunzi.
Siku hii ilikuwa ni baraza langu la mwisho kuhudhuria ambapo nilihitimu katika Chuo hicho na mahafali kufanyika Dec.12 mwaka 2009 katika Ukumbi wa Msimbazi Center.








Viongozi wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO),Saimon Simalenga Rais aliyeshinda kwa kura mbili tu! dhidi ya Mpinzani wake Eva-Sweet I. Musiba aliyeweka historia ya Chuo kwa kuongoza kwa kura nyingi zaidi kuliko inavyotajiwa kila Uchaguzi wa Chuoni hapo,John Magali(Makamu wa Rais) na Sada Nassor ambaye alikuwa mgombea katika nafasi ya Makamu wa Rais lakini wanawake walishindwa kumchagua kutokana na wanawake wenyewe kutoaminiana kuwa wanaweza kuongoza.Sada Nassoro alijiuzulu baadae katika nyanja ya siasa kwa madai kuwa alishinikizwa kugombea.





No comments:

Post a Comment