Saturday, March 27, 2010

KAMATI KUU KUKUTANA KESHO.

KAMATI kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha MApinduzi inakutna kesho jijini Dar es Salaam kwa kikao cha siku moja.

kikao hicho cha Kamati Kuu ambacho ni cha kawaida, kitafanyika chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Rais Jakaya halfan Mrisho Kikwete.

Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Yussuf Makamba,amezitaja agenda za kikao hicho kuwa ni pamoja na ile inayohusu maandalizi ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2010.

Agenda nyingine amesema ni ile inayohusu mapendekezo ya wana CCM watakaogombea nafasi ya Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Nafasi hizo zimekuwa wazi baada ya aliyekuwa Katibu Mwenezi,Sande Manala kujihuzulu kutokana na kashfa ya utapeli wa magari na Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini,Marehemu Hassan Biku.

uteuzi wa Mwisho wa wagombea kwa mujibu wa Katiba ya CCM kwa nafasi hizo hufanywa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM,Luten yussuf Makamba amesema kikao hicho cha Kamati Kuu kitapokea na kujadili Taarifa kuhusu masuala mbalimbali ya ndani ya Chama.

Wajumbe wote wa Kamati Kuu tayari wameishawasili jijini Dar es Salaam na kikao hicho kinatajiwa kuanza majira ya saa 5:00 asubuhi.

No comments:

Post a Comment