Sunday, March 7, 2010

HABARI KUTOKA RORYA WILAYA YA MARA.

MADIWANI 2 WACHANGIA WATOTO YATIMA TSH, MILIONI 36.800,000,00/=

NA:SAMSON CHACHA.

Madiwani wawili akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Charles Ochele na Kamanda wa Vijana Wilaya hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi , Lameck Airo , wamechangia Mfuko wa Watoto Yatima wilaya ya Rorya Jumla ya Sh. Milioni 36,800,000,00/= katika Harambee iliyofanyika Mwishoni mwa wiki katika Kanisa Katoliki, Obwele chini ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Michael Nsonganzila ,

Harambee hiyo ya kuwachangia Watoto yatima ilifanyika Feb 28 mwaka huu na kuhudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Rorya Kanali Bernadictor Kitenga na Mapadri kutoka wilaya za Rorya , Tarime na Musoma , ambapo Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili Bahati Bukuku alidumbuiza wananchi zaidi ya 2,000 waliofurika katika Harambee hiyo kwa ajili ya kuwachangia watoto Yatima Katibu Mwenezi wilaya hiyo, Samweli Kiboye alichangia sh 200,000,00/=

Akitoa shukurani hao waliofanikisha mchango huo,Askofu Nsonganzila alisema kuwa Viongozi hao wameonyesha Upendo wao kwa kuwasaidia watoto waliopoteza Wazazi wao ambapo Fedha hizo zitawasaidia kuwanunulia Chakula , Mavazi , Karo za Shule na Mahitaji mengine ya Lazima , na kuwaomba Wahisani na Watanzania Wenye Mapenzi mema kuwa na moyo wa kusaidia watoto Yatima.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Rorya Kanali Kitenga Aliyechangia 600,000,00/= alisema kuwa Viongozi na Wafanyabiashara katika Wilaya hiyo ya Rorya Waige mfano wa Madiwani hao wa kuchangia wasio jiweza , pia Watoto Yatima kwani hawakupenda kuwapoteza Wazazi wao ni Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kwamba Watu waliona Uwezo wasiwatenge Watoto hao kwani kutoa ni Moyo si Utajili , alisema mkuu huyo wa Wilaya bw, Kitenga ,

More News Please Contact:0788312145.

No comments:

Post a Comment