Sunday, March 7, 2010

(WASANII )PIA HABARI YA RAIS JK. TABORA.

Msanii wa The Comedy Orginal, Masanga Mkandamizaji,Emmanuel Mgaya akiteta jambo na wanafunzi wenzake katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Dar Es Salaam (DSJ).Masanja alipata Astashada( Cheti cha Utangazaji katika Chuo hicho Mwaka 2009, kufanya sherehe Disemba 12 mwaka huo huo katika,Uwanja wa Msimbazi Center.



Msanii wa Luninga,Simon Simalenga akituma Ujumbe, Pembezoni kwake ni mwanafunzi mwenzake,CR wa Darasa la Diploma IIA,Pendo Malogoi akisikilza kwa makini hoja zinazotolewa na wanafunzi wenzake hawapi pichani,nyuma yao ni Wanaofurahia jambo ni Mary na Eva-Sweet Israel Musiba(Picha na Codula Hechei).
HOJA:
Mwalimu wa Nidhamu akitoa Nasaha,Edwin Mpokasye ni Mwalimu wa Masomo
Radio na Research na Film.
SHUKRANI:

Naibu Mkuu wa Nidhamu,Madam Yusto Santipa akitoa shukrani kwa wanafunzi wanaohitimu Stashadada na Astashada katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Dar es Salaam (DSJ).Pia kwa Uongozi wa Chuo kwa kumteua kuwa Mwalimu Mkuu Msaidizi na Msimamizi wa Taaluma ya Habari( Coordinator of Studies) Novemba 2009.

SURA TOFAUTI ZA MKUU WA CHUO,REV.WILSON CHIDUO, ALIYEMALIZA MUDA WAKE.
AKISITIZA JAMBO.


HABARI KUTOKA TABORA ZIARA YA KIHISTORIA YA RAIS JK.
Na El - hadji Yuusuf
Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Halfani Mrisho Kikwete, kesho anatarajia kuvunja historia nchini kwa kufanya ziara katika kata ya kitunda wilayani Sikonge Mkoani Tabora, kwa kuwa Rais wa Kwanza kuitembelea kata hiyo toka Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, ameyasaema hayo alipokuwa akizungumza ba waandishi wa habari, kuwa Rais atafanya ziara hiyo mara tu baada ya kumaliza kulihutubia taifa kwenye kilele cha siku ya wanawake duniani.

Alisema kwa mujibu wa kumbu kumbu, kata ya Kitunda haijawahi kutembelewa na kiongozi wa ngazi za juu nchini kuanzia Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais tangu Tanzania ilipopata uhuru Disemba 9 mwaka 1961.

Alisema awali Rais kikwete, alipanga kuitembelea kata hiyo lakini alishindwa kufika katika kata hiyo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuharibu miundo mbinu ya barabara, lakini aliahidi kurejea na kufanya ziara nyingine katika kata hiyo.

Alisema akiwa kitunda Rais Kikwete ataweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Kitunda, ambacho pia kitakuwa na chumba cha Upasuaji kisha atafanya mkutano wa hadhara ambao utakuwa mkutano wa Kwanza kufanywa na Rais katika kata hiyo.

Machi 10 Rais kikwete, atakitembelea kijiji cha Milenia cha Mbola katika Tarafa ya Ilolanguru, wilayani Uyui Mkoani Tabora, ambapo atatembelea shamba la mkulima bora wa kijiji hicho na kisha kusalimiana na wananchi.

Rais kikwete anatarajia kurejea jijini Dar, mara baada ya kukamilisha ziara hiyo ya siku mbili mkoani Tabora.

Wakati huo huo Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kesho anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kitaifa yanaadhimishwa Mkoani Tabora.

Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya wanawake na watoto Magreth Sitta, Rais Kikwete atapokea maandamano ya wananchi saa 4 asubuhi katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini hapa na kisha kulihutubia Taifa kabla ya kuendelea na ratiba nyingine.

Waziri Sitta, alisema kuwa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yamebesha ujumbe Usemao " Baada ya miaka 15 ya Beijing wanawake wanaweza wapewe nafasi" huku serikali ikieleza imetekeleza mambo yapi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wanawake nchini.

No comments:

Post a Comment