Monday, October 25, 2010

DK BILAL AKIWANADI WABUNGE BUKOMBE NA BOGWE


AKISALIMIANA NA WAGOMBEA UBUNGE WA MAJIMBO YA BUKOMBNE NA BOGWE KAHAMA.

























NYOKA YAMPOKEA MGOMBEA MWENZA WA CCM

MKUU WA MKOA WA MARA,ENOS MFURU AKIWA NAE PIA MJUMBE WA BARAZA KUU L AWAZAZI MKOA WA DAR ES SALAAM,SALUM MADENGE JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI.

NYOKA AFANYA MAPOKEZI YAKE HAKUWA NA TAARIFA APATA MSHTUKO
NGONGOTI PIA HALIKUWA NYUMA KATIKA MAPOKEZI YAKE JIMBONI TARIME,SIRARI.
NGOMA ZA JADI ZIKIWA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA NGOMA ZETU ZINADUMISHWA.

mgombea Mwenza wa Urais alitafura hadi kwenye mti juu

ILIKUWA PATA SHIKA CCM BWANA INATOA WATU WA HEKIMA TIZNMA HIYOOO!!!



ZIARA YA DK GHARIB BILAL MKOA WA MARA







MGOMBEA MWENZA CCM NA JIMBO LA RORYA




Mgombea mwenz wa urais,kupitia CCM,Dk Gharib Mohammed Bilal akisalimina na mgombea ubunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo, wakati alipiwasili wilyani humo akitokea jimbo la Musoma Mjini.

MGOMBEA MWENZA CCM AMWAGA CHECHE SHY!!

MGOMBEA mwenza wa urais kupitia CCM,Dk. Mohammed Garib Bilal,ametoa onyo kali kwa wananasiasa wanaohubiri machafuko na kuwa siku zao zinahesabika.;

Akizungumza katika mikutano ya kampeni mkoani Shinyanga,Dk bila alisisitiza kuwa ,serikali ya CCM haiwezi kukaa kimya hasa kipindi hiki ambapo baadhi ya wanasiasa wameamua kwa makusudi kuhamasisha fujo na vurugu hali ambayo imesababisha mwanachama wa CCM, Stephen kwilasa kufariki dunia wilayani Maswa.

"hatuwezi hata siku moja kuwaachia wahuni kusmabaza propaganda za kuhamasisha vurugu hapa nchini.nchi hii ina sheria na taratibu zake na hawa wanaodhani madaraka yanapatikana kwa kufanya fujo hakika nawaambieni hawatafanikiwa ba hawatafika popote,”alisema Dk. Bilal katika kijiji cha Seg’wa kilichopo jimbola Maswa Magharibi.

Jimbo hilo awali lilikuwa likiongozwa na John Shibuda kupitia CCM,lakini alihamia CHADEMA baada ya kushindwa katika kura za maoni.

Dk Bilal alisema wananchi hawapaswi kusahau makubwa yaliyofanya na waasisi wan chi hasa Mwalimu Nyerere,kwa kuwakataa wapinzani wanaohubiri uvunjifu wa amani na kuwa kuna mipango mingi ambayo serikali chini ua CCM imeanga kufanya, alkini haitaweza kukfanikiwa kama watanzania wataanza tabia mbaya ya kuvamiana, kupigana na kuuana kwa sababu tu ya tofauti za kisiasa.

“Tumeongeza shukle za sekondari nyingi hata hapa Shinyanga.Mnajua kuwa zimesaidia sana kuwapatia watoto wetu maeneo ya kusoma. Mkakati wetu mpya ni kuzingatia walimu wa kutosha ba huduma nyingine kama vitabu,”alisema.

Dk Bilal alifafanua kuwa ujenzi wa barabara kuunganisha Mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi na umesiaidia kuwapungzia kero pale wanapohitaji bidhaa kutoka nje ya mkoa na kuwaomba wananchi hao kupima ahadi zinazotolewa na vyama vya upinzani kw akuwa zimejaa maneno matamu ambayo hayawezi kutekelezeka.

“Wanakuja na kusema watatoa kiola kitu bure, wanazungumza kutoa saruji kwa sh.5,000. hivi viwanda vitakuwa vya kwao? Wanazungumzia kusomehsa wanafunzi bure, katika shule zipi? Shule hizi hizi tulizojenga sise? Waulizeni maana wanazungumza mabo wasiyoyajua msikubaliane nao kwani hawana hoja hao: alisema na kuongez akuwa siku zote mtu asiye na hoja ndiye hupanga mipango mibovu kama hii ya kuhamasisha wafuasi wao kupiga watu.Naamini Shinyanga hamtakubali kuchafuliwa sifa nzuri ya ukarimu mliyonayo hwa wachaache tunawahesabia siku.

Dk Bilal yupo mkoani Shinyanga akitokea Mwanza,na anaelekea kahama.Huu ni Mkoa wa Mwisho kwa Tanzania Bara kufnaya mikutano ya kampeni ambapo atakuwa amekamilisha mwendo wa takribani kilometa 40,000 alipozunguka na msafara wake katika pande mbalimbali za nchi.

Oktoba 24 aatajia kufnaya mkutano mkubwa kisiwani Pemba ambapo taaifa za maandalizi ya Mkutano huo zinaelelza kuwa,ujumbe wa Bilal unatarajiwa kutoa salamu kwa chama cha CUF,ambacho kina ngome yake kiswani huo.

Dk Bilal anaongozana na mjumbe wa NEC Bi. Fatma Said mchumo na Mjumbe wa Baraza kuu la wazazi Mkoa wa Dar es Salaam. Salum Madenge.

Tuesday, October 19, 2010

CCM MARA YAENDELEA KUIMALIKA.

MGOMBEA Ubunge kwa tiketi ya CCM,jimbo la Musoma Mjini,Vedastus Mathayo Manyinyi akimnadi Mgombea udiwani kata ya Mwigobero,Ahmad Kitumbo wakati wa kampeni zake Wilayani humo zinazoendelea.

DC APOKEA HESHIMA KWA NIABA YA JK MAJITA.

MKUU wa wilaya ya Musoma,Godfrey Ngatuni,akipokea gwaride la heshima kwa niaba ya Amri jeshi Mkuu wa mjeshi ya Ulinzi na Usalama,Jakaya Kikwete wakati wa kufunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Bukumi Wilaya ya Musoma vijijini jana.

MKURUGENZI CCM AKINADI DIWANI WA BWERI

MKURUgENZI wa uchaguzi Mkuu CCM Taifa,Matson Chizi akimnadai mgombea udiwani kata ya Bweri,Deogratius Ndege.

Akisisitiza jambo katani Bweri

Mkuu wa Wilaya ya Musoma aliyevaa miwani,Dodfrey Ngatani akiwa na wahitimu wa mgambo wanawake wa kata ya Buruma jumla ya waliohitimu ni 165.





WANAMGAMBO WAHITIMU MAFUNZO

MUSOMA

MKUU wa wilaya ya Musoma,Godfrey Ngatuni,amevitaka vyombo vya ulinzi vya watu binafsi kuwapatia ajira askari waliopata mafunzo ya ulinzi kwa kuwa wanakuwa tayari wamepata uzoeufu wa kazi kuliko kuajili askari ambao hawana ujuzi wowote ili kuhakikisha usalama wa mali zao.
Aliyasema hayo jana wakati wa sherehe za kufunga mafunzo ya wanamgambo wapatao 250 wa vijiji vya Bukumi na Buruma Wilaya ya Musoma Vijijini,ambapo kati yao wanawake wapatao tisa walihitimu mafunzo hayo.
Alisema kuwa wanamgambo ni nguzo kubwa ya usalama wa wanachi kwa kuwa ndio wako karibu na wananchi zaidi na wafahamu wahalifu, hivyo ni vyema jamii kuwaheshimu na kuzingatia maamuzi yao ambao yanapelekwa kwa jeshi la polisi kutokana na makosa wanayofanya wahalifu pia kutokuwepo kwa vituo vya polisi hasa sehemu za vijijini.

Mafunzo hayo yaliyokuwa na lengo la kuimarisha usalama maeneo hayo hasa Busekera ambapo ni sehemu ya wafanyabishara walio wengi ambao ni wavuvi kutoka sehemu mbalimbali nchini ambapo wamekuwa wakivamiwa mara kwa mara na kunyanganywa mitubwi na nyavu zao na hivyo kusababisha wananchi hao kubaki katika hali duni ya maisha.

Wanamgambo hao watakuwa wanafanya ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na wanachi wa maeneo hayo ili kuimarisha ulinzi,na pale ambapo patakuwa hakuna uwezekano wa kuyakabiri majambazi sugu wametakiwa kutoa taarifa huska kwa jeshi la polisi Mkoani Mara ili kupamba nao zaidi.
Aidha amewataka kusimamia kikamilifu usalama wakati wa upigaji kura katika uchaguzi Mkuu wa oktoba 31 mwaka ambao utamchagua Rais,wabunge na Madiwani,na kuhakikisha wanakuwa kioo cha jamii kwa kufanya matendo mema, na kuacha kushirikiana na wahalifu pale ambapo baadhi yao wamekuwa wakijiunga nao kufanya uhalifu.

Wanamgambo hao watapewa vitambulisho na namba ambazo zitatambuliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kulinda usalama panapotokea matatizo katika nchi za nje na kupewa mafunzo zaidi ya kijeshi ili kuweza kupata ajira kwa vijana .
Alisisitiza pi kuwepo kwa mazoea ya wanachi kutoa ushirikiano pale ambapo panatakiwa kuwepo kwa zoezi la kuwatafuta wanamgambo na akina mama kujitokeza kwa wingi ili dhana ya 50 kwa 50 iweze kuboreka zaidi.

Thursday, October 14, 2010

NYERERE DAY.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma,Martin Msonganzila amevitaka vyama vya siasa kuwa makini katika Uchaguzi Mkuu kwa kuwa Baba wa Taifa alipenda nchi na Uchaguzi kuwa wa Amani na Utulivu.

Baba Askofu aliyasema hayo jana wakati wa sherehe za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kanisa la Mtakatifu Maria la Mwitongo Butiama na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha malumbano ambayo yanaweza kuhataraisha amani ya Nchi yetu kitu ambacho Baba wa Taifa alikuwa hapendi.

“Katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu,viongozi wa vyama vya siasa wasiwe ndo wachochezi katika kuvurugu amani ya nchi hii kwani kufanya hivyo si kumuenzi Baba wa Taifa”.Alisema Askofu Msonganzila.

Alisikitishwa pia kutowepo viongozi mbalimbali katika sherehe hizo pia wakazi wa Butiama kutoshiriki kikamilifu katika sherehe hizo ambzo ndo hasa kumbkumbu na siku muhimu kitaifa ambayo kila Mtanzania anapaswa kuenzi siku hii kwa mema yote aliyofonya baba wa Taifa katika Taifa hili na nchi nyingine za jirani.

Katika sherehe hizo ambazo wawakilishi kutoka nchi jirani kama Uganda walihudhuria na kuwataka Watanzania waeje mfano wao kuwa kumuenzi kikamilifu Baba wa Taifa kwani hata wao wana siku yao maalum ya kumuenzi ambayo ni Juni 1 kila mwaka kwa kumwombea kwa Mungu kuwa Mtakatifu.

Akizungumza mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Nyerere,Mwenyekiti wa kamati ya kumwombea kwa ajili ya mchakato wa kumwombea kuwa Mtakatifu nchini Uganda,Emmanuel Katumba alisema kuwa nchini Uganda pia wameanzisha siku kama hii ili kumuenzi kwani alifanya mengi mazuri katika ukombozi wa mji huo kuhakikisha Amani na utulivu uliopo Tanzania uwepo na Uganda.

Pia wameanzisha vipindi maalumu vua redio,magazeti na luninga kwa lengo la kuwasisitiza kumwombea ili kuharakisha mchakato mzima kwa kumwombea ili awe mtakatifu na kuanzisha midahalo,pia kutembelea makumbukusho mbalimbali ya kihistoria yalioyopo Uganda kama Namugongo na kibeo ya Rwanda.

Naye Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya mchakato wa kumwombea awe Mtakatifu, Tumwekwase Columbus alisema kuwa moja ya kazi za kikamati hiyo ni kuhakikisha inapanga mikakati mbalimbali ya kufanikisha sherehe hizo na kubuni mikakati mingine mipya na motisha kwa wakazi wa Uganda kutambua mkombozi wao wa Taifa ni Baba wa Taifa,Hayati Julius Nyerere kwa ajili ya kuboresha.

Wakati nchi za jirani wakifanya siku hiyo kwa umakini zaidi,nchini Tanzania siku hii imeonekena kuwa ya wana familia na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na vyama vya siasa kuienzi,bila kuwepo kwa viongozi wowote wa kitaifa,Jambo o ambalo kwa siku za usoni siku hii itaonekana kama mzaha.


Tuesday, October 12, 2010

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM AFUNIKA MARA.

Khadija Kopa anafanishwa na Mmiliki wa Blog hii? angalia je kuna ukweli ndani yake?
Umati wa watu uliofurika katika viwanja vya Mukendo Mjini Musoma wakati wa kampeni za kujinadi kwa mgombea wa Urais Jakaya Halfani Mrisho kikwete.

Muhidin Issa Michuzi akiwa na Manyerere Jackton,magwiji wa habari nchini Tanzania.Wakiwa katika kijiji cha Busekela katika kampeni za Rais Jakaya Kikwete ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

RAIS WA KWANZA KUFIKA MAJITA BUSEKELA






RAIS



JAKAYA KIKWETE NDIYE RAIS WA KWANZA KUFIKA MAJITA KIJIJI CHA BUSEKELA.

PICHA ZOTE NI ZA KIJIJI HICHO.
NI JIRANI NA UKEREWE MWANZA ENDAPO WAKAZI HAWA WATAKUWA NA KIVUKO.