Tuesday, October 19, 2010

WANAMGAMBO WAHITIMU MAFUNZO

MUSOMA

MKUU wa wilaya ya Musoma,Godfrey Ngatuni,amevitaka vyombo vya ulinzi vya watu binafsi kuwapatia ajira askari waliopata mafunzo ya ulinzi kwa kuwa wanakuwa tayari wamepata uzoeufu wa kazi kuliko kuajili askari ambao hawana ujuzi wowote ili kuhakikisha usalama wa mali zao.
Aliyasema hayo jana wakati wa sherehe za kufunga mafunzo ya wanamgambo wapatao 250 wa vijiji vya Bukumi na Buruma Wilaya ya Musoma Vijijini,ambapo kati yao wanawake wapatao tisa walihitimu mafunzo hayo.
Alisema kuwa wanamgambo ni nguzo kubwa ya usalama wa wanachi kwa kuwa ndio wako karibu na wananchi zaidi na wafahamu wahalifu, hivyo ni vyema jamii kuwaheshimu na kuzingatia maamuzi yao ambao yanapelekwa kwa jeshi la polisi kutokana na makosa wanayofanya wahalifu pia kutokuwepo kwa vituo vya polisi hasa sehemu za vijijini.

Mafunzo hayo yaliyokuwa na lengo la kuimarisha usalama maeneo hayo hasa Busekera ambapo ni sehemu ya wafanyabishara walio wengi ambao ni wavuvi kutoka sehemu mbalimbali nchini ambapo wamekuwa wakivamiwa mara kwa mara na kunyanganywa mitubwi na nyavu zao na hivyo kusababisha wananchi hao kubaki katika hali duni ya maisha.

Wanamgambo hao watakuwa wanafanya ulinzi shirikishi kwa kushirikiana na wanachi wa maeneo hayo ili kuimarisha ulinzi,na pale ambapo patakuwa hakuna uwezekano wa kuyakabiri majambazi sugu wametakiwa kutoa taarifa huska kwa jeshi la polisi Mkoani Mara ili kupamba nao zaidi.
Aidha amewataka kusimamia kikamilifu usalama wakati wa upigaji kura katika uchaguzi Mkuu wa oktoba 31 mwaka ambao utamchagua Rais,wabunge na Madiwani,na kuhakikisha wanakuwa kioo cha jamii kwa kufanya matendo mema, na kuacha kushirikiana na wahalifu pale ambapo baadhi yao wamekuwa wakijiunga nao kufanya uhalifu.

Wanamgambo hao watapewa vitambulisho na namba ambazo zitatambuliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kulinda usalama panapotokea matatizo katika nchi za nje na kupewa mafunzo zaidi ya kijeshi ili kuweza kupata ajira kwa vijana .
Alisisitiza pi kuwepo kwa mazoea ya wanachi kutoa ushirikiano pale ambapo panatakiwa kuwepo kwa zoezi la kuwatafuta wanamgambo na akina mama kujitokeza kwa wingi ili dhana ya 50 kwa 50 iweze kuboreka zaidi.

No comments:

Post a Comment