Monday, October 25, 2010

MGOMBEA MWENZA CCM AMWAGA CHECHE SHY!!

MGOMBEA mwenza wa urais kupitia CCM,Dk. Mohammed Garib Bilal,ametoa onyo kali kwa wananasiasa wanaohubiri machafuko na kuwa siku zao zinahesabika.;

Akizungumza katika mikutano ya kampeni mkoani Shinyanga,Dk bila alisisitiza kuwa ,serikali ya CCM haiwezi kukaa kimya hasa kipindi hiki ambapo baadhi ya wanasiasa wameamua kwa makusudi kuhamasisha fujo na vurugu hali ambayo imesababisha mwanachama wa CCM, Stephen kwilasa kufariki dunia wilayani Maswa.

"hatuwezi hata siku moja kuwaachia wahuni kusmabaza propaganda za kuhamasisha vurugu hapa nchini.nchi hii ina sheria na taratibu zake na hawa wanaodhani madaraka yanapatikana kwa kufanya fujo hakika nawaambieni hawatafanikiwa ba hawatafika popote,”alisema Dk. Bilal katika kijiji cha Seg’wa kilichopo jimbola Maswa Magharibi.

Jimbo hilo awali lilikuwa likiongozwa na John Shibuda kupitia CCM,lakini alihamia CHADEMA baada ya kushindwa katika kura za maoni.

Dk Bilal alisema wananchi hawapaswi kusahau makubwa yaliyofanya na waasisi wan chi hasa Mwalimu Nyerere,kwa kuwakataa wapinzani wanaohubiri uvunjifu wa amani na kuwa kuna mipango mingi ambayo serikali chini ua CCM imeanga kufanya, alkini haitaweza kukfanikiwa kama watanzania wataanza tabia mbaya ya kuvamiana, kupigana na kuuana kwa sababu tu ya tofauti za kisiasa.

“Tumeongeza shukle za sekondari nyingi hata hapa Shinyanga.Mnajua kuwa zimesaidia sana kuwapatia watoto wetu maeneo ya kusoma. Mkakati wetu mpya ni kuzingatia walimu wa kutosha ba huduma nyingine kama vitabu,”alisema.

Dk Bilal alifafanua kuwa ujenzi wa barabara kuunganisha Mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi na umesiaidia kuwapungzia kero pale wanapohitaji bidhaa kutoka nje ya mkoa na kuwaomba wananchi hao kupima ahadi zinazotolewa na vyama vya upinzani kw akuwa zimejaa maneno matamu ambayo hayawezi kutekelezeka.

“Wanakuja na kusema watatoa kiola kitu bure, wanazungumza kutoa saruji kwa sh.5,000. hivi viwanda vitakuwa vya kwao? Wanazungumzia kusomehsa wanafunzi bure, katika shule zipi? Shule hizi hizi tulizojenga sise? Waulizeni maana wanazungumza mabo wasiyoyajua msikubaliane nao kwani hawana hoja hao: alisema na kuongez akuwa siku zote mtu asiye na hoja ndiye hupanga mipango mibovu kama hii ya kuhamasisha wafuasi wao kupiga watu.Naamini Shinyanga hamtakubali kuchafuliwa sifa nzuri ya ukarimu mliyonayo hwa wachaache tunawahesabia siku.

Dk Bilal yupo mkoani Shinyanga akitokea Mwanza,na anaelekea kahama.Huu ni Mkoa wa Mwisho kwa Tanzania Bara kufnaya mikutano ya kampeni ambapo atakuwa amekamilisha mwendo wa takribani kilometa 40,000 alipozunguka na msafara wake katika pande mbalimbali za nchi.

Oktoba 24 aatajia kufnaya mkutano mkubwa kisiwani Pemba ambapo taaifa za maandalizi ya Mkutano huo zinaelelza kuwa,ujumbe wa Bilal unatarajiwa kutoa salamu kwa chama cha CUF,ambacho kina ngome yake kiswani huo.

Dk Bilal anaongozana na mjumbe wa NEC Bi. Fatma Said mchumo na Mjumbe wa Baraza kuu la wazazi Mkoa wa Dar es Salaam. Salum Madenge.

No comments:

Post a Comment