Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma,Martin Msonganzila amevitaka vyama vya siasa kuwa makini katika Uchaguzi Mkuu kwa kuwa Baba wa Taifa alipenda nchi na Uchaguzi kuwa wa Amani na Utulivu.
Baba Askofu aliyasema hayo jana wakati wa sherehe za kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kanisa la Mtakatifu Maria la Mwitongo Butiama na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kuacha malumbano ambayo yanaweza kuhataraisha amani ya Nchi yetu kitu ambacho Baba wa Taifa alikuwa hapendi.
“Katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu,viongozi wa vyama vya siasa wasiwe ndo wachochezi katika kuvurugu amani ya nchi hii kwani kufanya hivyo si kumuenzi Baba wa Taifa”.Alisema Askofu Msonganzila.
Alisikitishwa pia kutowepo viongozi mbalimbali katika sherehe hizo pia wakazi wa Butiama kutoshiriki kikamilifu katika sherehe hizo ambzo ndo hasa kumbkumbu na siku muhimu kitaifa ambayo kila Mtanzania anapaswa kuenzi siku hii kwa mema yote aliyofonya baba wa Taifa katika Taifa hili na nchi nyingine za jirani.
Katika sherehe hizo ambazo wawakilishi kutoka nchi jirani kama Uganda walihudhuria na kuwataka Watanzania waeje mfano wao kuwa kumuenzi kikamilifu Baba wa Taifa kwani hata wao wana siku yao maalum ya kumuenzi ambayo ni Juni 1 kila mwaka kwa kumwombea kwa Mungu kuwa Mtakatifu.
Akizungumza mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Nyerere,Mwenyekiti wa kamati ya kumwombea kwa ajili ya mchakato wa kumwombea kuwa Mtakatifu nchini Uganda,Emmanuel Katumba alisema kuwa nchini Uganda pia wameanzisha siku kama hii ili kumuenzi kwani alifanya mengi mazuri katika ukombozi wa mji huo kuhakikisha Amani na utulivu uliopo Tanzania uwepo na Uganda.
Pia wameanzisha vipindi maalumu vua redio,magazeti na luninga kwa lengo la kuwasisitiza kumwombea ili kuharakisha mchakato mzima kwa kumwombea ili awe mtakatifu na kuanzisha midahalo,pia kutembelea makumbukusho mbalimbali ya kihistoria yalioyopo Uganda kama Namugongo na kibeo ya Rwanda.
Naye Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya mchakato wa kumwombea awe Mtakatifu, Tumwekwase Columbus alisema kuwa moja ya kazi za kikamati hiyo ni kuhakikisha inapanga mikakati mbalimbali ya kufanikisha sherehe hizo na kubuni mikakati mingine mipya na motisha kwa wakazi wa Uganda kutambua mkombozi wao wa Taifa ni Baba wa Taifa,Hayati Julius Nyerere kwa ajili ya kuboresha.
Wakati nchi za jirani wakifanya siku hiyo kwa umakini zaidi,nchini Tanzania siku hii imeonekena kuwa ya wana familia na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na vyama vya siasa kuienzi,bila kuwepo kwa viongozi wowote wa kitaifa,Jambo o ambalo kwa siku za usoni siku hii itaonekana kama mzaha.
No comments:
Post a Comment