Sunday, December 25, 2016

ASKOFU MSONGANZILA AHIMIZA AMANI.



JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI.


Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Michael Msonganzila amewataka wananchi kuwa na Amani ambayo kila binadamu anapaswa kuenenda nayo kwani ukikosa amani hutaweza kupata nafasi ya kufanya shughuli za maendeleo.

Yameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya jimbo la Katoliki Dayosisi ya Musoma, kuwa kutokuwa na binadamu anapaswa kumpenda mwenzake kwa kujijengea moyo wa kusameheana,kupatana,kunyenyekeana katika uajibikaji wa shughuli za kijamii.

‘’Mwaka 2008 nilikuja kufanya kazi kama mtumishi katika kuhudumia wananchi wa Mkoa wa Mara katika shughuli mbalimbali za wananchi kwa kutoa elimu na malezi ili waweze kuwa tegemeo la nchi na lengo likiwa kudumisha Amani, ambaponimeweza kufanya juhudi katika miaka minane na kuhakikisha amani inapatikana katika Mkoa wa Mara,ambapo mapigano ya koo za waryachori na waryanchonka katika wilaya ya Tarime yamekwisha’’ Alisema Msonganzila.


Amesema wao kama taasisi ya dini wanaanzisha darasa maalum Nyegina Sekondari kwa mabinti wanaokimbia ukeketaji majumbani kwao ambapo watasoma kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni kupigwa msasa kisha wataanza masomo kama kawaida.

Amesema kwa kufanya hivyo mabinti hao watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao na katika kijiji wanachotoka hivyo kusaidia kuepuka majanga kama ukeketaji.



Amesema kuna uwezekano wa wananchi kukumbwa na uhaba wa ukosefu wa chakula kutokana na hali ya hewa na mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo ametoa wito kwa wananchi hususani wilaya ya Tarime kuacha tabia ya kuuza chakula nchini Kenya kwani, Serikali imekuwa ikigharamika tena kununua chakula nchini Kenya ambacho wananchi wa Tarime ukiuza.

Kuhusu mwenendo wa utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya tano Askofu huyo alisema kuwa mwelekeo wa serikali kwa sasa umekuwa ni mtetezi wa haki kwa wananchi wanyonge ingawa wengine hawafurahii hali hiyo kutokana na kuzibiwa mianya huku mizizi ya rushwa ikithibitiwa kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment