Wednesday, December 14, 2016

WAIGIZAJI FILAMU MKOA WA MARA WANOLEWA.

WIZARA ya habari, utamaduni, sanaa na Michezo kupitia bodi ya Filamu Tanzania imetoa mafunzo kwa waigizaji wa filamu Mkoa wa Mara ya kuwajengea uwezo waigizaji wa filamu ili waweze kuendesha kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Akifungua warsha hiyo ya siku tatu katika Shule ya Sekondari ya Mara, Kaimu katibu Mkuu, Wizara ya habari,Utamaduni, sanaa na michezo, Nuru Milao aliwataka kutumia mafunzo hayo kwa weredi mkubwa ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuutangaza Mkoa wa Mara na vivutio vyake.

Alisema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo wadau hao ili waweze kuongeza pato lao na Taifa kwa ujumla kwa kuwa wakifanikiwa wataweza kulipa kodi ya maendeleo kwa Taifa lao.

Akitoa salamu za kumkaribisha mgeni, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Joyce Fissoo alisema kuwa inashangaza kuona kuwa wachezaji wa filamu wengi wao nchini Tanzania wanaonyesha filamu za mapenzi peke yake bila kufanya utafiti wa kina na wakati kuna vivutio vingi vizuri nchini hapa ambavyo wanapaswa kuvionyesha katika filamu zao wawapo kazini.

Alisema kuwa kazi nyingi zinakataliwa kuruka hewani kutokana na mahudhuhi mabaya kwa mtanzania, ambayo kifamilia ambayo hayajengi bali kubomoa, kazi ambazo amesema kuwa huwa hawaruhusu kazi hizo zitolewa kwenye luninga.
“Kunataka kutambua kazi zenu kama zina ubora, hatutaki kuzuia, nia yetu ni kujenga ili kuwajengea uwezo nyie, ambapo mwaka jana filamu zipatazo 55 zilifanyiwa marekebisho” alisema Fissoo.

Naye Rais wa Shirikisho la filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba aliwataka waigizaj kufanya kazi kwa kujituma bila wasiwasi wa kuibia kazi zao, na kwamba Serikali imetoa fursa na haki ya kulinda kazi zao ili kila msanii aweze kuneemeka kupitia kazi yake.

Akitoa mada katika warsha hiyo, Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam, Richard Ndunguru, alisema kuwa wasanii wanapaswa kuwa na uandishi wa Script iliyo bora ambayo inalenga uwe na wazo au msukumo ambao ndio msingi unaoweza kumjenga muandaaji na kwamba hadithi yake inapagwa katika mfumo wa namba ambapo mada zipatazo 11 zitazungumzwa.




No comments:

Post a Comment