Tuesday, December 27, 2016

NYUMBANI KWA HAYATI MWALIMU NYERERE KUFANYIKA VIKAO VYA WABUNGE.





WABUNGE wa Mkoa wa Mara wakiwemo, wabunge wa afrika Mashariki wameamua kufanya kikoa cha kujadili maendeleo ya Mkoa nyumbani kwa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere Mwitongo kijijini Butiama wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara, kila mwaka ili kumuenzi Baba wa Taifa.

Kikao hicho kilifanyika siku ya sikukuu ya zawadi ya kuzaliwa Yesu kristo nyumbani Mwitongo kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika ukumbi uliondaliwa kwa ajili ya mazungumzo ambacho kilikuwa kinaongozwa na mwenyekiti wao ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini Pro. Sospeter Muhongo.

Wabunge hao walisema umefika muda muafaka wa kuungana kwa pamoja na kuacha itikadi za vyama vya siasa pembeni ili kuweza kusimamia na kuendeleza shughuli za maendeleo kwa vitendo ili wananchi waondokane na umaskini na kujikwamua kiuchumi na mkoa huo uweze kusonga mbele .

Mbunge wa Jimbo la Mwibara Kangi Lugola akitoa maazimio yaliyoazimiwa kwa niaba wabunge hao alisema masuala waliyoweka kipaumbele ni pamoja na kusimamia vizuri kwa kushirikiana na serikasa hali yake sio nzuri na kuhakikisha hakuna mwananchi ambaye atakufa kwa njaa.
Aidha vipaumbele vingine vilikuwa ni ujenzi wa hospitali ya Kwangwa ambayo itaitwa Kwangwa hospital ya rufaa ambayo imetengewa Sh Bilioni 5.5 ambayo imepekezwa imalizike katika awamu hii ya uongozi wa Rais John Magufuli.

Aidha wabunge hao waliitaka Wizara ya Mali asili na Utalii kutenga uzio kwa ajili ya kutenganisha hifadhi ya Mbuga ya Serengeti na wananchi, ambapo wanyama aina ya Tembo wamekuwa wakivamia mashamba na kuhatarisha maisha wanadamu na kusabaisha njaa kali kwa wananchi.

Kuhusu michezo walisema kuwa michezo ni ajira, hivyo timu ya polisi Mara ambayo iko nyuma kimechezo itaimarisha ikiwa pamoja na michezo mingine kama riadha ambayo historia yake ya kuwa wakimbiaji kutoka Mkoa wa Mara imefutika.




No comments:

Post a Comment