Tuesday, December 27, 2016
MUHONGO AJA NA MIRADI MIPYA JIMBONI KWAKE.
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini amewapatia mradi wa Sungura, Kuku na mradi wa kilimo cha mchaichai wananchi wa jimbo lake ambao utawakwamua kiuchumi na kuwa na maendeleo endelevu na kuepuka umasikini uliokidhiri miongoni mwao.
Akitambulisha kampuni ya kubuni na kutengeneza kazi za kujiajiri nchini Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo (TBCC), Elibariki Mchau alisema kuwa yuko tayari kuanza mafunzo kwa wajasiriamlai wadogo walio katika vikundi ili waweze kuanza ufugaji mapema na kujipatia pato ambapo Mbunge huyo aliamua kutoa mbegu za sungura na mbegu za mchaichai kwa viukundi vitakavyokuwa tayari kupokea mradi huo.
Ame kuwa mradi huo ni mradi wa biashara ambao unatoa ajira na kipato kikubwa na endelevu hivyo wanapaswa watatoa mafunzo hayo na mbinu za kuendesha miradi hiyo na usimamizibora ili kuhakikisha mkulima anazalisha kwa tija na kpata fadi kubwa zaidi ambapo pia kwa upande wa masoko wao watawaletea soko na kabla ya hapo watatoa mikataba ambao utamuhakikishia huduma bora mkulima na mfugaji.
Aidha akizungumzia juu ya mkojo wa mnyama huyo alisema kuwa mkojo wake ni kiwatilifu kwa ajili ya kupambana na wadudu wahribifu wa mazao ya kilimo na ni kiwatilifu kisichoo na kemikali ambapo kinyesi chake ni mbolea iliyo bora kwa mazao hasa mboga mboga na huisha udongo haraka na kurejesha uoto wa asili haraka.
Kwa upande mwingine nyama yake ni bora ambayo uaazwa kwa kilo moja sh.8,000, ambapo sungura mmoja anao uwezo wa kuzalisha sungura kati ya 60-100 kwa mwaka endapo atatuzwa vizuri na atampatia mfugaji kiasi cha sh. Milioni 1.4 – Milioni 2.4 na kwa kuwa ufugaji huu hufanywa kwa jozi yenye sungura jike 6 na dume moja, hivyo mfugaji atajipatia kipato cha Sh Milioni 8.6 hadi Milioni 14.4 kwa jozi moja kwa mwaka kama pato ghafi.
Kuhusu mradi wa kuku aina ya (super solomony), mradi huo utahusisha kumfuga kuku ambaye anatoa mazao ya kuku wa aina tatu, akiwemo kuku wa nyama(broiler), kuku wa kienyeji ajili ya supu na kupika pia mayai yenye kiini cha njano(yellow-york) ambayo pia hutotolewa.
Akizungumzia kuhusu mradi wa kilimo cha mchai chai, Afisa Utafiti wa kampuni hiyo, Selemani Boko alisema kuwa ekari moja ya mchai chai mbichi kwa ajili ya mafuta hutoa mavuno ya majani kilo 4,000 na majani makavu yaliyokaushwa kwa jua kilo 700, na ekari kwa moja kwa shamba moja litavunwa kwa misimu mitatu yenye mavuno 11 kwa mpando mmoja na kutoa faidi ya sh Milioni 4.8 kwa mwaka.
Katika mkutano wa hadhara wananchi wa kata hiyo walipiga nderemo, vigeregere na vifijo na kuupokea mradi huo ambapo wasio na vikundi vilisisajiliwa kuamua kukaa wakiongozwa na viongozi wao kuunda vikundi vya miradi hiyo, ambapo pia madiwani waliupokea mradi kwa kila kata ambapo kata zilizoko kwenye mwambao wa ziwa wamepewa mradi wa kilimo cha mchai chai na kata zingine ufugaji wa Sungura ambazo, baadhi ya kata ni Bwasi, Lusoli, Mugango, Bukumi-Busekela, Bukima, lifulifu,Nyakatende,Tegeruka na Nyegina
Aidha maamuzi ya fedha za mfuko wa jimbo pia yalifanyika katika kata hiyo,katika mkutano wa hadhara ambao pia uliwashirikisha madiwani wa halmashauri ya Musoma na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Vicent Naano kwa pamoja waliamua fedha za mfuko wa jimbo zinunue mbegu na mashine ya kukamua mafuta ya Alizeti.
Fedha za mfuko wa jimbo kiasi cha Sh. Milioni 38,347 zitanunua mbegu za Muhogo (Vipando) zipatazo 532,000 katika vijiji 68 yenye thamani ya Sh. Milioni 16, ambapo sh. Milioni 21.9 zitanunua mashine ndogo za kukamua mafuta ya Alizeti ambazo zitafugwa katika ofisi ya kata kwa afisa kilimo kila kata.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment