Sunday, June 10, 2018

WAZIRI LUKUVI AKIANGALIA MPAKA WA KENYA.



Mtaalamu wa upimaji, Huruma Lugalla akimwonyesha Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi moja ya alama zilizopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya Wilaya ya Rorya kijiji cha Kilongwe Mkoa wa Mara, kushoto kwa mtaamu huyo ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adamu Kigoma Malima na aliyevaa kofia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Doroth Mwanyika.

Tuesday, May 29, 2018

IJUE TFDA



TFDA herufi zake zimetafsiriwa kwa lugha ya kiingireza ikiwa na maana ya Tanzania Food and Drugs Authority, ikiwa na maana kuwa Mamlaka ya Chakula na dawa Tanzania.


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi


TFDA imepewa madaraka ya kufanya maamuzi mbalimbali ya kiutendaji kwa mujibu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 na ile ya Wakala za Serikali, Sura 245
Mamlaka ilianza kutekeleza majukumu yake rasmi tarehe 1 Julai, 2003

Dira ya TFDA ni kuwa Mamlaka inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa wote
Dhima ya Mamlaka ni kulinda afya ya jamii kwa kuzuia madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi

Majukumu ya TFDA

Kutathmini na kusajili vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi
Kudhibiti utengenezaji, uingizaji na usambazaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba na vitendanishi
Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa viwanda vya utengenezaji na maeneo ya mauzo ya bidhaa zinazodhibitiwa ili kuhakikisha viwango vilivyowekwa vinafikiwa


Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakikisha kuwa bidhaa husika zinafikia viwango vya ubora na usalama
Kusimamia majaribio ya dawa mpya na vifaa tiba
Kutoa leseni na vibali mbalimbali vya kuendeshea biashara ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba

Kudhibiti utoaji wa matangazo ya biashara ya bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA
Kuratibu madhara yatokanayo na utumiaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
Kuelimisha jamii kuhusu ubora, usalama na matumizi sahihi ya bidhaa zinazodhibitiwa

Mamlaka ina ofisi saba (7) za Kanda ambazo ni kaskazini, Arusha, Manyara, Tanga, na Kilimanjaro, kanda ya ziwa, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mwanza na Kagera, kanda ya mashariki, Pwani na Dar es Salaam,kanda ya kati, Dodoma, Morogoro na Singida,Kanda ya juu Kusini Mbeya Iringa, Njombe Songwe na Rukwa , kanda ya Kusini, Mtwara, Lindi na Ruvuma, kanda ya Magharibi ni Tabora, Kigoma na Katavi.
Muundo.


Mamlaka pia inashirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa katika kuhakikisha kuwa sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 inatakelezwa ipasavyo
Baadhi ya madaraka na majukumu ya TFDA yamekasimiwa kwa Halmashauri chini ya Kifungu Na. 121 cha Sheria na kupitia Kanuni za Kukasimu Madaraka na Majukumu ya TFDA kwa Halmashauri (GN No. 476) za mwaka 2015 na marekebisho yake GN No. 19 ya mwaka 2017

Wadau wa Mamlaka
Wizara na Idara mbalimbali za serikali
Mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi mbalimbali
Mashirika ya kimataifa (WHO, FAO, UNICEF)
Watengenezaji, waingizaji nchini, wasambazaji na wauzaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
Vyombo vya Habari (Wahariri/Waandishi)
Wasimazi mbalimbali wa sheria
Wafanyakazi wa sekta ya Afya na watafiti
Vyama vya wafanyabiashara wa bidhaa zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwa ni pamoja na wajasiriliamali
Watoa huduma mbalimbali
Walaji, watumiaji na wananchi wote kwa ujumla


Mafanikio

Kuwa na mifumo ya usajili, ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara wa bidhaa
Kufikia kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015 katika utendaji bora wa kazi
Maabara ya dawa ya TFDA kutambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)
Maabara ya Chakula na Mikrobiolojia ya TFDA kupata ithibati (Accreditation) kwa kiwango cha kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005
Kusogeza huduma karibu na jamii kwa kufungua ofisi saba (7) za Kanda na kuajiri wakaguzi katika vituo vya forodha Kuboresha ufanisi katika utoaji huduma kwa kutumia mifumo ya TEHAMA
maombi mbalimbali kufanyiwa kazi kwa njia ya mtandao (online system)
Kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa kutoa taarifa za madhara yatokanayo na
dawa (ADR reporting system) Mifumo mingine –LIMS, HR-MIS

Changamoto zinazoikabili Mamlaka
Jamii kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu majukumu ya TFDA na hivyo kutokutoa mchango wa kutosha katika kuhakikisha kuwa sheria inatekelezwa
Kutokuwepo kwa mifumo iliyowianishwa ya udhibiti wa bidhaa kati ya Tanzania na nchi za jirani (EAC, SADC, n.k)

Mabadiliko ya haraka ya teknologia, utandawazi na soko huria unaosababisha ongezeko la bidhaa katika soko hivyo kuongeza ugumu wa udhibiti
Kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu na wadau wasiofuata masharti ya sheria kwa hiari


Friday, May 18, 2018

Ajali Mbaya yatokea Musoma.


Ajali ilitokea Mei 13 katika eneo la Nyasho, baina ya gari aina ya scania namba T299 BXR likiwa na kibeba mizigo namba T858 BTB, lililokuwa linaendeshwa na Masha Mstapha ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo,ambapo aligonga gari aina ya Nadia Namba T248 BSG ambapo Didi Msira Koko na mkewe, Joyce waliumia vibaya na kukatika miguu ambapo wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.dreva wa bajaji ya harusi, Baraka Suguti hali yake pia siyo nzuri, yeye anaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Musoma, anasema hana uwezo angeenda Mwanza, scania hilo liliingia kwenye duka spea za magari la Mang'ombe Joseph.

Sunday, January 28, 2018

WAZIRI MKUU NA UWANJA WA NDEGE MUSOMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, juu ya ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Musoma katika uwanja wa ndege wa Musoma ambayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mara. Kiwanja hicho kitajengwa hivi karibuni, uwanja huu ukimalizika utaongoza pato la Mkoa wa Mara na Manispaa ya Musoma.

Wednesday, December 6, 2017

MBUNGE MATHAYO ATOA MILIONI 1.7 ZA KUONGEZA MITAJI KWA WAFANYABIASHARA.



MUSOMA.

WAKAZI wa kata ya Nyamatare wamemwomba Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Mathayo kuhakikisha anawaletea maji katika soko la biashara la Nyamatare kwani wanatumia maji ya dimbwi la maji machafu yaliyochimbwa kwa ajili ya ujenzi wa Choo katika soko hilo.

Wameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara wa kutambulisha viongozi wapya wa Wilaya hiyo waliochaguliwa katika chaguzi zilizopita wiki iliyopita.

Mkazi wa kata hiyo, Christina Mori ambaye ni mfanyabiashara katika soko hilo alisema kuwa kutokana na huduma duni ya maji iliyopo wanalazimika kuchota maji kwenye dimbwi la maji machafu kwa matumizi ya kuosha viazi vitamu ambavyo kwa kawaida huwa na udongo kutokana na kutokuwa na maji hali mbayo inahatarisha afya ya wananchi hao.

Changamoto zilizopo katika soko na kata hiyo kwa ujumla ni pamoja na huduma ya choo,uvujaji wa maji ovyo kutokana na ujenzi wa miundo mbinu ya barabara na mitaro.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma, Magiri Maregesi ametoa wiki mbili kwa mamlaka ya maji safi na taka Manispaa ya Musoma, (MUWASA) ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa ukakika kwani ulazaji wa mabomba ya maji umeishamalizika na uko mita kadhaa kuelekea katika soko hilo.
Naye Diwani wa kata hiyo, Masumbuko Magesa aliilalamikia Mamlaka hiyo kwa uzembe uliofanyika wa kutowasiliana kati ya mamlaka zote,na kusababisha mabomba ya maji kuwa ya ya mitaro ahali ambayo inahatarisha usalama wa mabomba ambayo yanaweza kuhujumiwa na ahata kuharibika.

Kwa upande wa vivuko vya barabara, Diwani huyo alilalamikia ucheleweshaji wa ujenzi wa vivuko ambao inawalazimu wananchi kupata hadha kubwa wakati wa matatizo yanapotokea hasa kwa upande wa huduma ya maziko ama panapotokea mgonjwa hali ambayo inawaletea hadha kubwa wananchi wa eneo hilo.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma, Fidelica Muyovella alisema kuwa barabara ya Nyasho-Nyamatare-Majita inahitaji jumla ya vivuko 65 lakini vitajengwa vivuko 20.
Katika kuongeza mitaji kwa wanawake wajasiliamali, Mbunge huyo alitoa kiasi cha Sh. Milioni 1.7 akishirikiana na viongozi wapya waliochaguliwa ili kuinua uchumi wa mwanamke na kuahidi kuwajengea mabanda mengine,ikiwemo uzio na choo.

Thursday, November 30, 2017

MJUE MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA MARA (Musoma Mjini)


Mmiliki wa Blog hii akiingia katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mara, amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mara kutoka Wilaya ya Musoma, na alishinda kwa kishindo katika nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa, ikiwa ni Wilaya moja ya Musoma, ikiwa imeungana na Musoma Vijijini ambayo ni Wilaya kichama kwa sasa.

WAGOMBEA WAKIJINADI.


Wegesa Hassan Witimu akipiga magoti kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Mkoa wa Mara, kuomba ridhaa ya kuwa Mwenyekiti,katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa CCM, Mkoa wa Mara, Wilaya ya Musoma Mjini.

WAJUE WAGOMBEA WA UWT MKOA WA MARA.


Wagombea wa nafasi ya kiti cha Umoja wa Wanawake(UWT) Mkoa wa Mara, wa kwanza ni Veronica Mwijarubi Kunenge(138), Mwajuma Hamisi Magoti(55) na Wegesa Witimu akishinda kwa kura 245.

Sunday, November 19, 2017

MAONESHO YA KILIMO MSETO MUSOMA-MARA

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adamu Kigoma Malima, akikagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya VI- Agro forest,Bweri Musoma.

KILIMO MSETO-MUSOMA



MKUU wa Mkoa wa Mara,Adamu Malima, amesema kuwa ili kuendeleza kilimo cha mkataba cha pamba katika Mkoa wa Mara haina budi kushirikiana kwa dhati kwa vikundi vya wakulima kuwa pamoja na kuhakikisha kilimo cha pamba kinakuwa kwa kasi kwa maendeleo ya Mkoa wa Mara.

Akizungumza katika kilele cha maonesho ya kilimo mseto kwa niaba yake,yaliyomalizika jana Afisa kilimo Mkoa wa Mara, Dennis Nyakisinda alisema kuwa ili vikundi vya wakulima viweze kupata tija ya kilimo bora haina budi kituo cha sasa kilimo Mseto cha (Vi Agroforestry) cha na kanisa la AICT Dayosisi ya Mara na ukerewe kiwe kituo cha mafunzo ya kilimo mseto cha Mkoa wa Mara ambacho kitakuwa kitovu cha mafunzo ya kilimo bora na ufugaji.

‘’Kituo hiki kitakuwa kitakuwa bora cha mfano kwa masuala mbalimbali jinsi ya kupanda miti,kutambua majina ya miti, ufugaji, ukulima wa kisasa kwa ajili ya maendeleo ya mkoani hapo na nchini kwa ujumla’’Alisema Nyakisinda.


Aidha alitaka Shirika la viwanda vidogo vidogo(SIDO) Mkoa wa Mara kuhakikisha linawashaidia wajasiliamali ili wapate uwezo kwa kupata ujuzi ili waweze kuanzisha vyao wenyewe kwa ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto za tabia nchi hawana budi kuzingatia kilimo mseto ambacho ndicho kilimo pekee chenye tija.

Ameongeza kuwa wakati huu ni wakati wa mapinduzi ya viwanda na kwamba kilimo mseto ndiyo injini pekee ya maendeleo ya mapinduzi ya viwanda nchini na kwamba wakulima hawana budi kushirikiana na mashirika mbalimbali ili kuweza kufanikiwa katika kukuza uchumi wa viwanda na kuyataka madhehebu mengine kuiga mfano wa kanisa la AICT kwani bila kuwa na chakula hakuna ibada.




Amewashukuru wafadhili wa Shirika la Vi Agroforestry la nchini Sweden na Kanisa la AICT la Dayosisi ya Mara na Ukerewe kwa kuwa kipaumbele kwa kuchangia nguvu kubwa ya kupanda miti ili mkoa huo uwe na mandhari nzuri na kuzitaka na taasisi nyingine kuwaunga mkono.

Maonesho hayo ya kilimo cha mseto ya siku tatu alipambwa na mabanda ya maonesho ya bidhaa mbalimbali zikiwemo, utengenezaji wa mkaa wa udogo uliochanganywa na kinyesi cha Ng’ombe, ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa,utengenezaji wa sabuni ya maji, mche na mbegu bora aina ya Mkombozi.


Wednesday, October 18, 2017

MWALIMU WA SEKONDARI AWA MWENYEKITI UVCCM MUSOMA VIJIJINI



Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Murangi, Martine Juma Chacha, akijieleza katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki,kata ya Mugango, Wilaya ya Musoma Vijijini, wakati akiomba kura,aliibu mshindi kwa kupata kura 150, akifuatiwa na Jackson Nyakia kikomati ambaye alipata 124.

Saturday, June 3, 2017

Makamu wa Rais awasili Mwitongo-Butiama


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alipokelewa na Chifu wa kabila la Wazanaki, Chifu Japheti Wanzagi, mara baada ya kuwasili alasiri katika Kijiji cha Mwitongo,alipozaliwa na kuzikwa mwasisi wa Taifa la Tanzania mzaliwa wa Mkoa wa Mara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

EWURA yawataka wazalishaji wa Gesi kupunguza gharama za mtungi.

BUTIAMA.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewataka wafanyabiashara wa mafuta ya gesi asilia kupunguza kiwango cha kununua gesi kwa watumiaji ili wananchi wa kipato cha chini waweze kuhimiri bei ya gesi na kuwasaidia katika kupunguza matumizi ya ukataji miti ovyo unosasabisha kutoweka kwa uoto wa asili ambapo kwa sasa watumiaji wa mkaa wanaongezeka na kusababisha mazingira kuharibika.


Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Mamlaka hiyo, kuwanja wa Mwenge-Mwitongo Wilaya ya Butiama, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Kanda ya Ziwa,Nyirabu Musira,amesema kuwa upunguzaji wa bei utasababisha upungufu wa matumizi ya mkaa ambao ulikuwa ukitumiwa na wananchi.

Hii ni katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa inafanyika kijijini Mwitongo Wilaya ya Butiama alipolelewa na kuzikwa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Leo kuna kongamano la hifadhi ya Mazingira linaloendelea katika Ukumbi wa Romani Katoliki jirani na kanisa alilokuwa anasali Baba wa Taifa, ambapo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba.

Gosol na mapambano dhidi ya Utunzaji wa Mazingira.


Mratibu wa mradi wa Shirika lisilo la kiserikali la Gosol la nchini
Finland,Heikki Lindfors kwa kushirikiana na Taasisi ya global Resource
Allience ya Madaraka Nyerere ya Mjini Musoma alitoa maelezo kwa
wananchi na waandishi wa habari waliofika katika banda la maonesho
nchini ambapo wamebuni mashine inayotumia mwanga wa jua kuoka mikate
itakayosaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na itatoa mashine hiyo
kwa vikundi vya akina mama bure na kutoa mafunzo kwa vijana wapatao
watano ya kutengenezaji wa mashine hiyo ambayo hapo zitauzwa nchini.

Saturday, May 27, 2017

WAKALA WA VIPIMO MKOA WA MARA WACHACHAMAA



MUSOMA.

Wakala wa vipimo Mkoa wa Mara (WMA),umewataka wasafirishaji kutumia
mizani kwa mujibu wa Sheria ya vipimo sura nambari 340 pamoja na
marekebisho yake ya mwaka 2002 ambayo inamtaka kila msafirishaji
kupima mizigo inayosafarishwa.


Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vipimo duniani ,katika
ofisi za mabasi yaendayo Mikoani katika kata ya Bweri Manispaa ya
Musoma, Afisa vipimo Mwandamizi, Almachius Pastory alisema kuwa
wamiliki wa mabasi wanapaswa kuwa na mizani ili waweze kutumia vipimo
kwa manufaa yao kwa kuzingatia uzito wa gari na kuepuka ajali
sizizokuwa za lazima wawapo katika safari.

Wakizunugmza kwa nyakati tofauti baadhi ya wasafirishaji wenye mizani
wa kampuni ya Musoma express, Veronica Innocent ambaye ni Mhasibu
alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wateja
kukataa kupimiwa mizigo yao na matokeo yakewa kupata hasara kwa
kupigwa faini katika mizani kwa kuzidisha uzito kwenye mabasi yao.


Alisema kuwa kuwa na mzani ni faida kwa wateja lakini wengi wao
wanaonekana kuwa hawana elimu ya faida ya kuwa na mzani ambayo endapo
utazidisha mzigo unasababisha uchakavu katika basi na kuwaomba
maafisa hao kutenga muda wao kwa ajili ya kutoa elimu kwa
wasafirishaji juu ya faida na hasara za kutokuwa na mzani.



Akitoa elimu kwa baadhi ya wasafirishaji katika stend ya mabasi
yaendayo Mikoani katika ofisi ya kampuni ya usafirishaji ya Ndiyo Mzee
Afisa Vipimo Mkoa wa Mara, Paulini Chilato alisema kuwa wakala wa
vipimo kazi yake ni kujua vipimo sahihi na endapo gari litazidi uzito
uliotakiwa unapaswa kupigwa faini na ili kuondoka na karaha hiyo ni
vyema uwe na mzani ili kujua kiwango sahihi kinachotakiwa cha kubeba
mzigo.


Naye Warioba Ngara wa kampuni ya usafirishaji ya Ndiyo Mzee alisema
kuwa atahakikisha kuwa na mzani huo kwani walikuwa wanafahamu mzani
unaotumika ni wa barabarani pekee na walikuwa wanatumia mzigo kwa
kuuangalia kwa macho na au kutumia uaminifu kwa mteja anapozungumza
kuwa gunia moja lenye nafaka lilijazwa mara mbili linachukua kilo
100 (lumbesa) na wanakubali kupakia katika basi.


‘’Nashukuru kupata elimu hii,nimepata ufahamu juu ya basi linapaswa
kuwa na ujazo wa kiwango kilichoandikwa kwa mujibu wa sheria,na
nimefahamu kuwa nikiwa njiani nasafiri salama nikiwa na uhakika wa
kufika salama na kuepuka faini zisizo za lazima’’Alisema Ngara.

Thursday, May 4, 2017

Banda la Monyesho-Solar Appropriate Technology-Mei Mosi


Mwalimu kutoka nchini Korea, Dk.Hong-Kyu Choi akitoa maelezo ya jinsi kifaa cha kutumia umeme wa jua na kuchaji simu kinachofanya kazi katika banda la umoja wa vijana wa Wilaya ya Serengeti waliohitimuu mafunzo ya kutengeneza kifaa hicho ambapo jumla ya vijana 91 wamehitimu,hao ni MKuu wa Magereza Mkoa wa Mara, ACP,Golleha Massunzu na Mkuu wa gereza Wilaya ya Srengeti,Masanja Maharangata.

Wakurugenzi na Mei Mosi

Eng.Bishanga wa Tanroads Mara,mfanyakazi bora.