Monday, December 31, 2012
TUKO MILIONI 44,929,002
MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI TUKO Watanzania.Milioni 44,92902.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema tumeongezeka sana kutoka mika ile na kufikia M.35. na kwamba Tanzania alisemakufikia mwaka 2016 tutakuwa M.51.
Amezitaka familia kutambua umuhimu wa kupanga uzazi, kwani kutakuwa kwa kazi kubwa hapo mbeleni kutokana na hali ya Uchumi, na kwamba ni lazima tufanye kazi kwa juhudi na maarifa.
WAGENI KUTAMBULISHWA KWA WENYEVITI WA MITAA.
KATIKA kuhakikisha hali ya Ulinzi na Usalama inaimarika, katika manispaa ya Musoma, wananchi wa kata 13 za Wilaya ya Musoma wametakiwa kutoa taarifa za wageni wao kwa Wenyeviti wa Mitaa,Mkuu wa Wilaya ya Musoma,Jackson Msome,amewaambia wananchi wa kata za Nyakato,Bweri na Nyasho kwa nyakati tofauti kuhusu usalama wao na kuwatambua wageni wanaoingia majumbani kwao.
kuhusu mauaji ya kutisha ya kukatwa watu vichwa yapo lakini idadi si iliyotajwa.na ni Wilaya jirani,
Kumekuwa na makundi ya watoto kati ya umri wa miaka 19-28 ambao wanajiita mdomo wa furu, mbio za vijiti, Jamaica mokaz,wanaume nenge, west lawama, wanaovamia raia wema kwa kuwakata na nyembe, kuchoma visu na kufanya uvamizi katika majumba.
Aidha amewatoa hofu wananchi wa Mji wa Musoma kuhusu taarifa isiyo sahihi ya mauaji ya watu 17 ya kukatwa vichwa, na kwamba katika matukio hayo hakuna mauaji ya watu hao bali ni uvamizi wa kawaida na kwamba tukio la mauaji ya mtu kukatwa kichwa lipo lakini si idadi iliyotajwa na ni kwa Wilaya ya Butiama.
Thursday, December 20, 2012
TUZO YA WALIMU BORA 2012-2013 CHANGAMKIENI JAMANIIII
DAR ES SALAAM
Uongozi wa Education and Expedition Agency Association kwa niaba ya kamati na bodi ya usimamizi wa tuzo hizi za walimu bora Tanzania awali ya yote tunapenda kuungana nanyi leo hii hasa kwa lengo kuu maalumu juu ya Uzinduzi wa tuzo za walimu bora Tanzania kwa mwaka 2012-2013.
Mchakato wa tuzo hizi za walimu bora Tanzania ulianza rasmi mwaka 2010 kwa kufanya tafiti takribani mikoa 18 na wilaya zake hasa kwa lengo la kutaka kujua na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na walimu juu ya changamoto walizo nazo.
Kila mmoja wetu hapa anatambua na hata watanzania walio wengi wanatambua kabisa na kuguswa na changamoto zinazowakabili walimu hapa nchini, katika kufahamu na kwa kusikia hata sauti za walimu wenyewe.
Baada ya kukamilika kwa utafiti wetu uliofanyika kwa kipindi cha miaka (2) moja ya vitu ambavyo tuliona kuwa itakuwa ni sehemu ya msingi katika kuwapatia motisha walimu ni juu ya kuandaa tuzo hizi ambazo malengo yake makuu ni kurudisha hadhi na heshima ya walimu na kiwango cha elimu kilicho polomoka.
Walimu hapa nchini wamekuwa na mapito makubwa na changamoto nyingi za kimaisha pamoja na sehemu zao za kazi, walimu wamekuwa ni jamii ambayo haina thamani ndani ya nchi hii, sauti zao wamepaza kadri wawezavyo lakini hakuna sikio linalopokea sauti zao hata kidogo. Je tujiulize jamii hii ambayo leo haina mtu wakusikia sauti yao madhara yake ni nini katika taifa hili hasa kwa mujibu wa kazi zao?
Hakuna taifa lolote duniani ambalo limeendelea na kupata mafanikio makubwa katika Nyanja zake zote bila msingi bora wa elimu, nasi tumegundua msingi bora wa elimu huanzia kwa mwalimu, Ikumbukwe taifa letu ni taifa changa ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi hasa kielimu, asilimia ya watanzania wasio jua kusoma na kuandika kwa vijana na watu wazima imekuwa ikiongezeka kwa kasi hali ambayo ni hatari kubwa sana kwa taifa letu hasa kwa mfumo tulionao wa kiulimwengu wa kuwa kijiji kimoja kutokana na ukuaji wa kitekonolojia nk.
Ikumbukwe kuwa hata kiwango cha ufauru kinachozidi kushuka kwa shule za msingi/sekondari na vyuo kila mwaka hakuna mchawi anae sababisha hali hiyo ni kutokana na walimu kupuuzwa, kudharauliwa kuanzia kijamii chini hadi watu wa juu, mpasuko uliopo kati ya walimu na elimu inayopaswa kutolewa ni kubwa kutokana na walimu kuvunjika moyo na hali ya kujitoa katika ufundishaji? Walimu ni wazalendo thabiti sana na jamii isiyo na makuu jamii inayovumilia mapito yote, lakini bado inabeba mzigo mkubwa wa kutoa elimu katika kuifundisha jamii katika kuikoa na ujinga na kuipa maarifa stahiki kwa mstakabali wa taifa.
Ili kurudisha na kuinua kiwango cha elimu hapa nchini msingi mkubwa hasa wa kuzingatia ni juu ya kuwajali na kuwathamini walimu, tunaona jitihada nyingi zinaelekezwa kwenye vitu vingi katika sekta ya elimu, kama ujenzi wa vyoo, madarasa, mabweni, nk lakini ukweli utabaki pale pale vyote unaweza kuwanavyo lakini je tujiulize vyote hivyo ni msingi wa elimu bila mwalimu. Sisi tuna amini kuwa ujenzi mzuri huanza na msingi, na katika vyote hivyo bila kujenga msingi wa walimu vyote ni sawa na bule.
Katika kutimiza adhima ya kuwa asasi ya mfano hapa nchini tumeona ni vema sasa kuelekeza nguvu ya kujenga msingi wa walimu katika kuwapa motisha ambazo tuna amini kwa nafsi moja au nyingine zitaweza kurudisha moyo na msukumo kwa walimu katika kujitoa kufundisha vizuri shuleni kwa sababu tuzo hizi ni tuzo endelevu ambazo zitakuwa zikifanyika kila baada ya mwaka, Kotokana na vigezo vya kushiriki tuzo hiyo vinalenga zaidi wajibu wa mwalimu katika kufanya kazi yake kwa usahihi basi mwalimu akiona mwalimu mwenzie amepata tuzo mwaka huu naye ataongeza juhudi na maarifa katika kazi yake ili naye apate tuzo ambayo italeta matokeo mazuri kwa wanafunzi wetu na kiwango cha elimu nchini kitapanda, kwa kutoa tuzo hiyo kwa mwanadamu wa kawaida tunaamini anaweza asiamini kuwa ndio chachu ya kurudisha hadhi, Heshima kwa mwalimu na elimu nchini lakini ni ukweli usio pingika matunda yake yataonekana hapo baade hapa nchini hasa matokeo ya utafiti tuliyo fanya.
Kwa mara ya kwanza tuzo hizi zitashirikisha walimu wa shule za msingi na walimu wa shule za sekondari kwa pande zote mbili shule za serikali na shule binafsi,pia tuzo hizi zitashirikisha walimu wa shule maalumu, na kuanzia mwaka 2015 tuzo hizi pia zitajumuisha hadi Zanzibar ili kutoa fursa kwa walimu nao kule kushiriki tuzo hizi
Kamati ya uratibu imeweza kuandaa kamati ya kutosha itakayo simamia usahili na vigezo katika kuwapata walimu bora kamati inayo ongozwa na Dr Wilson mahera Charles kutoka chuo kikuu cha dare s salaam kitivo cha hesabu (mathematics)Ambaye atashirikiana na wajumbe wengine 10 ambao ni walimu wastaafu,waratibu kutoka katika asasi za kielimu.
Vigezo vya kushiriki tuzo hizi za walimu bora tanzania
Ili mwalimu aweze kuingia na kushiriki katika shindano la utoaji wa Tuzo kwa walimu bora Tanzania, ni lazima awe na vigezo vifuatavyo;-
Awe raia wa Tanzania
Awe na umri kati ya miaka 18 – 54
Awe na cheti cha kuzaliwa au cheti cha darasa la saba, au kitambulisho cha kupigia kura au pasi(passport) ya kusafiria
Awe ameajiliwa kazi ya uwalimu kuanzia kipindi cha miaka mitano na kuendelea
Awe na mahudhurio mazuri kazini na kuhudhuria vipindi vyote vya kufundisha darasani
Awe ni mtu wa kujitoa kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini
Awe muadilifu kazini na katika jamii anayoishi
Awe anayejua wajibu wa kutimiza malengo ya kazi yake kwa kuandaa;-
(i)Azimio la kazi (ii)Andalio la somo (iii)Andalio la notes
9. Awe na Haiba inayo jitosheleza
10. Awe na Ushirikiano mzuri kati yake na walimu wenzie na wanafunzi kwa ujumla
11. Awe na uwezo wa kutosha katika kushauri walimu, wanafunzi, viongozi na jamii kwa ujumla
12. Awe mbunifu na anayemudu kukabiliana na changamoto zilizopo mfano;-mazingira duni ya kazi yake nk.
13. Asiwe na tuhuma za rushwa au aliye wahi kuwa na kosa la jinai
14. Awe anavaa uasilia kwa vitendo
15. Awe na matokeo mazuri kwa wanafunzi kwa ngazi zote anazo fundisha
16. Awe ameajiriwa na serikali au sekta binafsi
17. Awe tayari kushiriki mambo ya jamii mfano;- michezo,mazingira,majanga, nk.
18. Awe anaendana na sera ya elimu
19. Awe anaye kubalika na wafanyakazi wenzie na hata wanafunzi kwa ujumla
20. Asiwe amecha kazi ya uwalimu na kurudia kazi ya uwalimu
21. Awe amesomea taaluma ya uwalimu katika chuo/vyuo vinavyotambulika kiserikali.
Mchakato utakavyo endeshwa katika kuwapata washindi
Tutaanza kufanya mchakato wa kusambaza fomu za washiriki mikoa yote hapa nchini hadi wilayani na fomu hizo zitapatikana kupitia matawi yote ya benki ya posta Tanzania wakiwa ni miongoni mwa wafadhili wa tuzo hizi. sababu zilizopelekea fomu kutokwenda sawa na uzinduzi huu ni kutokana na kuchelewa kukamilika kwa taratibu zilizo jitokeza nje ya uwezo wetu.
fomu hizo zitaanza kupatikana rasmi kuanzia Desenba 15/2012 hadi februari 10/2013 na ndio utakuwa mwisho wa kuchukua fomu. jinsi ya kuwahamisisha walimu kujitokeza kuchukua fomu hizo tumeandaa matangazo yatakayokuwa yakitolewa na vyombo vya habari hapa nchini hususani ITV na Redio ONE ambao ni wafadhili wetu.
Baada ya walimu kuwa wamekamilisha zoezi la kuchukua fomu hatua itakayo fuata walimu watatangaziwa tarehe za usahili kila mkoa kupitia vyombo vya habari.
Baada ya usahili matukio yote ya uendeshaji wa tuzo hizi ikiwa ni pamoja na kuanzia ngazi za mikoa, ngazi ya kanda hadi ngazi ya Taifa yote yatakuwa yakiratibiwa kupitia kipindi maalumu kitakacho itwa ni wakati wa mwalimu kupitia ITV hadi siku ya kilele cha utoaji wa tuzo hizo Tarehe 25/11/2013.
Ndani ya mchakato huo utakavyo kuwa unaendelea pia tutatoa fursa kwa wananchini kushiriki kutoa maoni ya mwalimu mulengwa ambaye wanaishi naye karibu na kupiga kura kupitia namba maalumu ya simu za mkononi itakayo tangazwa hapo baadae ikiwa ni pamoja na fursa ya watu kutoa maoni kupitia tovuti yetu na mitandao ya kijamii.
Zawadi za washindi watakao shinda tuzo hizi ni kama ifuatavyo-:
A- washindi katika makundi 2 upande wa s/msingi na sekondari ni kama ifuatavyo?
mshindi 1- milioni 40 taslimu, pamoja na ufadhili wa kusoma kwa mwaka million 5 kwa miaka mitatu milioni 15. Jumla kuu million 55
Mshindi wa 2- million 30 taslimu, pamoja na ufadhili wa kusoma kwa mwaka million 4 kwa miaka 3 jumla million 12. Jumla kuu million 42.
Mshindi wa 3 – million 20 taslimu, pamoja na ufadhili wa kusoma kwa mwaka million 3 kwa miaka 3 jumla million 9. Jumla kuu million 29
Mshindi wa 4 – million 10 taslimu, pamoja na ufadhili wa kusoma kwa mwaka million 2 kwa miaka 3 jumla million 6. Jumla kuu million 16
Mshindi wa 5 – million 5 taslimu, pamoja na ufadhili wa kusoma kwa mwaka milion 2 kwa miaka 3 jumla million 6. Jumla kuu million 11
washindi wa sita hadi 10 kila upande watapata pikipiki mojamoja zenye thamani ya milioni 2,na laptop yenye thamani ya milioni 1.5 jumla milioni 3,500,000/= kila mmoja atapata zawadi yenye thamani ya 3,500,000/=
Washindi wa masomo kila somo moja watakuwa washindi 10 s/msingi washindi kumi 10 s/sekondari na jumla ya somo moja lina washindi 20 na mosomo yapo sita jumla watakuwa washindi 120, ambao watapata zawadi ya Tshs laki 3 na baiskeli 1 yenye thamani ya laki mbili kwa kila mshindi.
Na masomo hayo yatakayo shindaniwa ni kama itutavyo-:
1. Sayansi
2. Hisabati
3. kiswahili
4. Geograph
5. Historia
6. English
Ifuatayo ni taarifa ya Harambee ya kuchangia Mchakato wa Tuzo za walimu bora uliofanyika tarehe 2 november 2012 katika ukumbi wa Diamond jubilee V.I.P.
Siku ya harambee tulifanikia kupata kiasi cha sh. 42,000,000/= na ahadi walizotoa wananchi ni kiasi cha sh. 143,000,000/= na bado tunaendelea kupokea ahadi na kufuatilia ahadi zilizotolewa siku ya harambee
Na mwisho kabisa tunapenda kutoa ombi kwa wafadhili wengine waweze kujitokeza zaidi katika kufadhili tuzo hizi ili tuweze kutoa zawadi kwa walimu wengi zaidi.
Waandishi wa habari na vyombo vyote vya habari tunapenda kutoa ombi letu kwenu katika kuzitangaza vema tuzo hizi.
Pia na chukua fursa hii kuwashukuru wafadhili waliojitokeza Benki ya posta Tanzania, ITV na Redio one Vio company ltd,wise company limited,ipo professional ltd,na wote walioshiriki kuchangia kwa namna moja au nyingine tuzo hizi za walimu bora tanzanania.
Ahsanteni
Clemence A.Kambengwa
M/kiti EEAA
TENGA AWASHUKURU WALIOPIGIA KURA WARAKA
DAR ES SALAAM
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kupigia kura waraka wa marekebisho ya Katiba, kwani wametimiza wajibu wao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema marekebisho ya Katiba ni jambo muhimu, lakini lazima yapate ridhaa ya wanaohusika ambao ni wajumbe.
“Nawasukuru wajumbe kwa kupitisha jambo hili. Nawashukuru wote, waliokubali na waliokataa. Ndivyo demokrasia ilivyo. Tulitaka waseme ndiyo au hapana, hivyo tulitarajia kupata majibu yoyote kati ya hayo mawili.
Marekebisho mengine yalikuwa ni maelekezo (directives) kutoka FIFA na CAF. Katiba yetu inasema tutatekeleza maagizo ya CAF na FIFA, lakini kwa misingi ya utawala bora tuliona ni lazima tupate ridhaa kutoka kwa wajumbe,” amesema.
Jumla ya wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 waliunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba.
Vipengele vilivyoingizwa katika marekebisho hayo ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Vilevile Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.
Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
RAMBIRAMBI MSIBA WA AMINA SINGO
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa mtangazaji wa habari za michezo katika kituo cha redio cha 100.5 Times FM, Amina Singo kilichotokea usiku wa kuamkia jana.
Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti kupitia taaluma ya uhandishi wa habari, Amina alifanya kazi na TFF, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.
Tutamkumbuka kama mtangazaji wa habari za mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. TFF tunatoa pole kwa familia za marehemu Amina Singo, ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu Amina Singo mahali pema peponi. Amina
SITA ZATINGA ROBO FAINALI UHAI CUP.
Timu sita zimeshakata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20) wa klabu za Ligi Kuu ya Tanzania.
Hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayofanyika viwanja vya Karume na Chamazi, Dar es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitai maji Uhai itafanyika Desemba 19 mwaka huu kwenye viwanja hivyo hivyo.
Timu zilizofuzu kutoka kundi A ni Coastal Union ya Tanga, Mtibwa Sugar ya Morogoro na JKT Ruvu ya Dar es Salaam. Kundi C ni Oljoro JKT ya Arusha na Ruvu Shooting ya Pwani wakati iliyofuzu kutoka kundi A hadi sasa ni Azam pekee.
Katika mechi zilizochezwa leo asubuhi (Desemba 17 mwaka huu) Coastal Union na Mtibwa Sugar zimetoka suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, wakati Uwanja wa Azam ulishuhudia African Lyon ikiifunga Mgambo Shooting mabao 2-1.
Nafasi mbili za robo fainali zilizobaki kutoka kundi B zinawaniwa na timu za Simba, African Lyon na Polisi Morogoro. Mechi itakayochezwa leo saa 10 jioni katika Uwanja wa Chamazi kati ya Polisi Morogoro na Simba ndiyo itakayoamua timu zitakazoungana na Azam kutoka kundi hilo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Tuesday, December 18, 2012
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ZIARANI MKOANI WA MARA
WAZIRI wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo, kesho ataanza ziara ya kikazi Mkoa wa Mara.
Kwa Mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ofisini kwake,Hii ni mara ya pili kufanya ziara Mkoano humo, kutokana na kwamba Waziri huyo amezaliwa Mkoa wa huo, katika Hospitali ya Serikali ya Musoma na amesoma Shule ya Msingi, Nanaxchand iliyokuwa ya Wahindi,ambapo walisoma watoto wenye vipaji na maarufu Musoma,sasa (Iringo)ni shule pia aliyosoma Mwl. Pearl Lucas Thomas Musiba,Binti pekee wa Mwasisi wa TANU na Mwenyekiti wa Halmashauri,NDUGU LUCAS THOMAS MUSIBA aliyetumikia Taifa kwa mihula miwili miaka 10 hadi kifo kilipomchukua, moja ya shule tano zilizoko katika kitovu cha mji wa Musoma.
Waziri Muhungo ana familia yake ambayo iko Mtaa wa Mwigobero ambapo kwa sasa kuna kivuko kipya cha Serikali ambapo kinafanya safari zake,kutoka Mjini Musoma na Wilaya ya Rorya.
Ziara yake ya kwanza, Waziri Muhongo ambaye hakutaka kuambatana na waaandishi wa habari
alitembea wachimbaji wadogo wadogo katika vijiji vya Seka na Suguti,Musoma vijijini, Wilaya ya BUTIAMA.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Waziri wa Nishati na Madini atekwenda Wilaya ya Serengeti na Musoma.
kwa sasa nguzo za Umeme tayari zimetandazwa katika vijiji vya Bwai Paris,ambako ndo nyumbani kwa wazazi wa Profesa huyo.
Baadhi ya wakazi wa Majita(Tarafa ya Nyanja),wamemtaka Waziri huyo asiishie hapo bali afanye utandazaji wa nguzo hizo maeneo ya vijiji vyote.
"Hatukatai kuwa nyumbani kwanza,lakini asambaze nguzo hizo na kuhakikisha Umeme unawaka Vijijini,hii itasaidia vijana wengi wanaokimbilia mijini kwa kufuata huduma hiyo hasa jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.
BARAZA LA WAGANGA WA TIBA ASILIA LIMEITAKA TFDA KUCHUNGUZA MAKAMPUNI ZA MADAWA(VIRUTUBISHO KUTOKA NJE YA NCHI.
BARAZA la Waganga wa Tiba Asilia (BAWATA) limeitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kudhibitisha madawa yanayoingizwa nchini na kuuzwa kwa gharama kubwa kama madawa na virutubisho.
Katibu wa Baraza hilo, Shariff Karama amesema leo asubuhi katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo Jijini Dar es Salaam,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Aliyasema hayo baada ya kuulizwa swali na Uhuru,kutokana na kuwepo msukumo hafifu wa tiba za asili kutoka nchini kwetu na badala yake kuingizwa virutubisho kutoka nje ya nchi na vyenye gharama za juu, huku vikiwepo dawa nzuri za asili kutoka Tanzania ambazo hazitumiwi na watanzania.
Alisema kuwa kumekuwa na msukumo hafifu wa utumiaji wa dawa za asili zinazotengenezwa nchini na ambazo tayari zimedhibitishwa na mkemia mkuu wa Serikali jambo ambalo wananchi wengi wamekuwa wakienda kununua virutubisho visivyo kuwa na tiba ndani yake.
Akizungumzia juu ya vibali vya waganga wa tiba asilia, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Shaka Shemuiwa alisema kuwa Serikali imekuwa ikisuasua kutoa vibali vya waganga wa tiba asilia ili waweze kusaidia watanzania wengi ambao hawana uwezo kumudu matibabu kwa gharama kubwa huku madawa ya magojwa sugu ya kisukari na Malaria yakiendelea kupoteza mamilioni ya watanzania.
Aliiomba Serikali na jamii kwa ujumla kutenganisha waganga wa jadi na waganga wa Tiba asilia jambo ambalo linawezekana kwao kukosa kibali baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupiga marufuku waganga baada ya kukithiri kwa mauaji ya vikogwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na Wizara ya afya kutilia msukumo kuhamasisha tiba asilia kwa mujibu wa sheria ya tiba asilia ya mwaka 2000.
Alitaka pia jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaokiuka sheria ya uvutaji sigara hadharani iliyopitishwa na bunge mwaka 1985 ambayo ina hadhari kubwa kwa asiyevuta kutoka na moshi wake kuwa na sumu aina ya Nicotyne ambayo inatengeneza sumu kali.
"uwenda hata askari hawajui hii sheria kwani utakuta mtu anavuta sigara hadharani mbele yake lakini cha kushangaza anamwacha,lakini moshi huo una madhara makubwa".Alisema Shemuiwa.
Aliongeza kuwa mabadiliko ya tabia nchi na hewa ya ukaa pia ni tatizo kubwa,hivyo amewataka wananchi kupanda miti ili kuboresha mazingira.
Tanzania imejaliwa kuwa na hazina kubwa ya miti mingi ya asili ikiwemo Alovera, Moringa Tree,Mwarobaini,mibomo kaburi na mengineyo ambayo ni tiba nzuri kwa binadamu.
Pia Tiba asilia ni tiba nzuri ambayo haina madhara makubwa kwa mtumiaji kuliko madawa mengine.
Baadhi ya watafiti nikiwemo na mimi ambaye huwa situmii vidonge kwa ajili ya tiba nimegundua kuwa dawa hizi ni nzuri na hazina madhara mwilini.
Serikali kupitia Wizara ya Afya utoe msukumo wa hali ya juu na uwekezaji wa tiba asili ambazo nchi kama China,zinatengeneza tiba asili kuwa vidonge na vinapoingia nchini vinauzwa kwa gharama kubwa kwa nini tusitengeneze wenyewe?
WAFANYAKAZI KOTE NCHINI KUFANYA MGOMO
SHIRIKISHO la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limesema kuwa endapo Serikali haitapandisha mishahara ya wafanyakazi kama ilivyopangwa wataamua vinginevyo na kwamba wanaitaka itangaze kima cha chini cha mshahara na marupurupu kwa sekta binafsi kabla ya April 2013.
Rais wa Shirikisho hilo, Omary Juma amewaambia waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam Asubuhi.
Alisema kuwa Kamati ya Utendaji ya Shirikiswho hilo, katika kikao chake cha Desemba 13-14 mwaka huu Mkoani Morogoro pamoja na mambo mengine kilijadili kwa kina, hali ya mazingira ya kazi nchini na kushuhudia kuwepo kwa mazingira magumu ya kazi na yalidumu kwa kipindi kirefu bila ya kupatiwa ufumbuzi.
Ameiomba Serikali katika bajeti yake ya mwaka 2013/2014 ilenge kuongeza kima cha chini cha mishahara kwa sekta ya Umma kwa asilimia 100,kupunguza kodi ya mapato ya ajira hadi kiwango kisichozidi asilimia 11,kwani ni hatua ya awali ya kuwezesha mfanyakazi kukabiliana na ongezeko kubwa la mfumko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.
"Kwa tarbani miaka saba iliyopita, Serikali imekuwa ikitoa ahadi ya kubotresha mashlahi ya wafanyakazi lakini hadi leo hii hali za maisha ya wafanyakzi walio wengi ni duni, huku wakishudua watanzania wenzao wachache wakizidi kuneemeka na kuwa na utajiri wa kupindukia"Alisema Juma.
Aliongeza kuwa hadi sasa wafanyakazi walio wengi wenye mishahara ya kati ya Sh.70,000-100,000 wanaishi kwa Sh.3,000-4000 kwa mwezi na ndio walio wengi hasa katika sekta binafsi,hali kadhalika katika sekta ya Umma ambapo mtumishi wa chini analipwa sh.5,700 kwa siku na sh.170,000 kabla ya makato huku kodi kubwa kwa mfanyakazi ikikatwa pia kuwepo kwa ongezeko la wageni wanofanya kazi nchini kinyume cha sheria.
Aidha ameitaka Serikali pia kupunguza kodi kwa wafanyakazi kutokana na makato wanayokatwa wafanyakazi ambapo wafanyakazi wanakatwa kodi kwa asilimia 46 huku wawekezaji na wafanyabishara wakubwa wakilipia wasatani wa asilimia 24 tu.
"Utakuta mfanyabiashara anauza bidhaa zake,kwa kufuatilia soko kuu na lenye faida liko wapi, na akijipenyeza kidogo anaweza asilipe kodi na akishakamatwa anasema amekosea analipa kodi huku akijua amepata faida kubwa, sasa mfanyakazi aliye kwenye pay Roll' hawezi kukwepa kodi au kulipa deni chini ya kiwango kwa kuwa hauwezi kukimbia"Alisema Juma.
Kamati hiyo pia iliangalia hali ya ukosefu wa ajira nchini na kubaini kuwa hali sio nzuri kutokana na ongezeko kubwa la shukle na vyuo a,balo haliendani na ongezeko la vyanzo vya ajira na kwamba vijana wengi wanakwepa sekta ya Kilimo ambayo ndio yenye uwezo mkubwa wa kubeba sehemu kubwa ya ajira lakini kutokana na miundo mbinu isiyoridhisha wengi wao hukimbilia mijini.
Alisema kuwa mahusiano baina ya shirikisho na Serikali yataendelezwa pale madai ya wafanyakazi yatakapotekelezwa kwa muda mwafaka na maboresho ya Pensheni yalenge kuhakikisha kuwa kikokotoo kizuri cha Pensheni kilichop hivi sasa 1.540 ndicho kitakachopotishwa kwa mifuko yote na kwamba wafanyakazi hawatakuwa tayari kuona kikokotoo kingine kikubwa zaidi ya hicho.
Monday, December 17, 2012
MBUNGE VICENT NYERERE ASEMA KAMPENI MENEJA ALIYEHAMIA CCM HAJAWAHI KUMFANYIA KAMPENI.
Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Mara,kimepata pigo mara baada ya kuondokewa na kamepni meneja wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Kiboko Nyerere mara baada ya kurejesha kadi na kurejea CCM.
Inadaiwa kuwa Kampeni Meneja wa Mh. Mbunge, Nyerere alikuwa Juma Songo,lakini Mh Vicent mwenyewe amemkana na kusema kuwa hajawahi kuwa Meneja Kampeni wake ila Chama kimefanya kile alichokiita hiyo ndo Siasa.
Hata hivyo katika ziara hiyo ya Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, alidiriki kuwafukuza waandishi wa habari wakati wa tadhimini ya uchaguzi iliyofanyika katika ofisi za CCM Mkoa huku akiwaacha waandishi wake wa habari ambao alikwenda nao kwenda ziara yake Mkoa wa Mara.
Kitendo cha Mwenyekiti huyo kuwafukuza kinadharirisha taaluma ya habari,hasa kwa waandishi walioko Mikoani kuonekana hawafai,huku wakifanya kazui kila siku.
Taasisi zinazohusika na haki kwa waandishi na vyombo vya habari iliangalie kwa kila,na maelekezo yatolewe kwa ajili ya hili.
Huu ni udhalilishaji mkubwa ambao Kiongozi wa Juu kama Mwenyekiti wa wazazi Taifa, Abdallah Majura Bulembo ambaye aliwahi kuwa Diwani katika Kata ya Nyasho kufanya udhalilishaji huu.
UCHUNGU WA MWANA AUJAE MZAZI HASA MWANAMKE
Usemi wa uchungu wa mwana aujuae mzazi unajitokeza hapa kwa mara nyingine hasa kwa mwanamke ambaye kila wakati amekuwa akiangaika huku na kule klutafuta riziki huku akiwa hana msaada wowote kutoka kwa mumewe.
hali hii inajitokeza kutokana na kwamba mwanamke anakuwa mwangaikaji wa kutafuta riziki tangu mwanae akiwa tumboni mpaka mwisho wa maisha yake (kifo), hii mpaka lini?
Kitendo cha Mama Bhoke Nyasenso, kunywa sumu baada ya kugundua wanae wamekufa kwa kukosa hewa wakati masikini Mama wa Watu akiangaika kuandaa chakula cha kesho kwa wanae wapendwa hao watatu MUNGU awapumzishe AMEN!
Mama Bhoke kwa uchungu wa kutunga Mimba Miezi tisa,kujifungua na kuhangaika kuwasomesha anaambulia sifuri kana kwamba ndo anaanza maisha.
Serikali naomba kwa roho ya huruma ingalie jambo hili na Mama huyo asichukuliwe hatua zozote kwani inatia huruma na inachanga akili sana,hata kama ingekuwa ni wewe najua ungefanya hivyo.
Aiha elimu juu ya mazingira na madhara ya Mkaa inapaswa kutolewa kaunzia shule za Msingi ili watoto waweze kujua madhara yake,laiti wangekuwa na Elimu hiyo,pia Kifo hicho cha kusitisha kisingewakuta kwani wangemweleza Mama yao ambaye hana Elimu yoyote kuhusu madhara ya Mkaa.
Hii ni mara ya pili tangu mwaka huu uanze kwa watoto kufia ndani kwa matukio m balimbali likwemo la moto ambao pia waliwasha mkaa na kuendelea kupika na wakaenda kulala, ili tukio lilikuwa maeneo ya Kamunyonge Mjini Musoma,ambapo si kijijini, hawa pia hawakuwa na elimu hii ya kwamba kuwasha mkaa na ukauacha ndani ya chumba unakosa hewa, ili ni somo la (Sayansi).
Watoto waliokufa ambao ni wanafunzi shule ya Msingi Nyangoto ni Naomi(14) wa darasa la VII,Magreth(10) wa darasa la IV, na Debora Nyasenso(6) wa darasa la I.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya,Justus Kamugisha alidhibitisha tukio hilo.
Tukio la kifo cha watoto hao lilitokea Jumamosi Alfajiri,Dec.15 katika kijiji cha Nyangoto, Nyamongo, tarafa ya Ingwe,Wilaya ya Tarime.
Wednesday, December 12, 2012
POLISI YAENDELEA NA UCHUNGUZI TPA
DAR ES SALAAM
POLISI inaendelea na uchunguzi wa watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutaka kutoa malori 22 kwa kukwepa ushuru wa mamilioni bandarini, huku ikiwasaka watuhumiwa wengine waliohusika katika mchakato huo.
Akizungumza na Uhuru,kamanda wa polisi wa Bandari, Fotnatus Muslimu alisema kuwa kuwa tuhuma wazaotuhumiwa watumishi hao ni za kughushi nyaraka linahitaji uchunguzi wa kina na watakapokamilisha jalada litapelekwa kwa DPP kwa ajili ya kupangiwa mashitaka.
Watumiwa hao ambao wapo nje kwa dhamana kwa upande wa TPA kitengo cha mapato, Mary-Stella Minja, Amir Mshegama, Kennedy Kessy na Gladyness Magerere na Andrew Masaga ambaye ni mfanyakazi wa TRA na Antipas Otieno, kutoka kampuni ya Multi Model.
Kamanda Muslimu alisema kwa sasa wanaendesha msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika mchakato huo wa kughushi nyaraka na upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya kutoa maamuzi.
Watumishi hao walitiwa mbaroni hivi karibuni wakituhumiwa kuhusika na mtandao wa kutoa malori 22 yaliyoingia nchini mwaka 2010 yaliyopaswa kulipiwa ushuru wa bandari wa sh. milioni 616 ambapo wao wanadaiwa kubadilisha nyaraka na kuonyesha maroli hayo yaliingia nchini mwaka 2012.
Kwa mujibu wa taarifa hizo wakati wakitoa mzigo huo ambao nimali ya Kampuni ya Dhandoo a mjini Mbeya, nyaraka zilibainika kuwa ni za kughushi na kuna ukwepaji wa sh.milioni 600, kwani badala ya kuonyesha sh.milioni 616 nyaraka zilionyesha sh. milioni 16.
Kutokana na hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Injinia Kipande Madeni alisema matukio ya wizi na uhujumu wa mapato ya serikali ni makubwa na yanasababishwa na wafanyakazi wasio waaminifu wa TPA, TRA na kampuni za upakuaji na upakiaji mizigo bandarini.
Akizungumzia tukio hilo, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, alisema bandari ya Dar es Salaam imekuwa na sifa mbaya ya wizi wa mizigo na hivyo kuchafua jina la Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki zinazotumia bandari hiyo, hivyo ni lazima isafishwe ili vitendo vya udokozi viwe historia.
Sunday, December 9, 2012
MIAKA 51 YA UHURU YAFANA NA HALAIKI YA AINA YAKE
MIAKA 51 YA UHURU.
DAR ES SALAAM.
RAIS Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza leo katika maadhimisho ya Miaka 51 ya Uhuru amevunja rekodi ya kuhutubia kwani hotuba hiyo huwa inafanyika baada ya miaka mitano,ametoa hotuba ya kutambulisha viongozi wenzake wa nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)na kusema asiye na macho aambiwi tazama,asiye an
masikio aambiwi asikie.Rais Kikwete ameamua kutoa hotuba hiyo kwa ajili ya kuwatambulisha wageni kwa lugha ya Kiswahili na kusema kwa lugha ya Kiingereza kuwa kama hawafahamu Kiswahili watafuraia kwa kusikia majina yao na watainuka kwa kuwapungia mkono watanzania.
“Leo tuna bahati kubwa kwa kuwa tuna viongozi wa Nchi za kusini mwa Afrika SADC,wageni 12 tu wamepata fursa ya kuja kuona maadhimisho haya ya Miaka 51 ya Uhuru na kwa kuwa ratiba ya ndege inawalazimu kuondoka inanipasa niwatambulishe kwenu na niwakaribishe.
Ametoa pongezi kwao kwani wameifanya sherehe ya Miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika kuwa njema kwake kutokana na kwamba hotuba hiyo ndiyo ya mwisho kwake kwani hatatoa hotuba tena,kwani hotuba hiyo anapaswa kutoa Rais mwingine wa 2015.
Alitoa fursa kwa Rais wa Namibia kutoa salamu zake kwani siku hii na yake kwani siku nchi yetu inapata Uhuru ndiyo siku alikuja Tanzania kutoka Namibia kuja kujipanga kuhusu ukurasa mpya wa kupata ukombozi wa Msumbiji ambapo Tanzania imetoa mchango mkubwa kwa nchi yake kupata Uhuru.
Marais waliokuwepo ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Armando Guebuza,Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila,Rais wa Namibia,Ifikepunye ,Waziri Mkuu wa Lesotho na wengine.
Alisema yeye ana uhusiano maalumu na Tanzania kwani wakati Nchi yetu inapata Uhuru 9 Disemba 1961,ndiyo siku aliyokua Tanzania na alikimbia makaburi huku Namibia na kuja hapa kujipanga kuanza vita ya Ukombozi nchini kwake na kuja Tanzania kujipanga kwa ajira ya kuikomboa
Rais wa Namibia alitoa pongezi kwa watanzania kwa maendeleo ambayo imeyapata na kusema kuwa wakati nchi yetu inapata Uhurundiyo siku alifika nchini hapa,na baada ya kuondoka Dar es Salaam alikwenda Mjini Dodoma ambapo alikuwa na Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere.
Sherehe hizo zilipambwa na gwaride la halaiki, ambapo mwaka huu lilikuwa la aina yake huku likifunua vitabu ,zoezi ambalo ni staili ya China,ngoma kutoka Ukerewe ambapo watoto wa Umri wa miaka mitatu walikoga nyoyo za Marais wa nchi nyingine na watanzania ,ngoma nyingine kutoka Dodoma,Zanzibar Msondo Ngoma na TMK.
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ya mwaka huu ni uwajibikaji,Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya maendeleo.
Pamoja na kupewa kadi za mialiko,viongozi wa vyama vya siasa,baadhi yao hawakuhudhuria sherehe hizo,akiwemo, Dk Wilbroad Slaa,Zitto Kabwe,Prof Ibrahimu Lipumba,waliokuwepo ni Mh.John Cheyo,Dk.Bhatt Mtamwega Mgaywa.
Uenda walituma wawakilishi.
Friday, December 7, 2012
ZIARA YA MKUU WA MKOA WA MTWARA.
KIJIJI CHA NANGURUKURU-KILWA MASOKO WALILIA ZAHANATI
KILWA MASOKO.
WAKAZI wa kijiji cha Nangurukuru,kata
ya Kisingino,Wilaya ya Kilwa wameiomba Serikali kukamilisha zahanati ya Kijiji
hicho ili waondokane na hadha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu.
Katibu wa Ujenzi wa Zahanati hiyo,Rashid Changa
alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwaka 2007, na mpaka sasa iko
katika hatua za mwisho za upigaji bati na
baada ya hapo Serikali inapaswa kukamilisha ujenzi huo.
Jiwe la Msingi la Zahanati hiyo liliwekwa na Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Rais Utawala Bora George Mkuchika ,Machi 25 2011 ambapo ilitolewa
ahadi ya kuchangia kukamilisha ujenzi huo kiasi cha Sh.Milioni 40,kutoka kwa
Daktari wa Wilaya,Mike Mabimbi kwa ajili ya kumalizia jengo hilo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nangurukuru,Shaibu Mmula
alisema kuwa zahanati hiyo kwa sasa imeanza kuweka nyufa kutoka na kukaa kwa
muda mrefu na hivyo inaweza kuigharimu
serikali pamoja na wananchi fedha nyingi za ujenzi mpya endapo itabomoka.
Alisema kuwa wananchi wamechangia nguvu zao kiasi cha Sh.
Milioni 34 na Halmashauri kupitia mfuko wa jimbo imechangia Sh Milioni 1.5 .
Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu idadi na ongezeko la wanachama ni
hafifu kutokana na changamoto zinazoikabili Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na zahanati,soko
na stend, huduma ya maji.
Aidha Katibu Mwenezi wa tawi la Nangurukuru,Said matale alisema
endapo changamoto hizo zitapata utatuzi,hakuna chama chochote kinaweza kushinda uchaguzi Mkuu 2015
na ametoa wito kwa Serikali kuangalia uwezekano wa kuchimbiwa malambo hasa
katika maeneo ya Kwakumtoni, Karasha, Dodomezi na Lingaula.
Aliongeza pia kuwa kumekuwa na unyanyasaji kwa upande wa
wavuvi kubaguliwa kiitikadi na kwamba kama wewe si mwanachama wa Chama cha CUF
uwezi kuvua samaki katika Bahari,hiyo
ambapo tatizo hilo linaonekana kuwa sugu kwa upange wa Kilwa Kivinje.
Thursday, December 6, 2012
KITABU CHA PICHA MAHAFALI YA KWANZA YA SHAHADA YA SANAA NA ELIMU(STEMMUCO)
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu wakisubiri kutunukia Shahada yao katika mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Mtakatifu AugustinoTawi la Mtwara (STEMMUCO), |
Mgeni rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki,Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira,Milton Makongoro Mahanga akiwa na Mkuu wa Chuo
cha Stella Maris Mtwara (STEMMUCO),Mhashamu Baba Askofu Mkuu,Norbet
Mtega,akishiriki maandamano ya wanataaluma kuelekea viwanja vya Chuo kwa
ajili ya kuwatunuku Shahada wahitimu.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki,Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Milton Makongoro Mahanga akiwa na Mkuu wa Chuo cha Stella Maris Mtwara (STEMMUCO),Mhashamu Baba Askofu Mkuu,Norbet Mtega, mara baada ya maandamano kabla ya kuwatunuku Shahada ya kwanza wahitimu wa Shahada ya Sanaa na Elimu,katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustion Tawi la Mtwara juzi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia sherehe hiyo ambayo kwa wao haikuwa vyema kwani hawakuwa na maandalizi yoyote ya viti kwa ajili ya kuandika habari wakiwa wamekaa kwenye viti, waandishi wa print Media wanapaswa kuwa wanaandaliwa sehemu yao ya kukaa kuliko kuwatelekeza, huku hotuba zao zikijaa shukrani nyingi kwao, bila ya kuwajali, ni muda mwafaka sasa, taasisi zote zianze kuwajali wanataaluma hao ambao ni kiungo muhimu si kwa Serikali tu bali hata mashirika kama ya dini n.k.
MKUU WA CHUO akifurahi jambo na Mgeni rasmi,anaonekana kusema sherehe imekwenda MZUKA ETI EH!!!
Mgeni rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki,cha Mtakatifu Agustino,Stella Maris Mtwara( (STEMMUCO) Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Milton Makongoro Mahanga. akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu,Wini Musiba,mara baada ya kutunukiwa.
MAHAFALI YA KWANZA MTWARA (STEMMUCO)
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga akiteta jambo na Mhashamu Baba Askofu MKUU wa Chuo Kikuu cha Stella Maris( STEMMUCO) Norbet Mtega, mara baada ya kumaliza hotuba yake katika mahafali ya kwanza ya Chuo hicho.
MWENYEKITI wa Bodi ya Chuo
Kikuu kishiriki cha Stella Maris,Tawi
la Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (STEMMUCO),Mhashamu, Gabriel Mmole
ameipongeza Serikali kupitia bodi ya mikopo
kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Chuo hicho.
Aliyasema hayo juzi
katika mahafali ya kwanza ya Chuo hicho ya kuhitimu Shahada ya kwanza ya
Sanaa/ualimu (Bachelor of Art with Education) wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mahafali hayo yaliyofanyika
katika viwanja wa Chuo Mjini Mtwara.
Alisema anaishukuru Serikali kwani bila wao pasingekuwepo na
mafanikio yoyote ya Chuo kwani ukubaliwa wao wa kutoa mikopo kwa Chuo hicho
ndio umesababisha mafanikio katika kufanikisha wanachuo kumaliza masomo yao vyema.
“Natoa pongezi za dhati kwa serikali ya awamu ya nne ambayo
imetuwezesha kutoa mikopo kwa wanafunzi wetu bila kubagua itikadi za dini
ukizingatia kuwa sisi ni taasisi ya dini,bila wao tusingefanikiwa”. Alisema
Mhashamu Baba Askofu Mmole.
Akifungua Mahafali hayo ya kwanza ambayo yalianza kwa
maandamano, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga alisema ukosefu wa ajira kwa vijana walio wengi
unatokana na baadhi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu kutotaka ama kutoweza kuchukua
masomo ya Sayansi na hisabati, pia fani ya ualimu ambazo zina fursa ya ajira.
Alisema kuwa tatizo la wahitimu wa Vyuo Vikuu kurudisha
mikopo waliokopeshwa bado ni kubwa, ambapo kufikia Juni 2012, madeni ya
wahitimu wa Vyuo Vikuu yakiyokuwa yameiva yalikuwa Bilioni 160.7 na kati yake,
Sh Bilioni 39.5 zilitakiwa ziwe zimeishakusanywa kutoka kwa waliokopa lakini
asilimia 49 tu kati ya hizo zilikuwa zimekusanywa na bodi ya mikopo ya wanafunzi.
Aidha ametoa wito kwa Vyuo vya elimu ya juu kurekebisha
kasoro zilizopo kwa kutilia maanani masomo ya Hisabati na Sayansi na
kuhakikisha kila fani au program katika vyuo vikuu vyote kunakuwepo na masomo
ya ujasilimali (Bachelor of Business Administration/Management in Entrepreneurship)
ili kuwaandaa wahitimu kujiajiri kama hawatapata kazi za
kuajiriwa.
Alitoa wito kwa wahitimu kuwa tayari kufanya kazi popote
bila kubagua maeneo kama kama wengi wao wanavyopenda Mijini.
Katika awamu ya nne ya Serikali kutoka mwaka 2005/2006-2011/2012,
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo Iliyoundwa mwaka 2005, ilikopesha wanafunzi
480,472 jumla ya Sh. Trioni 1,133,386,869,000
ambapo Chuo hicho kimefaidika n amikopo hiyo ambapo asilimia 94 ya wahitimu,pia
imetoa ekari 140 kwa ajili ya mendeleo ya Chuo hicho,ambapo jumla ya wahitimu (kifungua
mimba) wapatao 1,100 wamehitimu.
Naye Mhitimu katika Chuo hicho, Wini Israel Musiba aliishukuru
Serikali kwa kutoa mikopo hiyo na kwamba
inajali familia duni si kama awali
ambapo jamii ilidhani mikopo ni kwa
watoto wa wakubwa peke yao,pia alitoa wito kwa Serikali kuweka miundo
mbinu ya barabara na Umeme ili walimu wafanya kazi zao kwa umakini zaidi kwa kuzingatia masomo ya sayansi yanayohitaji
maabara zenye Umeme hasa vijijini.
Subscribe to:
Posts (Atom)