Saturday, March 2, 2013

HATIHATI YA KIFO CHA CHADEMA YAINGIA TARIME-MUSOMA

TARIME NA MUSOMA.

BAADHI ya wanachama wa  Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA wamefunga ofisi ya Wilaya iliyoko Mjini Tarime Mkoa wa Mara kwa mabanzi  yaliyopigwa kwa misumari kwa muda wa siku tatu.

 

Wanachama wa Chama  cha Demokrasia  na Maendeleo Chadema Wilayani Tarime wamesikitishwa  kwa kitendo cha  Ofisi ya Chama Wilaya   kufungwa  kwa muda wa siku 3 hadi sasa ambapo mpaka jana mbanzi hayo yalitolewa na kuacha kufuri pekee ambapo baadhi yao walitaka kusikiana mapanga lakini hawakufanya hivyo.


Wanachama walisema kuwa kitendo cha kufungwa ofisi ya chama Wilaya kimewafanya wao wasipate huduma za kichama  na kwamba kitendo hicho cha kufunga ofisi kitarudisha nyuma chama kutokana na viongozi kutokuwa kioo kwa wanachama wake.

Mjumbe mmoja  wa chama hicho mkazi wa Nyamisangura ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa  sababu ya kufungwa kwa ofisi imekuja baada ya Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Lucas Ngoto kusimamishwa  uongozi na kamati Tendaji jambo ambalo  alikuafikiwa na baadhi ya wananchama na kuibua mgogoro mkubwa ambao umewafanya baadhi yao kugawanyika makundi.

Mjumbe huyo aliongeza kuwa  kwa sasa kunampasuko mkubwa ndani ya chama cha Chadema ambapo tayari kuna makundi mawili yanayodaiwa kuwa kundi moja ni la Mwenyekiti wa Vijana Taifa John Heche  na kundi la George Waitara ambao wanadaiwa   kuwa wapo mbioni na wanajipanga kugombea Ubunge uchaguzi 2015 kutoka ndani ya chama hicho.

“Sababu ya kufungwa kwa ofisi ni baada ya  Kaimu Mwenyekiti wa chama Wilaya  Lucas Ngoto kusimamishwa uongozi ambapo sababu hatuzijui na ieleweke kuwa ndani ya chama kuna makundi mawili haya makundi hayaelewani kati ya kundi la Heche na Waitara sasa huyu Kaimu  yeye yuko kundi la Waitara  kundi la Heche halimtaki jambo ambalo lilisababisha watu wa kundi la  La Waitara  kufunga Ofisi kwa mabanzi na kugonga misumari,kama tunataka kunusuru chama  hawa watu wasipewe nafasi za kugombea Ubunge watauwa chama yote haya ni kwa sababu ya kujitengenezea mazingira mazuri ya uchaguzi ujao”alisema Mjumbe mmoja.

Dominic Manyama Mkazi wa Mtaa wa Starehe alisema kuwa makundi yanayoendelea ndani ya chama  ni dalili ya Chama hicho kushindwa uchaguzi wa mwaka 2015  kwa madai kuwa Chama hicho kimekuwa kikiaminiwa na wananchi walio wengi na kuendelea kuwepo kwa makundi kutawafanya watu kutokuwa na imani ya Chama hicho.

Wanachama  wamewataka viongozi wa Kitaifa kufika Tarime kutatuwa mgogoro ili kukinusuru chama na kwamba vinginevyo baadhi ya wanachama watakihama chama hicho kwa kuwa kina mgogoro mkubwa wa kimadaraka na kuwa kufunga ofisi  inaleta picha mbaya kwa wanachama na watu wengine.

Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, Lucas Ngoto  alipohojiwa nini sababu ya yeye kusimamishwa uongozi na kuwepo kwa  makundi ndani ya chama na wakati uchaguzi ukingali bado alisema kwa sasa hawezi kuongea chochote na kuahidi kutoa taarifa baada ya siku tatu.

Katibu Mwenezi wa chama cha Chadema Wilaya Marwa Maruri  alisema kuwa  leo wanatarajia kukaa kikao cha Chama na kwamba taarifa kamili ataitoa  kesho juu ya maamuzi yatakayo kuwa yamepatikana kutokana na kikao  hicho.

Inasemekana kuwa,Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe anatarajiwa kufika siku yoyote kusuluhisha mgogoro huo huku ofisi kwa sasa ikiwa imefugwa kwa kufuri  na kungo'oa mabanzi yaliyokuwa yamepigiliwa na misumari.

Mjini Musoma Meya wa Manispaa hiyo,Alex kisurura alinusurika kung'olewa na madiwani wenzake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ubadhilifu wa fedha. 

MBEGU YA MAHINDI KUTOKA KENYA INA UGONJWA

TARIME.


Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara  imetoa tahadhari kwa
wananchi wa Kata ya Nyamwaga kutokana na mbegu mbaya  ya mahindi yenye
ugonjwa wa michirizi ya Mahindi yanapofikia kiwango cha kukomaa
iliyosambazwa kutoka Kenya na wakulima kuinunua kutokana na kuuzwa kwa
bei nafuu  kutoitumia.





Diwani wa Kata ya Nyamwaga ,Joseph Nyagala alitoa taarifa kutoka katani
kwake juu ya ugonjwa uliopo wa mahindi kupata michirizi.


“ugonjwa huo unakuwa hivi unapanda mahindi vizuri yakifikia hatua ya
kubeba muhindi  ganda la juu linakauka kana kwamba mahindi yamekomaa
ukivuna unakutana na aidha gunzi ama michirizi iliyopo kwenye mahindi
ambayo hayana chochote,hii ni hatari sana,mbegu za mahindi hayo yanauzwa
Sh.5000,ambapo mbegu bora ya SIDICO ni Sh. 9,000.Alisema Nyagala.



Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa alisema ugonjwa huo kwa sasa umefika Wilaya ya Bunda,ametoa tahadhari wananchi kutonunua mbegu hiyo,ambapo ameagiza wakulima kuyachoma,njaa kali itaukumba Mkoa huu.


WAJUMBE WA CCM WAJA JUU.

MUSOMA





WAJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapindunzi Mkoa wa Mara wamekuwa mbogo kwa watendaji wa Serikali kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapindunzi (CCM)  ya Mwaka 2010 kwa upande wa Maji, Umeme na Barabara.



Akitoa hoja katika kikao hicho Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo alisema kuwa tatizo la maji katika Wilaya hiyo limekuwa   likiwakabili wanachi wa Wilaya hiyo, ukizingatia kwamba wamechangia fedha nyingi ambapo alisema wanachi wake wamechangia jumla ya Sh Milioni 66 kwa ajili ya uchimbaji wa visima ambapo vyote havitoi maji.


Wakizungumza kwa nyakato tofauti wajumbe hao kutoka Wilaya za Tarime,Bunda,Musoma, Butiama Rorya na Serengeti walilalamikia pia kuwepo kwa matatizo hayo ambayo ndiyo haswa yanayowakibili wananchi likiwemo la  kukatika katika kwa umeme na baadhi ya sehemu kutokuwa na umeme wa kutosha pia ubovu wa barabara.


Akizungumzia juu ya ujenzi wa barabara ya Musoma-Majita-Busekela ambayo ilikuwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete wakati akiomba ridhaa kurudi madarakani,Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Butiama Yohana Mirumbe aliuliza swala hilo kuwa ujenzi huo utaanza lini.


Akijibu hoja hiyo,Meneja wa Tanroad Mkoa wa Mara, Emmanuel Koroso alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha barabara hiyo inaanza kujengwa ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani  ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010.


“Ndugu wajumbe sisi Tanroad tunatekeleza sana Ilani ya CCM,tunawahakiksihia kuwa barabara zote zilizosemwa kwa mujibu wa Ilani zitatengenezwa”.Alisema Koroso, huku akishangiliwa na wajumbe.



Msimamizi wa Ubora wa Maji Mkoa wa Mara, Mathayo  Athuman akitoa ushauri kuwa ni vyema mikataba yote iseme wazi kuwa mchimbaji (Mkandarasi) atalipwa baada ya kuwachimbia wananchi kisima chenye maji ya kutosha na atakayechimba afanye kazi zote ikiwemo ya kutafuta maji ,kuchimba kisima na kujenga miundombinu ya maji ingawa gharama yake ni kubwa lakini bora kuwa na visima vichache vyenye maji kuliko kulipia gharama za uchimbaji hata pale ambapo maji hayakupatikana.

UJIO WA MAKAMU WA RAIS, UWANJA WA NDEGE WASAFISHWA.

MUSOMA.

 UWANJA Ndege wa Musoma,wafanyiwa usafi leo asubuhi hadi mchana kwa ajili ya maandalizi ya maandalizi ya ujio wa Makamu wa Rais, Dk.Mohammed Gharibu Bilal,anayetarajiwa kuwasili kesho Mjini hapa kuzindua rasmi usafiri wa feri itokayo Musoma kwenda Wilaya ya Rorya, kivuko hicho kina utata wa jina aidah kiitwe Mv. Musoma ana Kinesi ama Rorya.

Makamu pia atazindua barabara ya Sirari.

Awali uwanja huo ulikuwa kichaka, lakini kwa sasa una mwonekano mzuri,ambapo hata hivyo kampuni ya ndege ya Auric Air inafanya safari zake, mara nne kwa wiki kutoka Musoma-Mwanza-Musoma kwa nauli ya Sh.70,000,ikiunganisha na ndege zingine kutoka Mwanza kwenda bongo, Dar es Salaam.

Saturday, February 23, 2013

MPASUKO CHADEMA TARIME.




 TARIME.


VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)  Wilayani
Tarime  wameshindwa kuafikiana  katika kikao cha kamati tendaji
kilichofanyika juzi kupata mwafaka uliosababisha kufugwa kwa ofisi.

Wanamtaka Mwenyekiti  wa Chama Taifa Freeman Mbowe kuwashuruhisha. 
 
Mjumbe mmoja alisema kuwa kwa sasa kunampasuko mkubwa ndani ya chama
cha Chadema ambapo tayari kuna makundi mawili yanayodaiwa kuwa kundi
moja ni la Mwenyekiti wa Vijana Taifa John Heche  na kundi la George
Waitara ambao wanadaiwa   kuwa wapo mbioni na kwamba wanajipanga kugombea 2015
 
Katibu Mwenezi wa Chama cha Chadema Wilaya Marwa Maruri  alikiri kwa
baadhi ya viongozi  kuondoka  wakati kikao kinaendelea.
 
Baadhi ya wanachama  Mjini Tarime walisema kuwa  sababu ya kufungwa
kwa ofisi kwa muda wa siku 3 imekuja baada ya Kaimu Mwenyekiti wa
Chadema Wilaya Lucas Ngoto kusimamishwa  uongozi na kamati Tendaji
jambo ambalo  alikuafikiwa na baadhi ya wananchama na kuibua mgogoro
mkubwa ambao umewafanya baadhi yao kugawanyika makundi.



Wednesday, February 13, 2013

MBWAMWITU HAWATATOWEKA TENA-SERENGETI




SERENGETI

Mkurugenzi  wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI) Dk.Simon Mduma amesema kuwa tishio la kutoweka Mbwa Mwitu katika hifadhi ya Serengeti kutokana na magonjwa mbalimbali ya mbwa litatoweka kwani tayari wamepata chanjo ili kuweza kumaliza magonjwa yanayosababisha kutoweka kwa Mbwa Mwitu.


Mbwa hao waliochukuliwa eneo la Loliondo wamefugwa katika Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa miezi mitatu hili likiwa ni kundi la pili lenye mbwamwitu 15 ambapo kundi la kwanza lilitolewa Agosti 30 mwaka huu likiwa na mbwamwitu 11 waliachiwa ndani ya hifadhi hiyo mwaka 1980 na kulikuwepo   Mbwa Mwitu wapatao 500.

Aidha Mbwamwitu wapatao 15 ambao walikuwa wamefugwa katika eneo la Nyamuma ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya juhudi za kuwarudisha wanyama hao ambao walitopotea miaka ya 1990 wanaendelea vizuri.


 Kukosekana kwa wanyama hao ndani ya hifadhi hiyo kumesababisha kukosekana kwa kivutio kingine muhimu ambapo watalii wanahitaji kuwaona.

Alitoa pongezi kwa  mashirika mbalimbal ikiwemo ofisi ya Rais,ambayo ilichangia Sh. M.30 kwa ajili ya mradi  wa mbwa mwitu kwani  imesaidia kuongeza kivutio muhimu.



Alisema kuwa kuna changamoto ambazo wanakabiliana nazo ikiwa ni pamoja mashirika mengi kutofadhili mradi huo ambapo kwa sasa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom ndio pekee iliyotoa ufadhili wa zaidi ya milioni 450.

Kutokana na kuruhusiwa kwa mbwamwitu hao sasa imeongezeka na kufanya idadi ya wanyama hao kufikia 26 ndani ya TANAPA ambapo Agosti 30 mwaka huu waliachiwa 11.


Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete aliagiza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kuhakikisha Mbwamwitu waliofunguliwa  katika mbuga ya Serengeti wanakuwa salama muda wote ili wasitoweke tena.


Sunday, February 3, 2013

CCM MWANZA WAHADHIMISHA KWA MICHEZO



MWANZA

CHAMA cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza kimefanya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya michezo mbalimbali ikiwemo ya mbio  za baiskeli yaliyosisimua wakazi wa Jiji la Mwanza.

Mbio hizo zilizoanzia katika ofisi za CCM Makao Makuu kuelekea Barabara ya kenyata-Usagara zilianza majira ya mbili asuhuhi na kuleta hamasha kubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Nyamagana ambao kwa pamoja walikuwa wakiwashingilia huku wakisidikizwa na gari la Katibu wa CCM Wilaya hiyo likiwa na bendera kubwa ya Chama.

Mshindi wa kwanza katika mbio hizo alikuwa Gegedi Maduhu  (25) mwenye namba 850, Mfanyabiashara ya bodaboda ya baiskeli na Mzaliwa wa kijiji cha Mwamoto-Ngokolo Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza mbio hiyo na kuwaacha wenzake kwa takribani dakika 10 na kumaliza mbio hiyo 10:40 katika Uwanja wa Kumbukumbu wa  Nyamagana.

Mshindi wa Pili alikuwa Paulo Mathias ( 19)  mwenye namba  831 Mkazi wa Shamaliwa kata ya Igoma Mwanza ambaye ni Mkulima wa mpunga aliyemaliza mbio hiyo 10:44 na Mshindi wa tatu alikuwa Kulwa Kalamo (20) mwenye namba 834 aliyemaliza kwa muda wa 10:46 na alipewa kombe na fedha taslimu Sh.300,000.

 Aidha akizungumza na  Uhuru, mara baada ya kukamilika kwa mbio hizo, Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Nyamagana,Raphael Shillatu alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kuhamasisha wananchi.


 “Mchezo huu ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia michezo ili kuleta hamasha kwa vijana kwani  michezo ni ajira, pia huleta Mshikamano, Umoja, Upendo, Utulivu na Amani na kukiwezesha chama kuwa na timu itakayofanya kazi pamoja na kuhakikisha ushindi kuanzia chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2015”Alisema Shillatu.

Aliongeza kuwa mkakati huo ni ahadi yake wakati akiwa  anagombea Kiti hicho kuwa atahakikisha anaimarisha michezo yote ifikapo maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama ikiwa ni pamoja na riadha ya Baiskeli, mpura wa Miguu kwa wanaume ,bao,na baadae kuanzisha michezo mbalimbali kwa wanawake ambao nduyo wenye hamasha kubwa  hadi ukomo wa Uongozi wake ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani kwa vitendo.

Aidha washindi hao walipewa vitita vya fedha zilizokuwa zimefugwa kwenye bahasha ambapo hata hivyo hazikutangazwa  kwa ajili ya usalama wao na kupewa bendera za CCM na mlingoti wake kupeperusha bendera hizo maeneo ya makazi yao.