TARIME NA MUSOMA.
BAADHI
ya wanachama wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA wamefunga
ofisi ya Wilaya iliyoko Mjini Tarime Mkoa wa Mara kwa mabanzi
yaliyopigwa kwa misumari kwa muda wa siku tatu.
Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani
Tarime wamesikitishwa kwa kitendo
cha Ofisi ya Chama Wilaya kufungwa kwa
muda wa siku 3 hadi sasa ambapo mpaka jana mbanzi hayo yalitolewa na
kuacha kufuri pekee ambapo baadhi yao walitaka kusikiana mapanga lakini
hawakufanya hivyo.
Wanachama
walisema kuwa kitendo cha kufungwa ofisi ya chama Wilaya kimewafanya wao
wasipate huduma za kichama na kwamba
kitendo hicho cha kufunga ofisi kitarudisha nyuma chama kutokana na viongozi
kutokuwa kioo kwa wanachama wake.
Mjumbe
mmoja wa chama hicho mkazi wa
Nyamisangura ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kuwa sababu ya kufungwa kwa ofisi imekuja baada ya
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Lucas Ngoto kusimamishwa uongozi na kamati Tendaji jambo ambalo alikuafikiwa na baadhi ya wananchama na
kuibua mgogoro mkubwa ambao umewafanya baadhi yao kugawanyika makundi.
Mjumbe huyo
aliongeza kuwa kwa sasa kunampasuko
mkubwa ndani ya chama cha Chadema ambapo tayari kuna makundi mawili yanayodaiwa
kuwa kundi moja ni la Mwenyekiti wa Vijana Taifa John Heche na kundi la George Waitara ambao wanadaiwa kuwa wapo mbioni na wanajipanga kugombea
Ubunge uchaguzi 2015 kutoka ndani ya chama hicho.
“Sababu ya
kufungwa kwa ofisi ni baada ya Kaimu
Mwenyekiti wa chama Wilaya Lucas Ngoto
kusimamishwa uongozi ambapo sababu hatuzijui na ieleweke kuwa ndani ya chama
kuna makundi mawili haya makundi hayaelewani kati ya kundi la Heche na Waitara
sasa huyu Kaimu yeye yuko kundi la
Waitara kundi la Heche halimtaki jambo ambalo
lilisababisha watu wa kundi la La
Waitara kufunga Ofisi kwa mabanzi na kugonga misumari,kama tunataka
kunusuru chama hawa watu wasipewe
nafasi za kugombea Ubunge watauwa chama yote haya ni kwa sababu ya kujitengenezea
mazingira mazuri ya uchaguzi ujao”alisema Mjumbe mmoja.
Dominic
Manyama Mkazi wa Mtaa wa Starehe alisema kuwa makundi yanayoendelea ndani ya
chama ni dalili ya Chama hicho kushindwa
uchaguzi wa mwaka 2015 kwa madai kuwa Chama hicho
kimekuwa kikiaminiwa na wananchi walio wengi na kuendelea kuwepo kwa makundi
kutawafanya watu kutokuwa na imani ya Chama hicho.
Wanachama wamewataka viongozi wa Kitaifa kufika Tarime
kutatuwa mgogoro ili kukinusuru chama na kwamba vinginevyo baadhi ya wanachama watakihama
chama hicho kwa kuwa kina mgogoro mkubwa wa kimadaraka na kuwa kufunga
ofisi inaleta picha mbaya kwa wanachama
na watu wengine.
Kaimu
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, Lucas Ngoto
alipohojiwa nini sababu ya yeye kusimamishwa uongozi na kuwepo kwa makundi ndani ya chama na wakati uchaguzi
ukingali bado alisema kwa sasa hawezi kuongea chochote na kuahidi kutoa taarifa
baada ya siku tatu.
Katibu
Mwenezi wa chama cha Chadema Wilaya Marwa Maruri alisema kuwa
leo wanatarajia kukaa kikao cha Chama na kwamba taarifa kamili
ataitoa kesho juu ya maamuzi yatakayo kuwa yamepatikana kutokana na
kikao hicho.
Inasemekana
kuwa,Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe anatarajiwa kufika siku
yoyote kusuluhisha mgogoro huo huku ofisi kwa sasa ikiwa imefugwa kwa
kufuri na kungo'oa mabanzi yaliyokuwa yamepigiliwa na misumari.
Mjini
Musoma Meya wa Manispaa hiyo,Alex kisurura alinusurika kung'olewa na
madiwani wenzake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ubadhilifu wa fedha.
No comments:
Post a Comment