MUSOMA.
WAZIRI wa Ujenzi Barabara na Viwanja vya Ndege,Dk.John
Magufuli amekipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa kutekeleza
Ilani ya CCM.
Aliyasema hayo jana wakati akimkaribisha Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib
Bilal wakati wa kuzindua ukarabati wa barabara ya Nyanguge-Musoma inayopakana na mpaka wa
Mikoa ya Simiyu na Mara,sherehe zilizofanyika katika kijiji cha Mmazami, Wilaya
ya Butiama.
Alisema kuwa ushiriki wa Meya wa Manispaa ya Musoma (CHADEMA),
Alex Kisurura unaonyesha dhahiri kuwa
anatekeza vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi, na kusimamia vyema ujenzi wa
barabara za Manispaa kwa fedha ambayo ni ya Serikali inayoongozwa na CCM.
“Serikali hii inaongozwa na Chama cha Mapinduzi,haina
ubaguzi wowote,kwani imetoa fedha jumla
y a sh. Milioni 496 za ujenzi wa barabara zake na kati ya hizo tayari wamepewa sh. Milioni 341 inaonyesha
Meya huyu, Alex Kisurura ana mwili wa
CHADEMA lakini moyo ni wa CCM
tumpongeza”alisema magufuli huku akishangiliwa na wananchi.
Aliongeza kuwa “Tunawajengea barabara,km 2 kwa
watembea kwa miguu na pikipiki upande wa kulia na kushoto,kama wanataka
kuandamana waandamane sana ila waachie nafasi za magari kupita huku wakijua
kuwa barabara hiyo imejengwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi”alisema
Magufuli.
Alisema katika kuhakikisha mtandao wa barabara za
lami zinajengwa na kwamba fedha nyingi zimetolewa
katika Wilaya za Mkoa wa Mara, ambapo alitoa pongezi kwa Serikali
ya awamu ya nne kwa jitihada zake katika kuhakikisha Mkoa wa Mara
unapata maendeleo.
Wilaya zilizotengewa
fedha ni pamoja na Serengeti Sh.
Milioni 57.6, Musoma Milioni 496,Bunda Sh. Milioni 975,Butiama Sh. Milioni
334,halmashauri ya Wilaya ya Musoma Sh. Milioni 519 ,Wilaya ya Rorya Sh.
Milioni 977 na Wilaya ya Tarime Sh. Milioni 854.
Aidha amelitaka Shirika la Umeme Tanesco kutoa kibanda
chake ili kupisha upanuzi wa barabara ambapo hawatalipwa fidia yoyote.
Makamu wa Rais yuko ziarani Mkoa wa Mara,ambapo leo
atafanya uzinduzi kivuko cha Mv.Musoma kinachofanya safari zake kutoka Musoma
kwenda Kinesi Wilaya ya Rorya ambacho pia nia hadi za Rais Jakaya Kikwete
kuleta kivuko kipya ili kupunguza hadha kwa wananchi.
Pia amekutana na viongozi wa Kamati ya Siasa ya Mkoa
wa Mara katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa.
No comments:
Post a Comment