Mkuu wa Wilaya ya
Butiama,Angeline Mabula amesema kuwa hali
ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya hiyo imeimarika tofauti na hapo awali ambapo
ilikubwa na matukio ya mauaji ya kutisha.
Alikuwa akizungumza na Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Radio, Magazeti na Luninga juu ya mafaniko ya awamu ya nne katika
Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2005-2012
“Kwa siku za hivi karibuni, Wilaya ilikumbwa na wimbi
la mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina, Serikali imechukua kila
tahadhari kuhakikisha kwamba mauaji hayatokei tena,elimu imeendelea kutolewa,
ili kuhimiza ulinzi shirikishi ambao utakuwa suluhisho la tatizo la mauaji”Alisema
Mabula.
Alisema kuwa historia inaonyesha kwamba, mbali na
mauaji yatokanayo na ugomvi wa koo, wizi wa mifugo na ugomvi/migogoro ya ardhi
mauaji ya sasa ya kuchinja watu hayakuwahi kutokea, yameibuka tu kwa
udanganyifu wa watu kutaka kujipatia
utajiri wa haraka haraka.
Serikali inafanya kila linalowezekana kuchukua hatua
za kisheria dhidi ya wahalifu wa aina zote, kwa kuwafichua na kuwafikisha mbele
ya vyombo vya dola ili kulinda raia wake na mali zao.
Aidha Wilaya ina vituo 10 vya polisi Buhemba, Bisumwa,
Bukima, Suguti, Kiagata, Kyabakari, Kigera etuma, Butiama, Saragana na Tegeruka.
Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua
katika kuwahimiza na kuwaelewesha wananchi kuwa ulinzi wao na mali zao uko
mikononi mwa wananchi wenyewe wakishirikiana na Polisi, dhana ya Polisi jamii
na ulinzi shirikishi inaendelea kuhimizwa.
Wilaya imeweka mpango madhubuti wa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa vijana au
wanamgambo waliokwishapitia mafunzo ili kuimarisha ulinzi na Usalama katika
maeneo yao na kuwatahadharisha kutojichukulia sheria mikononi.
Amewataka vijana na akinamama kuunda vikundi ili
wapewe vitendea kazi ambavyo vitawasaidia katika kazi zao za ujasiliamali na
kwamba jumla ya Sh. Milioni 90 zimetegwa kwa aili ya kuwawezesha vijana na akina
mama ,ambapo kati ya hizo Milioni 45 ni za Vijana na Milioni 45 ni za vikundi
vya akina mama ambapo watapewa vitendea kazi watakapokuwa wamejisajili.
Aidha
vikundi 4 vya wajasiliamali vilipewa mikopo yenye thamani ya Sh. 180,000,000 kutoka mfuko wa
wajasiliamali unaofadhiliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vikundi
vilivyopewa fedha ni Mwangaza SACCOS Buhemba Tshs. 80,000,000, Imani Bwai (Kiriba) Shs. 31,000,000 na Mwamucha SACCOS (Mugango) Tshs. 30,000,000
|
|
Katika kipindi cha miezi sita halmashauri imeweza
kusimamia vizuri fedha zilizopatikana katika vyanzo mbalimbali kwa ajili ya
kugharamia matumizi ya mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya
maendeleo. Pia Ruzuku ya Serikali imeongezeka kutoka Sh.571,556,000 mwaka 2005 hadi Sh.975,426,302 mwaka 2012
sawa na 59%.
No comments:
Post a Comment