Saturday, March 2, 2013

WAJUMBE WA CCM WAJA JUU.

MUSOMA





WAJUMBE wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapindunzi Mkoa wa Mara wamekuwa mbogo kwa watendaji wa Serikali kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapindunzi (CCM)  ya Mwaka 2010 kwa upande wa Maji, Umeme na Barabara.



Akitoa hoja katika kikao hicho Mbunge wa Jimbo la Rorya, Lameck Airo alisema kuwa tatizo la maji katika Wilaya hiyo limekuwa   likiwakabili wanachi wa Wilaya hiyo, ukizingatia kwamba wamechangia fedha nyingi ambapo alisema wanachi wake wamechangia jumla ya Sh Milioni 66 kwa ajili ya uchimbaji wa visima ambapo vyote havitoi maji.


Wakizungumza kwa nyakato tofauti wajumbe hao kutoka Wilaya za Tarime,Bunda,Musoma, Butiama Rorya na Serengeti walilalamikia pia kuwepo kwa matatizo hayo ambayo ndiyo haswa yanayowakibili wananchi likiwemo la  kukatika katika kwa umeme na baadhi ya sehemu kutokuwa na umeme wa kutosha pia ubovu wa barabara.


Akizungumzia juu ya ujenzi wa barabara ya Musoma-Majita-Busekela ambayo ilikuwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete wakati akiomba ridhaa kurudi madarakani,Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Butiama Yohana Mirumbe aliuliza swala hilo kuwa ujenzi huo utaanza lini.


Akijibu hoja hiyo,Meneja wa Tanroad Mkoa wa Mara, Emmanuel Koroso alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha barabara hiyo inaanza kujengwa ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani  ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010.


“Ndugu wajumbe sisi Tanroad tunatekeleza sana Ilani ya CCM,tunawahakiksihia kuwa barabara zote zilizosemwa kwa mujibu wa Ilani zitatengenezwa”.Alisema Koroso, huku akishangiliwa na wajumbe.



Msimamizi wa Ubora wa Maji Mkoa wa Mara, Mathayo  Athuman akitoa ushauri kuwa ni vyema mikataba yote iseme wazi kuwa mchimbaji (Mkandarasi) atalipwa baada ya kuwachimbia wananchi kisima chenye maji ya kutosha na atakayechimba afanye kazi zote ikiwemo ya kutafuta maji ,kuchimba kisima na kujenga miundombinu ya maji ingawa gharama yake ni kubwa lakini bora kuwa na visima vichache vyenye maji kuliko kulipia gharama za uchimbaji hata pale ambapo maji hayakupatikana.

No comments:

Post a Comment