Wednesday, October 26, 2011

MTOTO MCHANGA ATUPWA AKUTWA HAI.

MUSOMA.


MTOTO Mchanga wa jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa wa wiki mbili ,Agosti 25 ameokotwa akiwa ametupwa kwenye korongo katika Mtaa wa Mtakuja na Zanzibar, kata ya Mwisenge,kikiwa kimetupwa na mtu asiyejulikana.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishina Msiadizi wa Polisi (ACP),Robert Boaz alisema kuwa mtoto huyo amegunduliwa na watoto wa shule ya Msingi wa Tatu Issa (32) walipokuwa wakipita kwenye korongo hilo wakielekea shuleni na ndipo waliporudi nyumbani kumpatia taarifa Mama yao.

Alisema Mama huyo alimkuta mtoto huto akiwa mtupu na alikuwa hai ,ndiopo alipotoa taarifa kwa Polisi,mtoto huyo amehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara iliyoko katika Manispaa ya Musoma.

Aidha ametoa wito kwa watu ambao wanahisi kuna mama alikuwa mjazito na hana ujauzito watoe taarifa kituo cha Polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Katika tukio jingine lililotokea katika wilaya ya Bunda, majira ya saa 10 jioni stend ya Mabasi, mtoto mchanga wa jinsia ya kiume wa Chausiku Kelaryo( 21), mwenye umri wa wiki moja na nusu ameibiwa.

Alisema Chausiku alimwachia Mama mmoja asiyemfahamu kumshikia ili akanunue mboga sokoni, kutoka sokoni akakuta mama huyo ametoweka na mwanae.

Ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya hiyo kama kutakuwa na utata juu mama huyo na kwamba hakuwa na ujauzito watoe taaifa kituo cha Polisi ili hatua dhidi ya mama huyo zichukuliwe.

NOTI BANDIA ZAKAMATWA



MUSOMA.

JUMLA ya noti bandia zipatazo 16 za Sh 10,000 na Sh. 5,000 zipatazo 12 zimekamatwa katika Manispaa ya Mji wa Musoma.


Akizungumza na Mwandishi wa habari hii ofisini kwake Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Mkoa wa Mara, Robert Boaz alisema tukio hilo limetokea Agosti 24 mwaka huu katika mtaa wa Jamatini majira ya saa 2 usiku katika Super Market ya Msendo wakati mteja akinunua vocha ya Sh.5,000.

Alisema baada ya kuugundua si noti halali alipiga simu kwa askari wa doria na kumkamata mtuhumiwa aliyemtaja kuwa Mashaka Samson, mkazi wa Musoma Mjini mtaa wa Karume.

Kamanda Boaz alisema noti hizo zilikuwa na namba tofauti tofauti ambapo noti zipatazo nane za Sh.5,000 zilikuwa na namba aina moja AA 084 598 na nne zikiwa na namba ADO 845 927, noti za 10,000 zilikuwa nne , tatu zikiwa na namba BB 0315203 na moja ikiwa na namba BC 031 5209.

Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu mashitaka.


Saturday, October 22, 2011

VIONGOZI WA MWENGE 2010


Mkimbiza Mwenge kitaifa, Nassoro Ally Matuzya akifuraia mara baada ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

KAMPUNI YA SIMU TANZANIA YAHUJUMIWA.

MUSOMA.



KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Mara imehujumiwa kwa kukatiwa mikongo ya simu yenye urefu wa Mita 4,000 na wananchi wasio wema na kusababisha hasara kubwa ya Mamilioni ya fedha kwa kipindi cha miezi sita.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa na Mwandishi wa habari hii ofisini kwake wakati wa mahojiano, Meneja wa kampuni hiyo, Richard Augustine alisema ingawaje kampuni inajitahidi kutoa huduma nzuri kwa wakazi wa Mji wa Musoma na Tarimr lakini inakubiliwa na changamoto mbalimbali.

Alisema kwa sasa wakazi wa kata za Bweri machinjioni na Rwamlimi na Wilani Tarime ambao wanakosa huduma hiyo muhimu majumbani kwao kutokana na tatizo hilo ambalo limeipatia kampuni hasara ya kiasi cha Sh Milioni 50.

Aliongeza kuwa ukaratabati wa miundo mbinu ya kupitisha maji, barabara imekata baadhi ya mikongo maeneo ya kiwanda cha Nguo cha Mutex suala ambalo linashughulikiwa ili kiwanda hicho kiweze kuendelea kupata huduma.

“Suala hili la ukarabati wa barabara na upitishaji maji ni lazima tuwe tunashirikiana ili kuepuka gharama zingine zisizo za lazima, pia suala la ushirikiano baina ya vyombo vya dola na kampuni yetu ni jambo la msingi sana ili kuhakikisha vitendo vya namna hii vinatokemea,kwani wahujumu hawa wanafahamika na wengine tumekuwa tukiwakamata na ni wezi sugu wanafahamika”Alisema Richard.

Akizungumzia kuhusu kutanua wigo wa mtandao alisema kampuni ina mkakati huo kwani kwa sasa huduma ya simu ya mkononi ya TTCL Mobile haifiki maeneo mengi ukilinganisha na kampuni zingine, sanjali na mtandao wa Broad band ambao kwa sasa watumiaji wengi wamekuwa wakifahidika nayo.

Akizungumzia juu ya kupanda kwa gharama za umeme alisema gharama zimekuwa kubwa kulinganisha na awali ambapo huduma hiyo ilikuwa ikipatikana,haipungui japo kuwa kuna mgao na kwa maeneo mengine yameathiri utendaji kwa kampuni hiyo, kutokana na matumizi makubwa ya mafuta kwenye generator, huku Ankara pia zikipanda.



“Nilifikiri gharama zitapungua kutokana na mgao wa umeme,lakini cha ajabu tumekuwa tukitumia mafuta kwa wengi tukijua Ankara za Tanesco zitapungua lakini imekuwa kinyume zinakwenda sambamba” Alisema Richard kwa mshangao.


UWEKAJI MAMBOMBA YA MAJI WAKWAMA

BUNDA.

MKANDARASI ambaye alikuwa aanze kazi ya ujenzi wa miundo mbinu katika Mradi wa Maji wa vijiji vya Mugeta na Nyang’aranga katika Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara hajaanza kazi hadi apatikane mtaalamu mshauri wa Mkandarasi.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hii, Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Bunda, Tanu Deule alisema kuwa limetolewa agizo kutoka Wizara ya Maji jijini Dar es Salaam kuwa huduma ya kutandaza mabomba isitishwe kwanza hadi atakapopatikana Mtaalamu MShauri wa Mkandarasi huyo.

Jiwe la Msingi la Ujenzi wa mradi wa maji wa Mugeta na Nyang’aranga katika Wilaya ya Bunda liliwekwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa na ziara yake ya kikazi Mkoa wa Mara ulitarajiwa kuanza septemba mwaka huu.

Mradi wa maji wa vijiji vya Mugeta na Nyang’aranga umebuniwa ili kusaidia wananchi wapatao 5,000 wa vijiji hivyo kuondokana na adha ya kutafuta maji yasiyo salama kwenye umbali mrefu.

Lengo ni kuwawezesha wapate maji safi na salama karibu na makazi yao ili waweze kuwa na afya bora na kutumia muda wao kwa shughuli za maendeleo na kuboresha mahudhurio ya wanafunzi shuleni.

Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Bunda Tanu Deule alisema Mradi huo unahusisha uchimbaji wa kisima kirefu cha maji chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa, ujenzi wa bomba kuu la kupeleka maji kwenye tanki umbali wa kilomita 1. 982, ujenzi wa mtandao wa mabomba kilomita 31.158 ya kusambaza maji kwa watumiaji, Ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji, ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 100,000, kuweka mfumo wa umeme kwenye kisima cha maji, Ujenzi wa nyumba ya pampu na usimikaji wa pampu ya kusukuma maji.

Mradi huo unajengwa kwa ubia kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japani kupitia mfuko wa “Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund (FACF) ulio chini ya Wizara ya Kilimo na Chakula.

Mradi unakadiriwa kugharimu jumla ya Tsh 270,000,000,Serikali ya Japani (J FACF) itatoa Tsh 240,000,000,Serikali ya Tanzania kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Bunda itatoa Tsh 23,000,000 ,Wananchi watachangia nguvu zao sawa na Tsh. 7,000,000

Mpaka sasa Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha Tshs 107,000,000 kutoka Serikali ya Japan na Tshs 90,778,809 zimetumika, na Halmashauri imekwisha toa Tshs 3,000,000.

Aidha Kazi ambazo tayari zimekwisha kufanyika ni pamoja na uchimbaji wa kisima kirefu na Ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 100,000 kwenye nguzo ya urefu wa mita 10 katika kijiji cha Mugeta.

Sanjali na hilo kuna kazi ambazo bado hazijafanyika ikiwa ni pamoja na kununua mabomba na kuyalaza kwenye njia kuu na njia ya kusambaza maji kwa watumiaji, kuvuta umeme hadi kwenye kisima cha maji, kununua pampu na kuisimika na kujenga nyumba ya pampu.


Monday, October 17, 2011

UZINDUZI WA MWENGE MKOANI MARA.





MUSOMA/SERENGETI.

MBIO za Mwenge wa Uhuru Mkoani Mara zimemaliza vyema kwa kuweka mawe ya MSingi na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mtumwa Rashid Khalfani katika Wilaya mbili za Musoma vijijini na Serengeti.

Akisoma risali ya Utii, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa alisema Mwenge wa Uhuru na Miaka 50 ya Uhuru imefungua nyumba mbili za walimu katika shule ya Sekondari ya Osward Mang’ombe na Jengo la OPD Zahanati ya Masurura za Butiama,Wilaya ya Musoma Vijijini zilizogharimu jumla ya Sh 364,740,500.

Aidha Mwenge wa Uhuru umepitia miradi minne yenye thamani ya Sh. 207,619,980 na Mradi wa Soko la Musati na Ujenzi wa shule ya Msingi Mapinduzi ‘B’na Zahanati ya Park Nyigoti na ofisi ya kijiji cha Robanda ilizinduliwa.

Mwenge wa Uhuru 2010 Wilayani Serengeti ulipitia miradi mitatu hadi kukamilika kwake ilikuwa na thamani ya Sh. 201,516,729.89 na kufunguliwa.

Aidha ujenzi wa nyumba mbili za walimu Shule ya Sekondari Osward Mang’ombe uligharimu jumla ya Sh. 300,000,000 kati ya hizo Mchango wa Mbunge wa jimbo Nimrode Mkono ukiwa ni Sh. 274,000,000.

Ujenzi wa jengo la Zahanati ya Masururla umegharimu kiasi cha Sh. 64,740,500, soko la Musati limegharimu kiasi cha Sh. 35,000,000, ujenzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi ‘B’ Sh. 75,000,000,Zahanati ya Park Nyigoti ambayo ni guvu kazi ya wananchi wenyewe kupitia ruzuku kutoka halmashauri ni Sh. 34,955,980 na Ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Robana umegharimu Sh.62,664,000 zikiwa ni nguvu kazi.



Alisema kuwa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2010 umeendelea kutekelezwa kwa mapambano dhidi ya Malaria na kwamba maambukizi ya malaria yamepungua toka asilimia 49 mwaka 2009/2010 hadi Asilimia 35 mwaka 2010/2011 Wilaya ya Musoma.

Wilaya ya Serengeti maambukizi ya Malaria yamepungua toka 48.9 asilimia sawa na watu 24,496 mwaka 2009/2010 hadi asilimia 27 sawa na watu 50,818 mwaka 2010/2011 na kusababisha kupungua kwa vifo toka 137 kwa mwaka 2009/2010 hadi vifo 97 mwaka 2010/2011.

Wilaya ya Musoma vifo pia vimepungua kutokana na malaria toka vifo 59 mwaka 2009/2010 hadi vifo 42 mwaka 2010/2011, jtihada za makusudi zinahitaji kwani bado muamko wa kutumia vyandarua kwa baadhi ya wanannachi ni changamoto kubwa ambayo inahitaji kutiliwa pamoja na kwamba serikali imetoa vyandarua vyenye dawa(viuatilifu) 154,591 na Wilaya ya Serengeti vyandarua 115,816.




Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru umezinduliwa Mkoa wa Mara kijiji cha Mwitongo, Butiama mahali alipozaliwa Baba wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere na maadhimisho ya miaka 12 tangu kifo chake ambapo mara baada ya kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru na Makamu wa Rais, Dk Mohammed Bilal na Mwenge wa Mwitongo,Mvua kubwa ya ghafla ilinyesha.

Thursday, October 13, 2011

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KANUNI ZA FILAMU

MUSOMA.



WAMILIKI wa Filamu Tanzania wamepewa siku 90 za marekebisho ya filamu zao vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.



Agizo hilo limetolewa mbele ya Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharibu Bilal na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi, wakati wa uzinduzi wa kanuni za sheria ya filamu na Michezo ya kuigiza za mwaka 2011 zilizofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji wa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Alisema zipo filamu nchini Tanzania ambazo hazina maadili kwa watanzania na ni hatari kwa vizazi vijavyo.



Aliongeza kuwa Serikali baada ya kutumia Sheria ya picha za sinema(Ordinance Cap 230) kwa takribani miaka 46 iliona kuna umuhimu wa kuwa na sheria inayoilenga mazingira na hali halisi ya kitanzania,hivyo ikaona umuhimu wa kutunga Sheria mpya, yaani Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na.4 ya mwaka 1976 yenye ni ya kuulinda utamaduni wa kitanzania na kuhakikisha Watanzania wanapata hurudani stahiki zinazofuata taratibu zilizowekwa na zinazozingatia maadili.



Akizindua kanuni hizo, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Bilal alisema kuwa alisema Serikali inadhamini na kutambua mchango unaotokana na tasnia ya filamu,ambapo Rais Jakaya Kikwete wakati anahutubia Bunge alizungumzia dhamira yake ya dhati katika kuimarisha tasnia hiyo ya filamu.
Pia serikali kupitia bajeti yake ya mwaka 2009/2010. Ilitoa unafuu kwa kupunguza kodi katika uingizaji wa vifaa kama kamera kwa ajili ya kutrngrnrza filamu ili kuwapatia ajira wasanii wa tasnia hiyo na hatimaye waweze kuchangia na kukuza Uchumi,sanjali na kuandaa sera, Sheria na miongozi inayosimamia tasnia hiyo.



Alisema kuwa kanuni hizo zilizozinduliwa zinawakumbusha wadau wa Filamu na michezo ya kuigiza kwamba tasnia hiyo inasimiwa na Sheria na kwamba hamna budi kuhakikisha filamu na Michezo ya kuigiza zinazotengenezwa nchini nza zinazoingizwa toka nje ya nchi zinawiana na mila, desturi na maadili ya Tanzania.




“Lakini nikiri pia zipo filamu na michezo ya kuigiza ambazo kwa kweli zinalinda maadili, zinatangaza nchi yetu na zinatoa pato kwa wasanii, lakini ni chache sana,na kazi nyingi za filamu na michezo ya kuigiza hziwanufaishi kw akiwango stahili,wasanii wa tasnia hio wala kuliingizia Taifa pato stahiki,hivyo wadau wa filamu hawana budi kuhakikisha kazi zao zina viwango vya hali ya juu na zinachangia katika kumkomboa na kumpa msanii pato stahuki na zinachangia pato la Taifa” Alisema Gharibu.



Aidha akitoa mfano wa nchi ya Marekani, Makamu wa Rais,Dk. Mohammed Gharibu Bilal alisema wasanii wa nchi hiyo wanachangia pato la Taifa kwa fani za muziki na filamu kwa kiasi kikubwa,ambapo India iko katika kundi la nchi zinazoendelea.



Tasnia ya Filamu na Televisheni huiingizia zaidi ya Dola Bilion 6.1 na imetoa jumla ya ajira 571,000 mwaka 2008,huko Uingereza ikiingiza zaidi ya paundi 4.5 Bilioni takribani Sh. trioni 9 katika uchumi wa nchi hiyo,hata Tanzania inawezekana endapo fursa zilizopo zitatumika vizuri.




Aidha amemwagiza Wzairi huska kuhakiksiha inaimarisha Bodi kuu ya filamu, Bodi za Mikoa na Wilaya kw akushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), na kuhakikisha kanuni zilizozinduliwa zinawafikai wahusika wote na kupanga namna ya kuzitekeleza mapema ili zitoe matokeo chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Uzinduzi huo ulihudhuriw na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fennella Mukangara, Mkuu wa Mkoa wa Mra John Tupa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda, Mwenyekiti wa Bodi ya filamu, Rose Sahoye na watumishi wa Wizara na Asasi zake.