Saturday, October 8, 2011

SHAMRA SHAMRA BUTIAMA ZAANZA KWA MICHEZO

SHAMRA SHAMRA za miaka 50 ya uhuru zinaanza kesho (leo) kwa kuanza na
michezo mbalimbali katika kijiji cha Mwitongo (Butiama) mahali
alipozaliwa muasisi wa Taifa hili, Hayati Baba wa Taifa, Julius
Nyerere.


Blog hii inamulika matukio ambalimbali yakiwemo ya maonyesho ya vibanda kutoka Wizara ya habari, vijana Utamamaduni na michezo pamoja na kumalizika kwa
mafunzo ya michezo kwa walimu wa michezo wa shule za Msingi sekondari
na viongozi wa riadha.
Akizungumza katika kiwanja cha mazoezi mara baada ya kumalizika kwa
mafunzo hayo, wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Baraza la Michezo la
Taifa, Mohammed Kiganga alisema kuwa mafunzo hayo yalikuwa na lengo la
kuwapa uzoefu walimu wa michezo, ambayo ni program ya Taifa kwa Mikoa
yote nchini.


Naye mwezeshaji mwingine, Richard Mganga alisema kuwa katika mafunzo
hayo mada mbalimbali zilitolewa zikiendana na mazoezi makali ambayo
mara baada ya darasa wadau hao uanza michezo kwa vitendo(Theory and
Practical) .


Mganga alisema Michezo itakayochezwa ni mipira wa miguu, Netball,
Riadha mbio fupi, mashindano ya baiskeli, Mchezo wa bao ambao mwasisi
wake ni Hayati Mwalimu Julius Nyerere na michezo mbalimbali ya watoto.
Katika semina hiyo mada mbalimbali zilitolewa ikiwa ni pamoja na
Ukimwi na michezo, Netball, Nyanja za michezo,sheria za soka, stadi za
mpira wa miguu ambapo mwezeshaji, Richard Kiganga aligusia namna ya
kutengeneza viwanja vya mpira wa miguu, riadha na netiboli na sheria
za mpira wa miguu.


Wahitimu hao ambao watapewa vyeti hapo baadae ni kutoka shule za Msingi za, Kigera, Nyegina ziliyoko
manispaa ya Musoma, Makore, Mkiringo, Kwibara, Bukumi,Suguti, Seka,
Mirwa na Nyambono ‘B’.shule za sekondari ni Mmazami, Masaba,Kyanyari,
Rusoli, Makojo, Mugango, Kiagata, Bumangi, na Buhemba, na viongozi

No comments:

Post a Comment